Mtu akiandika hivi huwa najisikia hasira

"Jomoni inaxikitixha xana tyu, xaxa tyufanyaj akati 2mezoea. Noma keli mxhkaji wang"

Mtu mmoja aliniandikia kama hivyo nilimuuliza una ulemavu wa mdomo?
 
Kaka kuna magazeti na magazeti ya kusoma..siku hizi hawa waandishi wa habari (wote wa radio, runinga na magazeti) ndio wamekuwa wanaongoza katika "kukibananga" Kiswahili. Inasikitisha sana kumsikia au kusoma mwandishi wa habari akisema au kuandika sentensi ..." hii ni kati ya NYIMBO bora sana mwaka huu"

Au utasikia "timu haikupata matokeo" unajiuliza timu haikupata matokeo kwa namna gani, kama ilipambana na timu nyingine ni lazima tu itakuwa ilipata hayo matokeo, inaweza kuwa ilipoteza mchezo au ikasuluhu yote bado ni matokeo.
 
kibangubangu, Halafu unakuta anaeongea hivyo ni mdada mrembo au mkaka kapigilia pamba za kufa mtu...
 
Mtu akiandika hivi "cna kitu kabisa. cc unacmaje?mambo vp ? "Yaani sijui ninamuona vipi?
 
Wakuu
Kuna matamshi ya namba naona ni magumu kwa watu wengi.
Unakuta nne wanatamka 'ine' au 'yine', thelathini wanatamka 'salasini' au 'selasini', fedha wanaitamka 'feza'.

Hivi huwa tatizo ni nini?

Naona tu watu wengi wanatamka hivyo sasa sijui ni mtindo mpya au inakuaje?
 
Aisee maneno kama.
KO, TYU, XAXA, jomon,
Huwa najua ni kiswahili cha Aliens.
 
[QUOTE="kibangubangu, unakuta mtu anakutumia sms
"Habari za hasubuhi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…