Mtu anatekwa Stendi ya Magufuli huku watu wanaangalia? Wananchi tunatakiwa kujitafakari, imekuaje tumekuwa mazombi hivi?

Mtu anatekwa Stendi ya Magufuli huku watu wanaangalia? Wananchi tunatakiwa kujitafakari, imekuaje tumekuwa mazombi hivi?

Wewe ungefanyaje? Tatizo la hii nchi ni kuwa na Idadi kubwa sana ya Keybord woriour. Tuna Keybord woriou wengi kuliko Taifa lolote lile Duniani.
Mengi tungeweza kurusha mawe, kurekodi kama bonge, kutumia chochote ambacho kipo hapo kusaidia...... ukiona mtoto wako anachukuliwa na watu wenye bunduki hutapambana? You'll do anything to save them
 
IMG-20241201-WA0048.jpg
 
Mengi tungeweza kurusha mawe, kurekodi kama bonge, kutumia chochote ambacho kipo hapo kusaidia...... ukiona mtoto wako anachukuliwa na watu wenye bunduki hutapambana? You'll do anything to save them
Unaongea wingi au umoja?
 
Hatuna nguvu za kupambana,
Tunashindia Miguu ya Kuku na utumbo wake.

Halafu hizo nguvu kidogo tunazopata tunazimalizia kwenye kubishana kuhusu Mpira.
 
Dar unaibiwa watu wanakuangalia.

Dar unaporwa simu na vibaka Raia wanakuangalia

Dar unatekwa stand Raia wanakuangalia bila kuhoji

Dar mji wa wajanja,hakuna kama Dar Tanzania [emoji3][emoji13]
Dar unakata roho watu wanakuangalia tu wengine wanchukua video.
 
Mimi nashauri .....tusijatibu tupambane kubadili ile sheria iliyowapa nguvu....kosa likokule .....mazingira kukutesa huwa haraka sana ...na mguvu kubwa.....ukiwa huma mbavu....dak 2 uko ndani gari.....pia its higly timing .....sehemu tulivu kidogoo.....sikia tuuuu
Nchi yao, chama chao, serikali yao na BUNGE lao. Sasa niambie utapambanaje ili sheria ibadilishwe? Tafadhali tupe hiyo mbinu.
 
Hivi wachawi na waganga wa kienyeji huwa ni kweli au waongowaongo tu.
Kama ni kweli kwa nini wasitusaidie kutusafishia hawa watu - watokee majibu mwili mzima - waende wakipiga makelele barabarani - wafe meno yakiwa nje???
Kuna watu walisoma dua juzi..vipi imefanyakazi??
Wapi wazee wa -gamboshi - nyinyi si tumekua tukisikia kuna hadi treni za miujiza - Tanga tunasikia nyinyi ni wazee wa majini - au ni hadithi za abunuwasi tu???
 
Wakuu,

Mtu wa pili huyu anatekwa sehemu ambayo kuna watu na hakuna kitu raia tunafanya? Tunasubiri apotee ndio tuje mtandaoni kuanza kulaani na kulisema Jeshi la Polisi, Samia na Serikali yake?!

Pia soma: Breaking News: - Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulika katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Wana Dar tuna nini? Ndio hatuna umoja kiasi hiki? Hili jambo lingetokea Chuga au sehemu nyingine wangekiwasha hadi kieleweke, na ijulikane hao watu ni akina nani. Walau hata kwa Bonge walijiongeza tukio likarekodiwa, huko watu wamekaa tu kama ndezi.

Wamejaribu kwa bonge wakaona jinsi watu hatuna umoja, leo wakaenda kwa chembamba wamprove kuwa wananchi tupo tupo tu!

Kwanini lakini tunakuwa mazombi hivi?
Wanaume wa Dar.
 
Ndugu ,bunduki haina mwenyewe .
Uantaka kuniambia raia zaidi ya 50 wangebeba .mawe makubwa na mazito na kuanza kurusha unafikir hao mammbwa na mabunduki yao wangebaki , kuna mikoa huwez fanya huo upumbavu eitha utakua marehem ama sanasana gari yako itabaki majivu ..ila dar ni pa kiduwani watu wa huko wanajua kula stareh tu
 
Stendi, kila mtu yuko bize na mabegi yake plus makelele kibao na harakati za kutosha.

Mpk ukafahamu mtu huyu anatekwa, halafu upate interest ya kurekodi kisha uwashe data na kamera, unakuta watu washamaliza yao .
mbona ikitokea ajali watu wanakuwa fasta kuchukua picha?
 
Watanzania ni watu wa kipekee sana. Hapo atapita mwizi wa mchicha fungu moja watapiga waue kabisa ila binadamu anaibwa wanatazama tu. Tupo hivyo.
Ipo hivyo
Haibadiliki damu yetu
Sema watu wa Dar,baadhi ya watu mikoa mingine hawawezi ruhusu ujinga kama huu utokee
 
Mtu mkubwa hivyo unakuja dar na Basi duh ACT na nyie mjitafakari Kama mna budget ya kuendesha chama
 
Nchi yao, chama chao, serikali yao na BUNGE lao. Sasa niambie utapambanaje ili sheria ibadilishwe? Tafadhali tupe hiyo mbinu.
Instead unataka upambane na watekajii khaaaaa
 
Back
Top Bottom