Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Niliwahi kukaribishwa chakula kwenye familia fulani ya kishua nikapikiwa ugali na nyama ya mchuzi. Nikaona ili nifaidi vizuri lile chuzi nikawa kila nikimega tonge natumia dole gumba langu kupiga lile shimo katikati ya donge la ugali ili kuchota ule mchuzi. Kumbe kuna dogo wao wa miaka mitatu hajawahi kuona kile kitu. Basi aliponiona kakimbia kwenda jikoni akiita mama mamaa njoo uone mama yake kaja dining anamuulizia nione nini. Dogo karopoka mgeni anatengeneza kwa kutumia ugali kichoteo cha mchuzi. Niliona aibu acha tu.

[emoji23][emoji23][emoji119]
 
Mwanangu amekulia sehemu ambayo hakuna Waislamu hajawahi ona mtu akiwa amevaa yale sijui majuba au hijabu manguo meusi ya kufunika uso na mwili mzima.

Nilienda naye Morogoro kwa wazazi, asubuhi akakutana na mama wa kiislam Jirani yetu amevaa yale manguo. Naona mtoto kaja ndani spidi analia na kumuita Mama yake. Mamaaaaa kuna jini linakuja. Kidogo tunaona yule mama anakuja nyumbani. Dogo yupo chumbani amejifunika blanket. Ikabidi tuombe msamaha kwa yule mama maana alisikia na akawa amekasirika. Tukaanza muelekeza mtoto kwani alikuwa mtoto wa miaka 4 kipindi hiko.
Aisee!
 
Mimi wa kwangu alikuwa na miaka kama minne, so nilikuwa nikienda washroom anaipiga pombe yote kwenye grasi then anarudishia so mimi nikirudi sijui kama kaipiga ya kwenye grasi. Hawa watoto hawa
Nooma sana ,wanapenda pombe balaa,mama zao wanatulaumu sisi eti
 
Watoto ni balaa.
Kuna wazazi fulani walikua wanalala pamoja na watoto wao.
Usiku mkubwa wakiamini watoto wamelala wanaangusha godoro la spea wanafanya yao.
Kuna siku wakaulizwa " kwanini mnapenda kukandana hapo?" Next day ilibidi wahamishwe chumba.

Na kuna mmoja huyo alimshtaki baba ake kwa uncle wake.
" Uncle huyu baba ikifika usiku anampiga mama, baba anampandia juu mama, mama analia tuu"
Mama wa watu aliona aibu.

Kuna dogo mmoja yeye alienda kutoa siri ya maumbile ya babaake kwa watoto wenzake lakini na watu wazima wapo.

"Basi mie babaangu ana KOJO kubwa hiloo!"
Haifahamiki aliliona katika mazingira gani hilo KOJO.

Kuna moja hiyo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili, vitoto vya USWAZI vinacheza nje mtaani pao. Wapo kama wanne hivi, umri una range miaka 3 mpaka 4.
Kitoto kimoja cha kike kilikua kimevalishwa chupi tu hana nguo nyengine.
Nikakiona kitoto cha kiume kikimfunua chupi kuangalia kule ndani halafu vinacheka.
Njia mzima najiuliza vitoto vidogo vile vimejifunzia wapi mambo kama yale.?
 
Nagonga kimtindo Leo nimekakuta kimeikaribia nikakimbia nayo faster
Niliwahi gonga hako kasungura kesho yake niliamka natetema kama lile gari/mtambo wa kuvunjia rami, labda sababu sikuwa nimekula vizuri. Toka siku hiyo mimi na sungura hapana aisee
 
Tuliwahi kumtembelea jirani, tukaletewa soda hatujakaa sawa mtoto wake akaja na likikombe likubwa anaomba soda, ukimuwekea anaipiga tarumbeta anaomba tena, sio mtoto wangu ila nilihisi aibu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sure..

Comedy zao burudani sana.

Kuna mwamba wangu mmoja yeye anakimbiza vifaranga anavinyonga, yaani kuku akitotoa pale home inabidi wawekwe mbali nae.

Kosa umfunge kuku kamba asweze kukimbia utamkuta yeye anamchezea chezea shingo, nataka nije kumfundisha kuchinja kuku sabab naona ndo anapoelekea
Mfundisho kuwapenda kwa kuwalisha chakula na maji yeye akiwepo.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Tuliwahi kumtembelea jirani, tukaletewa soda hatujakaa sawa mtoto wake akaja na likikombe likubwa anaomba soda, ukimuwekea anaipiga tarumbeta anaomba tena, sio mtoto wangu ila nilihisi aibu.
Ungemkabidhi yote halafu ungetulia unamuangalia tu.
 
Back
Top Bottom