Mtu akifa anatakiwa azikwe wapi? Migogoro ya kuzika maiti

Mtu akifa anatakiwa azikwe wapi? Migogoro ya kuzika maiti

Alifariki dada angu mwaka juzi, mi nikasafiri usiku kucha kuwahi mazishi , nafika nakutana na huo ujinga!

Mume wake wa zaman na mume wa sasa wanagombea kuzika maiti, tukaanza kuuweka issue mpaka ikafika mahakamani!

Kuna mambo yanashangaza sana!
Huwezi Elewa mpaka siku mpendwa wako kama mtoto wako alafu atokee mtu mwingine aamue mahali pengine pa kumzika
 
Hio biashara nilishaikataa, tuwe kama mabohora tu, ukifa unazikwa hapo hapo tu ulipofia na waliokuwepo haijalishi ni kwenu au sio kwenu ili mradi kuwe na watu tu wakuzika.

Kuna kuzikwa na kufukiwa Mkuu.
Hapa tunazungumzia Maziko
 
Umetumia misingi na utamaduni wa kabila la Wapare, umama umama umetajwa sana, patrilineal na matrilineal ni msingi sana, ukiachika, mahari kurudishwa, kuhama makazi, kukosa makazi, kutengwa, ugomvi, na etc

Hakuna utamaduni hapo.
Hapo tunazungumzia haki na ukweli.

Kwa sasa Afrika hakuna utamaduni isipokuwa Baadhi ya makabila kama bushmens, wàtiñdiga, Wahadzabe n.k.


Kwa kukuweka sawa Wapare sio Matrilineal society tangu mwanzo
 
Kwahiyo ukifika wewe kumzika ndo atafufuka? Maiti azikwe haraka ndani ya masaa 24 ukifika utaonyeshwa kaburi

Kwa nini azikwe asifukiwe tuu au kutupwa baharini au kukatwa kataa na kugeuzwa chakula cha mbwa?
 
Siku ukifiwa na unayempenda ndio utapata jibu la swali lako.

Ni sawa na uulize kuna faida gani mtu anayefia Marekani au Ughaibuni alafu asafirishwe kuzikwa huku Bongo.
Nimeshafiwa na wapendwa wangu kadhaa, baadhi ya ndugu waligombania kuhusu suala la mazishi.

Kwa utashi wangu nilijiridhisha kwamba malumbano hayo sababu yake kubwa ni kugombania Mali katika muktadha wa urithi, vinginevyo ni ignorance tu
 
Mtu atamuacha babaye na mamaye na kuambatana na mumewe/mkewe na kuwa mwili mmoja, acheni ufitini aliewaambia nyie familia mnamamlaka ni nani?, babu yenu kafa hajatengana na mkewe nyinyi mnalazimisha. Huko walipo wanakula maisha kwa Upendo uliotukuka nyie endeleeni na fitina zenu.

Mtu akifa automatically ndoa haipo katika msingi wa hicho ulichoandika.
Hakunaga ndoa na Mfu au marehemu.

Ukiandika mambo ya dini uwe na uelewa nayo.
Kifo ndio kinatenganisha na kuvunja ndoa
 
Nimeshafiwa na wapendwa wangu kadhaa, baadhi ya ndugu waligombania kuhusu suala la mazishi.

Kwa utashi wangu nilijiridhisha kwamba malumbano hayo sababu yake kubwa ni kugombania Mali katika muktadha wa urithi, vinginevyo ni ignorance tu

Ûkiona uliachia jua haukuwa na bond kubwa na wala haukuwa na uhalali na maamuzi yoyote juu ya jambo hilo.
Subiri siku ufiwe na mtu ambaye unamamlaka juu yake na mpendwa wako ndio utaelewa vizuri

Umemlea mtoto kwa miaka yote alafu mwisho wa siku anatokea mwanaume mwingine baada ya kifo cha mwanao anasema ni mtoto wake na anataka achukue mwili akazike anakojua utakubali?
 
Alifariki dada angu mwaka juzi, mi nikasafiri usiku kucha kuwahi mazishi , nafika nakutana na huo ujinga!

Mume wake wa zaman na mume wa sasa wanagombea kuzika maiti, tukaanza kuuweka issue mpaka ikafika mahakamani!

Kuna mambo yanashangaza sana!
Daaah! Hao waume zake wana akili za hovyo sana

Mahakama iliamuaje?
 
Yuda
9 Lakini hata Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na shetani kuhusu mwili wa Musa, hakuthubutu kutamka hukumu juu ya shetani, bali alisema, “Bwana akukemee!”

Hayo mambo ya kugombea mwili mpaka kwenye biblia
Ni kweli kabisa

Shetani alijua Musa aliheshimika sana hivi kwamba watu wangeanza kuabudu alipozikwa Musa

Ndio maana Mungu alificha alipokufa Musa kumzuia Shetani
 
Mtu kuolewa katika ukoo fulani haimaanishi kuwa ukoo huo unamamlaka ya kuamua Mwanamke huyo azikwe wapi. Mwenye mamlaka ni Mhusika mwenyewe kama aliomba, au mumewe au watoto wake kama ni wakubwa wanaojiweza kiuchumi.
Umeandika mambo lukuki lakini umeonesha njia kwamba KIPATO CHA UPANDE FLANI ndio kinaweza kutoa muelekeo wa mazishi yafanyike wapi.

Jambo lingine ni mila na desturi za jamii flani. Zipo jamii ambazo ni nguvu ipo ujombani na jamii nyingine nguvu ipo kiumeni. Jambo hili huwa linatazamwa kama msingi mkuu wakati wa ibada ya wapi mtu azikwe.
Ingawa yote hayo yanaweza yakabadilika kutokana na mauti yalipomkuta mwanafamilia. Mfano kama amefia sehem x na anatakiwa akazikwe sehem q lakini familia haina mgogoro,busara ikatumika na kila mtu asiamue kujionesha yeye ni nani basi mwili utazikwa popote pale tena kwa makubaliano ya pande mbili
 
Shukrani sana Mkuu



Siku hizi hakuna hizo mila na desturi ndio maana mimi naitwa Robert na wewe unajiita Half Amerika.

Bibi na babu zangu walikuwa Wakristo na kwa mila zetu hakuna kitu kinaitwa Ukristo.

Mila na desturi sio ruhusa kuoona makabila tofauti lakini siku hizi Watu wengi wameoa na kuolewa na makabila tofauti.

Kwa kifupi hizo mila za kiàfrika siku hizi hazipo labda kwa wàtiñdiga, Wahadzabe n.k huko
Sijui kwa kabila lako ila kwa kabila langu bado kuna miongozo inafuatwa bila kujali usasa.
 
Ukichagua pa kuzikwa tuachie na nauli ya kukupeleka unapotaka
 
Sijui kwa kabila lako ila kwa kabila langu bado kuna miongozo inafuatwa bila kujali usasa.

Kwa Tanzania hii makabila yenye mila hayazidi matano.
Lakîni sisi wengine kuanzia Wapare, Wachagga, wahayà, wasukuma , Wanyamwezi na makabila mengi màarufu hayana kitû kinaitwa ûtamaduni.

Kama kûngekuwa na utamaduni au hizo mila pasingekuwa na kitu kinaitwa sijui Tanganyika sijui Tañzania. Kila kabila lingekuwa ñçhi kamili
 
Back
Top Bottom