Mtoto wa Rais Samia, Abdul ana cheo gani Serikalini/Wizara ya Nishati hadi akutane na Rais Museveni?

Mlishazoea uongo na upotoshaji tu .unajiandikia tu hapa hata bila aibu wala ushahidi wa aina yoyote ile.pambana kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa uone kama huta fanikiwa kimaisha ,chapa kazi acha wivu na umbea umbea tu wakuandika maneno ya uongo uongo tu hapa
 
Huyo ni mfanyabiashara na yupo Uganda kwa mambo ya biashara zake. Wewe kinakuuma nini?

Museveni ameidhinisha mradi wa kampuni yake wa kuzalisha umeme wa Jua tena huko huko Uganda ! Wewe kinakuuma nini?

Tangu lini shughuli binafsi za mtu zikawa shughuli za ikulu?
 
Kijana anapiga dili za first class.... kwa namna alivyo pose kwa ile picha na Museveni ile ni high protocol!!

Uzuri hawa 'wenzetu' huwa hawana aibu wakati wa kula... huwa tayari hata kugombania sinia ya pilau pale inapobidi!
Ulitaka akae amechuchumaa ? Mawazo mengine ni ya kijinga sana
 
Nadhani ni wazi sasa, anayoyafanya Doto magari kule mtandaoni NDIO uhalisia wa UCHAWA unaonekana hapa.

"Huna baya, ukifa hauozi, hujawahi kulala njaa, siti yangu mbinguni chukua wewe n.k"

Imagine, taarifa kutoka kwa raisi wa nchi, inayozungumzia maendeleo ya nchi, kwenye eneo fulani la nchi; UNAKUJA KUTUAMBIA ni biashara binafsi?

NImeona kuwa G55 ya raisi, sasa imezuiliwa kuwa tracked; unadhani ni kwasababu za kiusalama?

Kazi ipo.
 
Kha! Hutuba za Nyerere tena! Huu wakati wa Samia usiturudishe Nyuma bhana.
Alisema IKULU ni Mahali patakatifu, hawa wanapageuza pango la wanyanganyi Hadi mtoto asiye na qualificatn yoyote anawakilisha IKULU.

Ndomana zimefutwa kumbe HOTUBA za Mwl Nyerere!!!
 
Uchawa gani?

Wewe ukiwa Rais inamaanisha mtoto wako hapaswi kujihusisha na jambo lolote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…