Habari zenu za usiku huu wanajamvi,
Ni hivi mimi nina My girlfriend wangu ambaye teyari ana mtoto na jamaa mwengine,ila huyu mtoto wake hajatulia kwa kweli na huyu mama yake simuoni kuchukua hatua zozote kuhusu hilo anamdekeza sana bana mie inaniuma lakini nikumuambia anasema mie silipendi kinda lake hilo,
Siku moja nilikwenda na rafiki yangu kumtembelea yaani ilikuwa ni aibu mara kamsachi huyo rafiki yangu,mara kutoka nje kaanza kurusha mawe ndani,mara kachukua chupa ya konyagi tuliyokuwa tunakunywa na kupiga fundo moja,yaani ni maudhi kwa kweli kwenda kumtembelea na hata anapotaka kuja kunitembelea akiniambia anakuja na hilo kinda lake binafsi nakosa raha najua lazima atanitia aibu/hasara ya kuvunja vitu,
Kuna cku uzalendo ulinishinda nikamuambia kuwa huyu mtoto wako kwa kweli mie siikubali tabia yake yaani umemlea kama yai unaogopa lisipasuke,basi adhabu niliyopewa ni kunyimwa uroda miezi mitatu.
Naomba ushauri wenu wana jamvi nimfanyeje mama yake ili amrekebishe huyu mtoto wake?