Mtoto wa ndugu yangu kakoswa koswa kutekwa na watekaji wa watoto

walikuyu

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2018
Posts
934
Reaction score
1,981
Habari za usiku wakuu!

Jamani juzi kati hapa kuna mtu alipost uzi fulani kuhusiana na tatizo la utekaji wa watoto baadhi ya maeneo ya dar es salaam. Leo almanusura tumpoteze mtoto wa ndugu yetu, tukio lilitaka kutokea maeneo ya kimara matosa, mtoto aliitwa na watu wasiojulikana walikuwa kwenye noa nyeusi tinted mtoto aliambiwa akachukue pipi lakini mtoto alisita akakimbia, ivyo ndio ikawa pona pona yake.

Ivyo naomba niwaombe wazazi na walezi tuwe makini sana na watoto wetu.

Niwatakie usiku mwema.
 
makafara ya uchaguzi mwakani hayo. mashetani kabisa hawa. Mungu ataumbua watu wakubwa tu siku si nyingi.
 
Daah Mungu anasaidia TU maana leo nimekutana na mtoto wa darasa la kwanza kanapita porini peke yake umbali wa kilomita tano hv
Eneo ni hatari kuna Nyati na tembo smtms hakuna makazi ya watu wala wapitanjia!

Nilikapa lift, niliwaza mbali sana kwa jinsi dunia watu wamekuwa wanyama.... Kufika kakashuka na kusema "asante Mungu akubariki"

Wazazi tulinde watoto wetu, hasa pia mida ya kutuma dukani usiku ni hatari, bora uende mwenyewe tu
 
Daah Mungu anasaidia TU maana leo nimekutana na mtoto wa darasa la kwanza kanapita porini peke yake umbali wa kilomita tano hv
Nilikapa lift, niliwaza mbali sana kwa jinsi dunia watu wamekuwa wanyama....

shida ukimpa lift watu wengine wanawezadhani ndio unamteka, ukapopolewa na mawe na kuchomewa gari yako kabisa. unampandishaje kwenye gari mtoto usiyemjua?
 
Hii hali mbona sio nzuri, mamlaka zinasema chochote kweli?
 
Zamani nilikuwa nawashangaa wazungu wanawafundisha watoto wao wasiongee wala kuwajibu strangers
Baadae nikajua umuhimu wake
Na mimi nikawafundisha watoto
Hata umuitaje kama hakujui imekula kwako
Wazazi na hata mliomo humu bila watoto jaribuni kuwafundisha watoto wasiongee wala kuwaitikia wasiowajua hata wapepe box la pipi
Watoto huku hawapewi kitu
Kama ni sumu au ana allergy
Kweli sisi tuko tofauti kwa sababu ya upendo lakini mambo yamebadilika sana siku hizi
Hakuna kumuaminia mtu mtoto na ajue hakuna cha anti wala anko
 
Daah Mungu anasaidia TU maana leo nimekutana na mtoto wa darasa la kwanza kanapita porini peke yake umbali wa kilomita tano hv
Nilikapa lift, niliwaza mbali sana kwa jinsi dunia watu wamekuwa wanyama....
Wazazi tulinde watoto wetu, hasa pia mida ya kutuma dukani usiku ni hatari, bora uende mwenyewe tu
Duh mungu mwema sana sipati picha angekutana na majambakuzi aya ingekuwa stori nyingine
 
Daah Mungu anasaidia TU maana leo nimekutana na mtoto wa darasa la kwanza kanapita porini peke yake umbali wa kilomita tano hv
Nilikapa lift, niliwaza mbali sana kwa jinsi dunia watu wamekuwa wanyama....
Wazazi tulinde watoto wetu, hasa pia mida ya kutuma dukani usiku ni hatari, bora uende mwenyewe tu
Inasikitisha sana
 
Hii hali mbona sio nzuri, mamlaka zinasema chochote kweli?
Amna kitu kabisa kwa hari ilivyo mbaya serikali ingetoa neno lolote lakini mpaka sasa kimya
 
  • Thanks
Reactions: Lax
shida ukimpa lift watu wengine wanawezadhani ndio unamteka, ukapopolewa na mawe na kuchomewa gari yako kabisa. unampandishaje kwenye gari mtoto usiyemjua?
Ni hatari kweli, niliumia nafsi kuona yuko mwenyewe eneo hilo, ni mbuga ambapo smtms kuna tembo au nyati ambao ni hatari mnoo
Hakuna makazi ya watu, wapita njia ni nadra Sana!!
Wazazi wengine hawathamini usalama wa watt wao
 
Back
Top Bottom