Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Katika jamii, ni jambo lisiloepukika kukutana na watu wanaotukana au kusema maneno ya kuumiza. Hali kama hii hutufikisha kwenye options mbili: kulipiza au kujibu kwa hekima bila matusi. Biblia inatufundisha kuchagua option ya pili: kutokurudisha tusi - kujibu kwa upole na kusamehe.
Yesu Kristo ni mfano bora wa jinsi ya kumjibu anayekutukana bila kumtolea matusi. Yesu alipokuwa akiteswa, alidhihakiwa, alipigwa, na kutukanwa hadharani. Hata hivyo, hakulipiza kisasi kwa maneno au matendo mabaya. Kuna wakati alikaa kimya au alijibu kwa hekima.
“Alipotukanwa, hakurudisha tusi; alipoteswa, hakutisha bali alijikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki.”
(1 Petro 2:23)
Wakati aliposulibiwa, watu walimcheka na kusema:
“Aliwaokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe!”
(Mathayo 27:42)
Lakini Yesu hakujibu kwa maneno ya chuki, badala yake aliwaombea watesi wake:
“Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.”
(Luka 23:34)
Yesu ni Mungu. Ndiye aliyetuumba. Alipotukanwa alikuwa na uwezo wa kuwafanyia chochote waliomtukana au kumdhihaki, lakini hakufanya hivyo. Ametuachia kielelezo tufuate nyayo zake(1 Petro 2:21).
"Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. Ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Mwenyezi Mungu. Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.” Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema..”
(Warumi 12:17-18)
Tukifanya hivyo maisha yatakuwa mazuri hata humu JF.