Alivyoapishwa Samia Suluhu kwa kujua mapenzi na imani kubwa waliyokua nayo Watanzania kwa Magufuli alisema baada ya kuapa kua rais wa Tanzania kwamba yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Na amerudia kusema hivyo mara kadhaa.
Mkuu @kambwembwe, kwanza asante kwa hoja hii, pili ni kweli, Rais Mama Samia aliwaahidi Watanzania kuwa yeye ni kama Magufuli, atamuenzi kwa kauli na matendo, na kutekeleza yote ya Magufuli na ni kweli anatimiza ahadi.
Kwa vile rais Magufuli hakuwa malaika, ni binadamu, ana mazuri yake na mabaya yake, hivyo mtu akifa, ni mazuri yake tuu ndio anatuachia, na mabaya zake anazikwa nayo, anaondoka nayo, na mabaya hayo hayana haja ya kusemwa tena!, marehemu hasemwi vibaya, tumwache apumzike dalama. Ila katika kumuenzi mtu, unachukua yale mazuri tuu ndio unayaenzi na kunayaendeleza, na yale mabaya, unaachana nayo, aliisha zikwa nayo.
Katika utekelezaji wa awamu zote, pia hutokea makosa, Awamu ya kwanza ya Mwalimu, enzi za Azimio la Arusha na siasa ya ujamaa na kujitegemea, kulitokea makosa fulani fulani katika maeneo mengi, ikiwemo operesheni vijiji, na kwenye miiko ya uongozi, ukijumlisha na athari za vita ya Kagera, kiukweli kabisa Nyerere was right kung'atuka, na nchi ilikuwa kwenye hali mbaya sana. Awamu ya Mwinyi alipoingia, aliendeleza mazuri ya Nyerere, na kuyabadili mabaya ikiwemo kupitisha Azimio la Zanzibar likalifunika Azimio la Arusha, Mwinyi akafungulia ruhksa zote. Mkapa alipoingia akaenzi ya Mwinyi na kuleta privatization, JK naye akaenzi ya Mkapa na kutuingiza kwenye utandawazi, JPM was a game changer, akaleta ya kwake na katika kuyatekeleza, kuna makosa fulani fulani yametendeka na awamu hiyo, Sasa Mama Samia ndio ni kweli yuko lama JPM, anamuenzi kwa kauli na matendo, ila pia anarekebisha baadhi ya moakosa, kwa kutumia mfumo mpya wa to heal the nation. Kati ya makosa hayo ni makosa kwenye "hire and fire", na hili msiseme tunamsema marehemu, no, sisi wa kusema hili tulilisema wazi
Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ...
Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete ...
Anachokifanya Mama Samia, kuwateua baadhi ya waliotumbuliwa na JPM, ni wale tuu the fine guys waliotumbuliwa kwa makosa. Kwa hili kiukweli Mama Samia atabarikiwa sana na nchi itabarikiwa
Sasa mimi nauliza kama ni sawa Rais Samia kumuweka uwaziri mtu au watu waliyojitokeza mbele ya umma au kunaswa sauti zao wakimkashifu na kumkejeli the late Magufuli.
Hizo voice notes wewe ulizisikiliza?, kwenye waliorudishwa kuna yeyote wewe ulimsikia akimshfu JPM?. Mimi nimezikiliza zile voice notes zote, kuna wengine kiukweli kabila walisema ukweli mtupu kumhusu JPM na wala hawakukashifu chochote, ila bado waliomba msamaha na JPM aliwasamehe na yakaisha.
Wananchi kwa ujumla wao wanaomuenzi Magufuli na kupenda mwelekeo kisiasa na kiuchumi wa Tanzania kuendelea na mwendo wa Kimagufuli hakika wanakwazika sana kuona mtu yeyote aliyejitokeza wazi kumpinga na kumkejeli Magufuli anaaminika kushika Wizara nyeti kwenye Serikali ya mrithi wa Magufuli.
Poleni sana kwa kukwazika, Eais Samia is healing the nation, kama kuna watu wa Magufuli ambao mnakwazika kwa anayoyafanya Mama Samia, kuwateua baadhi ya wale JPM aliowatumbua, ndio sasa mjue kuwa japo Samia ni kama JPM, ila kwenye haki bin haki, JPM was JPM na Samia is Samia. ni watu wawili tofauti kama mbingu na nchi.
P