Mtoto wa Rais Samia, Abdul ana cheo gani Serikalini/Wizara ya Nishati hadi akutane na Rais Museveni?

Wana nongwa!
 
Kuna wizi gani hapo?

Au unajiskia tu raha kutamka neno Wizi?
Kama hujawahi kuona/kusikia utajiri wa Viongozi wetu basi wacha tukae kimya.

Kwani zile mambo ya Richmond, Epa, Iptl, Kagoda, Ndege ya Rais zilikuwa ni nini kama sio Wizi?

Hayo mambo ya ununuzi wa ndege mtumba kwa hela za mpya ni nini kama sio Ufisadi huo.

Vipi kuhusu Vichwa vya Treni?

Mkuu, Viongozi wa Nchi hii ni wezi period
 
Hayo yote uliyoyasema hapo yanahusianaje na Rais Samia? Ameiba nini? Lini na wapi?
 
Hayo yote uliyoyasema hapo yanahusianaje na Rais Samia? Ameiba nini? Lini na wapi?
Kwahiyo awamu hii tumepata Malaika anatuongoza Watanzania?

Umeulizwa hapo Juu, kama huyo Mtoto wa Rais hajawa Muajiriwa wa Serikali, ameenda huko Uganda kama Nani?

Kama ameenda kama Mfanyabiashara, vipi amepata wapi mtaji wa hizo dollar Milioni 1 katika Umri huo wa chini ya miaka 45?
 
Samia asipokuwa mwangalifu,huyu mwanae yatakuja kumkuta kama yaliyomkuta Mtoto Marehemu Rais Dos Santos wa Angola.Binti alikuwa anapiga dili kwa mgongo wa Baba yake akiwa Rais,baada ya Baba yake kuondoka madarakani ndipo alipoionja joto ya Jiwe!
 
Umeona shida yako?

Hata umesahau ulisemaje!! Ulimsema Samia kuhusu wizi na umeshindwa kuthibitisha. Alafu bado unaendeleza ujinga wako.

Mtoto wa Samia ni mfanyabiashara na ameenda kwa mambo yake binafsi ya kibiashara kuzalisha umeme wa jua hapo Uganda.

Siku hizi kuna mikopo ya bank unakopeshwa kufanya uwekezaji. Hela sio lazima utoe mfukoni

Huo wizi uko wapi hapo?
 
Labda ni rafiki yake...
 
Wewe ndiyo mpumbavu,Mtoto wa Museveni ni Mkuu wa Jeshi gani?Museveni alimuondoa Jeshini muda sana baada ya kuona anafanya vitendo vinavyomuaribia katika utawala wake.
 
Sawa Mkuu

Uwe na jioni njema

Wacha tuinjoi nyama choma na Beer siku zikisogea 🍗🍺
 
Sasa katiba ipi ivunjwe? Kwani hana haki ya kwenda Uganda? Kwani uliambiwa kaiwakilisha serikali kwenye jambo lipi?

Kama kachukuliwa kwa mkataba fulani?


Huu mwengine ni ujinga hata kuujadili.


Wewe kama huna, huna tu.
Ila mwambie Samia kuwa ata Mtoto wa Rais wa Angola Marehemu Dos Santos Binti yake alikuwa anapiga dili za mafuta kupitia mgongo wa Baba yake,baada ya Baba kuondoka madarakani serikali ya Angola imemburuza kortini na Mahakama imeamuru Isabel Dos Santos arudishe Dola milioni 500 alizopiga kwenye Shirika la Nishati la Angola maarufu Sonangol!
 
Tulisema lengo la kuuza Bandari ni biashara haramu. Aliye jirani na Museveni amshitue tutakuwa kama Kenya kuleeee karibu na mpaka wa wapenda vita…
East Africa inatengeneza bomu la nuklia kupitia Tanganyika
 
Labda ana ajira hapo wizarani ..ni mtanzania kuajiriwa ni haki yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…