Mtu anayesema 'Katiba haileti chakula mezani' ni mjinga na mpumbavu

Mtu anayesema 'Katiba haileti chakula mezani' ni mjinga na mpumbavu

Ng'ombe nyingine hii hapa.

20261013_101021.jpg
 
Wakulima hawahitaji katiba,walilima kabla katiba haijaja,ilipokuja na hata sasa,wakulima wanahitaji maji ya uhakika/irrigation schemes,pembejeo,soko
Katiba haijamzuwia mtu kufanya biashara,kuanzisha kiwanda, kusoma nk
Acheni kufanya katiba ni hitajio muhimu na la dharura la nchi,fanyeni kazi kenge nyie
Hiyo bajeti ya umwagiliaji itapangwa na nani na kikao cha ukoo, muwe mnatumia akili basi.
 
Hiyo bajeti ya umwagiliaji itapangwa na nani na kikao cha ukoo, muwe mnatumia akili basi.
Mpe Elimu kua mfano ibara flani ya katiba ya Warioba inaonesha jinsi kilimo,uvuvi nk vitakavyokua vinaendeshwa
 
Huwezi kutenganisha katiba na maisha ya watu, huwezi kuitenganisha katiba na uchumi wa mtu, ajira ya mtu, afya ya mtu, elimu ya mtu.

Swala muhimu si tu “katiba inaleta chakula” bali pia katiba inaweza kuathiri mazingira yanayowezesha watu kupata chakula, kazi na huduma mbalimbali.

Katiba ndiyo inayoweka kanuni za mamlaka, haki, uwajibikaji na namna taasisi za serikali zinavyofanya kazi.

Haki ya kuishi imewekwa na katiba, haki ya kufanyakazi inawekwa na katiba, utaratibu unaofuatwa na machinga, bodaboda umewekwa na katiba, mshahara unaotegemea ukanunue chakula unawekwa na katiba.

Uhuru wa wanasiasa wanaotamka hayo maneno nao umewekwa na katiba.

Bila katiba hakuna serikali hakuna vyama vya siasa hakuna shule, hakuna mahakama.

Mtu yeyote anayesema katiba haileti chakula ni wa kupuuzwa kwa ujinga wake, ni mpumbavu maana hata cheo alichonacho amekipata kupitia katiba anayoidharau.

By Quinine wa JF.
Usiwalaumu sana, maana kuna watu waliletwa duniani kula. Hawana lingine wanalofanya ni chakula tuu!!
 
Back
Top Bottom