Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Kuna dada mmoja rafiki yangu,alinitembelea home, siku hiyo nilikua nipo na kabinti kangu , kana miaka mitatu .

Tukawa tupo mezani wote watatu wakati wa chakula cha mchana .

Baada ya kumaliza kula binti wa watu kabakiza chakula , akadai kashiba.

Kabinti kangu kakaropoka" icho chakula unamwachia nan? , unadhani baba yangu anapesa za mchezo" .

Duh niliona aibu sna ,sijui ayo maneno kayatolea wapi.
Sasa waonaje aibu wakati kaongea uhalisia?
 
Tuliwahi kumtembelea jirani, tukaletewa soda hatujakaa sawa mtoto wake akaja na likikombe likubwa anaomba soda, ukimuwekea anaipiga tarumbeta anaomba tena, sio mtoto wangu ila nilihisi aibu.
Mi vitoto kama hivyo navikazia jicho tu
 
Unapokuwa mgeni hasa kwenye nyumba yenye mtoto ni vyema kuwa makini sana....

Jamaa mmoja alienda ugenini sasa akawa ameketi sebleni wanaangalia TV sasa jamaa remote ilikuwa pembeni yake akaamua kuichukua abadili channel..pembeni alikuwa mtoto wa mwenyeji wake akaanza kumuuliza jamaa, "Wewe si mgeni?, Si umekuja saivi tuu? Mbona unatumia remote kama vile ni yako?"

Jamaa aliona aibu sana yani....
Mtoto alimjibu vizuri kabisa, hakuwa na kosa kabisa
 
Sure..

Comedy zao burudani sana.

Kuna mwamba wangu mmoja yeye anakimbiza vifaranga anavinyonga, yaani kuku akitotoa pale home inabidi wawekwe mbali nae.

Kosa umfunge kuku kamba asweze kukimbia utamkuta yeye anamchezea chezea shingo, nataka nije kumfundisha kuchinja kuku sabab naona ndo anapoelekea
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwanangu amekulia sehemu ambayo hakuna Waislamu hajawahi ona mtu akiwa amevaa yale sijui majuba au hijabu manguo meusi ya kufunika uso na mwili mzima.

Nilienda naye Morogoro kwa wazazi, asubuhi akakutana na mama wa kiislam Jirani yetu amevaa yale manguo. Naona mtoto kaja ndani spidi analia na kumuita Mama yake. Mamaaaaa kuna jini linakuja. Kidogo tunaona yule mama anakuja nyumbani. Dogo yupo chumbani amejifunika blanket. Ikabidi tuombe msamaha kwa yule mama maana alisikia na akawa amekasirika. Tukaanza muelekeza mtoto kwani alikuwa mtoto wa miaka 4 kipindi hiko.
Kafanya vzr sana
 
Sure..

Comedy zao burudani sana.

Kuna mwamba wangu mmoja yeye anakimbiza vifaranga anavinyonga, yaani kuku akitotoa pale home inabidi wawekwe mbali nae.

Kosa umfunge kuku kamba asweze kukimbia utamkuta yeye anamchezea chezea shingo, nataka nije kumfundisha kuchinja kuku sabab naona ndo anapoelekea
Kama nakuona ukiwa unamtizama mwamba anavyowachezea kuku

Hongera sana endelea kuenjoy na huyo mwamba muandalie kesho iliyo njema ili kesho aseme bila wazazi wangu mmi nisingekuwa hapa.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kitoto changu nilikipeleka hospital kuchek malaria sasa baada yakutoka hospital tukakaa bar flan jiran na hospital kumnunulia chips akawa anagonga pale mara siakaamza kulilia bia , eti nataka biaaa ,ninunulie bia nikawa nazuga pale muhudumu naomba malta huyu dogo malta anaitaga bia dogo likaanza sitaki hio nataka pombee kulikuza na wazee pale wakawa wananiona kama mpinga kristo halafu Chakushangaza sijawah kula gambe mbele yake na mama yake hanywi na kilikua na miaka miwili dah
Duu! Pole sana.
 
Mwenyewe mkuu sipendi mtu abakize chakula na kitupwe, unasema mapema kama ni kingi.......
Sitaki uharibifu watu wanalala njaa ujue. Una binti smart Kwa kweli
Mimi sina mzaha na chakula. Dogo alikuwa na tabia ya kula na kuacha chakula sasa hivi kaacha. Nikiona kaacha chakula, atakimaliza kwa lazima. Anavuta mdomo wee, lakini sasa hivi yuko powa.
 
Ila hii tabia ya mtu anajipakulia chakula mwenyewe halafu eti anakula nusu au robo anaacha huwa ni tabia mbaya sana.
Mbaya kweli. Ni ulimbukeni tu wa kibongo. Hawa wenzetu wanathamini sana chakula. Hata akienda hotel akila chakula kinachobaki anabeba. Mimi nikienda kula huwa nawaambia wapunguze maana siwezi kumaliza.
 
Mimi sina mzaha na chakula. Dogo alikuwa na tabia ya kula na kuacha chakula sasa hivi kaacha. Nikiona kaacha chakula, atakimaliza kwa lazima. Anavuta mdomo wee, lakini sasa hivi yuko powa.
Hongera Kwa malezi mkuu. Thamani ya bidii ya mtu kwenye utafutaji lazima iheshimiwe.
 
Wengjne mazingira yetu mgeni akiwepo hakuna mtoto atajipitisha mbele za wageni,

Na hiyo tabia ya kuropokaropoka watoto wwnu wanaiga kwenu wazazi na walezi,wafundisheni watoto kuwa na khaba si kila wanachokiona/kusikia ni lazima waongee,

aisee simpendi mtoto mropokaji,
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
Mimi sina mzaha na chakula. Dogo alikuwa na tabia ya kula na kuacha chakula sasa hivi kaacha. Nikiona kaacha chakula, atakimaliza kwa lazima. Anavuta mdomo wee, lakini sasa hivi yuko powa.
😂😂😂😂😂🚮
Screenshot_20231129_104759_WhatsApp.jpg
 
Mambo ya Watoto yanafurahisha sanaa....wakikua hawaamini ukiwapa story za mambo waliofanya wakiwa watoto
Kabisa Mkuu...
Watoto wana vituko sana...
Mimi huwa nacheka...Ni vile tu wangu wamekuwa sasa wameanza kuona na aibu...

Ila kipindi hicho nilikuwa nacheka mno vituko vyao..sasa hivi na'enjoy vituko vya watoto wa Majirani.
 
Back
Top Bottom