Mtu akiandika hivi huwa najisikia hasira

Mtu akiandika hivi huwa najisikia hasira

"Jomoni inaxikitixha xana tyu, xaxa tyufanyaj akati 2mezoea. Noma keli mxhkaji wang"

Mtu mmoja aliniandikia kama hivyo nilimuuliza una ulemavu wa mdomo?
 
Wapo wengi saaaana

Ukiona hivi ujue hawasomagi magazeti kwa asilimia kubwa, waandishi wa magazeti ni msaada mkubwa sana kuweka kiswahili vzr

Na Waalimu wa zamani walikuwa wapenzi wakubwa wa kusoma magazeti

Sasa mtu atakuaje maneno sahihi wakati yuko busy kuchat na mxhkaj na msela pamoja na youtube??
Kaka kuna magazeti na magazeti ya kusoma..siku hizi hawa waandishi wa habari (wote wa radio, runinga na magazeti) ndio wamekuwa wanaongoza katika "kukibananga" Kiswahili. Inasikitisha sana kumsikia au kusoma mwandishi wa habari akisema au kuandika sentensi ..." hii ni kati ya NYIMBO bora sana mwaka huu"

Au utasikia "timu haikupata matokeo" unajiuliza timu haikupata matokeo kwa namna gani, kama ilipambana na timu nyingine ni lazima tu itakuwa ilipata hayo matokeo, inaweza kuwa ilipoteza mchezo au ikasuluhu yote bado ni matokeo.
 
Mtu akiandika hivi "cna kitu kabisa. cc unacmaje?mambo vp ? "Yaani sijui ninamuona vipi?
 
Wakuu
Kuna matamshi ya namba naona ni magumu kwa watu wengi.
Unakuta nne wanatamka 'ine' au 'yine', thelathini wanatamka 'salasini' au 'selasini', fedha wanaitamka 'feza'.

Hivi huwa tatizo ni nini?

Naona tu watu wengi wanatamka hivyo sasa sijui ni mtindo mpya au inakuaje?
 
Aisee maneno kama.
KO, TYU, XAXA, jomon,
Huwa najua ni kiswahili cha Aliens.
 
[QUOTE="kibangubangu, unakuta mtu anakutumia sms
"Habari za hasubuhi"
 
Back
Top Bottom