Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Kitoto changu nilikipeleka hospital kuchek malaria sasa baada yakutoka hospital tukakaa bar flan jiran na hospital kumnunulia chips akawa anagonga pale mara siakaamza kulilia bia , eti nataka biaaa ,ninunulie bia nikawa nazuga pale muhudumu naomba malta huyu dogo malta anaitaga bia dogo likaanza sitaki hio nataka pombee kulikuza na wazee pale wakawa wananiona kama mpinga kristo halafu Chakushangaza sijawah kula gambe mbele yake na mama yake hanywi na kilikua na miaka miwili dah
Hii ni chai. Mtoto wa miaka miwili, mwenye wazazi wasiokunywa bia/pombe mbele yake. Aone bia na alilie eti anataka pombe?
 
Mbona kuna mtoto wa jamaa yangu tuliemda naye benki akiwa na Baba yake. Alipowaona askari wana bunduki akaamza kulikia bunduki pale CRDB Mpanda. Kwani mzazi wake alikuwa na bunduki hadi dogo aliloe bunduki?
 
Mm nilienda kijijini issue za kulima, mtoto wa mwenyeji wangu ilipofika muda wa chakula akawa ananisukuma na kunivuta huku ananiambia "ondoka tule".

Kumbe bhana yule mwenyeji wangu alipika chakula alaf akakiweka ili nikiondoka ndo wale. Sasa yule dogo akakosa uvumilivu ikabidi anichane. Muda huohuo niliondoka na sikuwahi kukaa pale muda wa chakula.
daah watoto wakweli sanaaa
 
Kuna dada mmoja rafiki yangu,alinitembelea home, siku hiyo nilikua nipo na kabinti kangu , kana miaka mitatu .

Tukawa tupo mezani wote watatu wakati wa chakula cha mchana .

Baada ya kumaliza kula binti wa watu kabakiza chakula , akadai kashiba.

Kabinti kangu kakaropoka" icho chakula unamwachia nan? , unadhani baba yangu anapesa za mchezo" .

Duh niliona aibu sna ,sijui ayo maneno kayatolea wapi.
Mwenyewe mkuu sipendi mtu abakize chakula na kitupwe, unasema mapema kama ni kingi.......
Sitaki uharibifu watu wanalala njaa ujue. Una binti smart Kwa kweli
 
Niliwahi kukaribishwa chakula kwenye familia fulani ya kishua nikapikiwa ugali na nyama ya mchuzi. Nikaona ili nifaidi vizuri lile chuzi nikawa kila nikimega tonge natumia dole gumba langu kupiga lile shimo katikati ya donge la ugali ili kuchota ule mchuzi. Kumbe kuna dogo wao wa miaka mitatu hajawahi kuona kile kitu. Basi aliponiona kakimbia kwenda jikoni akiita mama mamaa njoo uone mama yake kaja dining anamuulizia nione nini. Dogo karopoka mgeni anatengeneza kwa kutumia ugali kichoteo cha mchuzi. Niliona aibu acha tu.
 
Hahahaha...mgeni
 
Mwenyewe mkuu sipendi mtu abakize chakula na kitupwe, unasema mapema kama ni kingi.......
Sitaki uharibifu watu wanalala njaa ujue. Una binti smart Kwa kweli
😄
 
Kuna dada mmoja rafiki yangu,alinitembelea home, siku hiyo nilikua nipo na kabinti kangu , kana miaka mitatu .

Tukawa tupo mezani wote watatu wakati wa chakula cha mchana .

Baada ya kumaliza kula binti wa watu kabakiza chakula , akadai kashiba.

Kabinti kangu kakaropoka" icho chakula unamwachia nan? , unadhani baba yangu anapesa za mchezo" .

Duh niliona aibu sna ,sijui ayo maneno kayatolea wapi.
Huyu mtoto ana akili sana
 
Kitoto changu nilikipeleka hospital kuchek malaria sasa baada yakutoka hospital tukakaa bar flan jiran na hospital kumnunulia chips akawa anagonga pale mara siakaamza kulilia bia , eti nataka biaaa ,ninunulie bia nikawa nazuga pale muhudumu naomba malta huyu dogo malta anaitaga bia dogo likaanza sitaki hio nataka pombee kulikuza na wazee pale wakawa wananiona kama mpinga kristo halafu Chakushangaza sijawah kula gambe mbele yake na mama yake hanywi na kilikua na miaka miwili dah
Kuna katoto changu kana miaka miwili kanapenda pombe balaa.kakiipatia kanaigonga kinoma hata kisungura.Sasa hivi huwa nakaficha kasiione.
 
Wakuu kwema?

Kama tunavyojua watoto walivyo, hawana aibu, wanafanya kile wanajisikia kwa wakati huo, japokuwa kuna wengine wananya kukukomesha. Wanajua mama/baba huwa hataki kuninunulia kitu fulani mkifika supermarket anapiga kelele duka zima wanasikia analilia mdoli😂😂.

Ama unajua mtoto wako huwa hali kitu fulani, unakaribishwa umpe mtoo unasema mwananguhuwa halagi hivi, picha linaanza mwanai alaililia na kula kitu!

Vipi mdau, ni tukio gani mtoto wako aliwahi kukuambisha mbele za watu?
Nilijisikia vibaya pale mwanangu aliposema baba hapa tunakula mpaka tunashiba, hivi naweza kubaki hapa mpaka shule ifunguliwe mwakani? Alikuwa anayasema haya kwa jirani yetu tulipokwenda kutoa pole ya msiba.
 
Back
Top Bottom