Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
❤️🧎Kwanza kwanini umuache mtoto aende kucheza kwa jirani?? Ukiachana na unyanyasaji wa kingono kuna mambo mengi yanaweza kutokea utamlaumu nani
1. Kuna mama alimruhusu mtoto akacheze kwa jirani watoto wanacheza bila uangalizi akatumbukia kwenye shimo la choo baadae anaenda kumwita aje kula wenzie wanasema aliingia mulee. Bahati mbaya mtoto alishapoteza maisha zamani.
2. Kuna watoto wengine ni watundu, anaweza kuwa sio wako bali hao wa jirani wakaharibu kitu mwanao ataunganishwa na kama sio kuangushiwa msala kabisa itakubidi ulipe.
3. Kuna mtoto alienda kucheza kwa jirani yule jirani anajishughulisha na kutengeneza sabuni za maji. Bahati mbaya aliacha michanganyiko yake ovyo ( kwake inaweza kuwa kawaida) mtoto yule alipoona akanywa aliugua kwa muda mrefu mwishowe alifariki dunia.
Kuna cases nyingi sana za aina mbali mbali, naamini kama mzazi ukiwa na ratiba ya mwanao nzuri atakuwa busy nyumbani hatawaza hata kwenda kwa jirani kucheza.
Sikuhizi hakuna, wote wafungiwe...fungia mtoto wakike Sio unafungia wakiume.utakuja kunishukuru.
ukilifungia Toto lakiume ujue unalea ndezi.hakikisha unajua michezo anayo cheza bas.Sikuhizi hakuna, wote wafungiwe...
Watu wamevurugwa...