Aneifanya hiyo biashara kwa bajaji moja na anaitegemea hiyohiyo kwa kuendesha maisha na huku kampa mtu amletee 20k per day anajiunguza mwenyewe.
Ila kwa experience yangu nimeona wengi wana mishe nyingine bajaji inakua extra, na bajaji sio moja.
Kuna mwamba ana bajaji 10+, zinampa pesa nzuri mno.
Nadhani mleta uzi jaribu kufanya tafiti, na hizo bajaji wengine huwapa mkataba kua baada ya kipindi fulani bajaji inakua ya huyo dereva, so tajiri anachukua pesa kwa muda fulani baada ya hapo kijana bajaji inakua yake. Hapo hata ikae 2 yrs chombo inakua vyedi maana kijana anaimaintain kama yake.
Hizi biashara ukiziangalia kichwakichwa kama ufanyavyo hamna utayoona ina faida, zote utaona watu wanacheza makida makida, kumbe pesa ipo ni dharau zako tu na miscalculation zako.