Hiyo hoja ni ya kawaida sana, inayotolewa na watu wanaoona kwamba Yesu ni mtume tu lakini sio Mungu.
Ndugu yangu, ukisoma Biblia kwa mapana, utaona ushahidi mwingi kwamba Yesu ni Mungu aliyevaa mwili. Ngoja nikudadavulie hapa hoja zenye msingi wa Maandiko:
1. Yesu alisema Yeye ni Mungu
Yesu alisema mambo ambayo kwa Wayahudi ilikuwa ni sawa na kuchukua nafasi ya Mungu, ndiyo maana walitaka kumpiga mawe:
Kwa mfano alisema: "Mimi na Baba tu umoja."
— Yohana 10:30
Wayahudi walipotaka kumpiga mawe, walisema:
"...kwa sababu wewe, uliye mwanadamu, wajifanya kuwa Mungu."
— Yohana 10:33
2. Yesu alisamehe dhambi — Jambo linalofanywa na Mungu tu
“Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kusamehe dhambi...”
— Mathayo 9:6
Wayahudi walishangaa kwa sababu waliamini ni Mungu tu anayeweza kusamehe dhambi.
3. Yesu aliitwa Mungu na wafuasi wake — na hakuwakemea
“Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!”
— Yohana 20:28
Kama Tomaso angekuwa amekosea kumwita Yesu Mungu, mbona Yesu hakumkemea kwamba amekosea — alikubali.
4. Yesu alikuwa na asili ya ki-Mungu hata kabla dunia haijaumbwa
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Neno akafanyika mwili, akakaa kwetu.”
— Yohana 1:1, 14
5. Wanaokana Yesu kuwa ni Mungu wana kikomo cha uelewa
Yesu alifundisha kuwa wale wasioamini kwamba yeye ni Mungu, hawamjui Baba pia:
“Kama hamuamini mimi ni Yeye, mtakufa katika dhambi zenu.”
— Yohana 8:24
“Yeye aliyeniona mimi amemwona Baba.”
— Yohana 14:9
6. Yesu alifanya miujiza kwa nguvu yake mwenyewe
Marko 4:39
"Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, 'Nyamaza, utulie!' Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu."
Yesu hakusema "kwa jina la Baba," au "kwa jina la Mungu," — alisema kwa amri yake mwenyewe, na bahari ikamtii. Hii ni ishara ya kuwa yeye ni Muumba mwenyewe.
Sikiliza tena anavyosema katika
Yohana 10:17-18
"Kwa sababu hii Baba anipenda, kwa kuwa nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi mwenyewe nautoa. Ninao uwezo wa kuutoa, tena ninao uwezo wa kuutwaa tena."
Hapo Yesu anaonyesha anafanya kwa hiari yake mwenyewe, na tena ana uwezo wa ki-Mungu wa kufufuka — jambo ambalo hakuna mwanadamu yeyote anaweza kulifanya kwa nguvu zake mwenyewe.
Huo ni uthibitisho wa wazi kuwa Yesu hakutegemea tu nguvu ya Baba, bali alikuwa na mamlaka na uwezo wa kipekee wa Mungu Mwana. Umenipata mkuu?