Mtoto wa Rais Samia, Abdul ana cheo gani Serikalini/Wizara ya Nishati hadi akutane na Rais Museveni?

Sioni shida akifanya biashara halali
 
Sioni shida akifanya biashara halali
Majuzi Rostam Aziz katangaza anawekeza $100m Zambia kwenye LPG umeona kazua mjadala wowote, si kila mtu anaelewa ni mfanyabiashara ata kama alianza kama fisadi.

Sana sana kilichozua mjadala siku hiyo aliposema majaji watanzania ni wakupigiwa simu, lakini hakuna aliezungumzia uwekezaji wake.

Same Bakhresa, Sawaya, Mo Dewji na matajiri wengine tukisikia wana mpango wa kuwekeza $25m million sehemu hiyo wala sio habari; wanajulikana ni wafanyabiashara matajiri, shughuli zao rasmi zinajulikana na wanakopesheka ata bank zilizopo nje ya Tanzania.

Shida sio mtoto wa raisi kuwekeza, shida ni hizo hela anatoa wapi; hawana historia ya utajiri kwenye familia yao.
 
Tulisema lengo la kuuza Bandari ni biashara haramu. Aliye jirani na Museveni amshitue tutakuwa kama Kenya kuleeee karibu na mpaka wa wapenda vita…
East Africa inatengeneza bomu la nuklia kupitia Tanganyika
Umeandika upuuzi mtupu. Unaweza kuweka ushahidi wowote wa maandishi unaoonyesha bandari kuwa imeuzwa?.
 
Tumerudi kulekule, wahuni wameanza kuhuni nchi
 
Tutamkumbuka mpka akili zitukae sawa,kila nafsi itataja jina lake. Ngojea tuwekwe sawa kwanza.
 
Huyu mtoto wa rais ni kwamba anafundishwa kazi za biashara za kimataifa baina ya Tanzania na mataifa mengine na mwalimu wake ni Rastam.
Hata hii DP world watakuwa wana shea ya kifamilia na ndio maana mkataba ulikuwa wa kimya kimya bila kumhusisha mwana sheria wa serikali.
Mwana sheria wa serikali hakuwa na habari ya kile kilichokua kinaendelea bungeni wakati wa kipitisha mkataba maana tuliona hakutoa mchango wowote.
Bahati mbaya nchi ina usalama wa watawala na sii usalama wa taifa.
 
Hela za kuwekeza lazima zitoke mfukoni kwake? Hakuna benki zinakopesha? Hakuna partnership anaweza fanya na watu wenye mitaji?

Maswali yako hayana msingi. We unataka kujua watu hela wanapata wapi watafute binafsi wakueleze sio unatuletea maswali ya kimaskini hapa. Au nikuulize wewe hapa hela zako unapata wapi?
 
Wapi imesemwa mwanasheria wa serikali hakushirikishwa mkataba wa DP World?
 
Mnajisumbua!

Nchi hii siku hizi uongozi ni wa kurithi. Ni mwendo wa ufalme na umalkia tu! Mfumo ushabadilishwa kitambo! Na ndomana wakaibuka (walamba asali)

Endeleeni kupiga kelele.
 
Wewe una historia ya kuingia JF kwenye familia yako?
 
Kwa hicho lingine Magu alisema ni kichaa tu anayeweza kufanya mambo ya hovyo akiwa ikulu
 
Watanganyika tusipisimama hizo familia zimeshaganya cartel ndani ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…