Mtu asiyewatunza watu wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko atheist

Mtu asiyewatunza watu wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko atheist

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Katika jamii yoyote yenye maadili mema, jukumu la kuwahudumia na kuwatunza watu wa nyumbani ni la msingi sana. Biblia katika 1 Timotheo 5:8 inasema: “Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.”

Mbele za Mungu, Atheist ni mtu mbaya kwakuwa haamini kwamba kuna Mungu. Ndio sababu katika Zaburi ya 53:1 Atheist anaitwa mpumbavu.

Sasa mtu asiyetimiza wajibu wa kuihudumia familia yake, Mungu anamhesabu mtu huyo kuwa ni mbaya kuliko Atheist.

Kwahiyo watoto uliowazaa katika ndoa na nje ya ndoa ni wa kwako. Unapaswa kuwatunza. Kama umewatelekeza, wewe ni mtu mbaya kuliko Atheist.

Jiulize: umewapa mimba wasichana wangapi na wanawake wangapi tangu uanze uasherati na uzinzi? Inawezekana kabisa watoto waliozaliwa kwa mbegu zako hadi sasa ni 100+. Wote hao unapaswa kuwatunza. Kama hujui wako wapi, anza sasa kuwatafuta uwatunze.

Kuwatunza watu wa nyumbani mwako ni kuwahudumia kwa mali zako. Ni kuhakikisha wanapata malazi, chakula, mavazi, elimu na kuwa na afya njema hadi watakapoweza kujitunza wenyewe. Pamoja na hayo unapaswa kuwa karibu nao kihisia. Uwaonyeshe upendo na moyo wa kuwajali. Kama hufanyi hayo, tambua leo kuwa wewe ni mtu mbaya, na madhara ya kuwa mtu mbaya yatakupata.
 
Ni madhara gani anayoyapata asiyewatunza wa nyumbani mwake?
Kuna madhara ya kiroho na kijamii. Nakutajia hapa baadhi:
1. Anapoteza heshima katika jamii. Mtu asiyejali familia yake anaonekana mtu katili, asiye na huruma.

2. Anajisababishia migogoro na mafarakano. Mke na watoto aliowatelekeza, wataishi kwa uchungu na kukosa amani. Matokeo yake wanaweza kumfungulia hata kesi kwa kutowajali.

3. Anajiletea laana na hukumu. Kama Andiko lile lilivyosema, mtu wa namna hii ameikana imani. Kwa maneno mengine, anajiweka katika kundi la wale watakaokosa kuingia mbinguni.

4. Anapata athari za kisaikolojia. Mtu anayepuuza familia yake hukumbwa na msongo wa mawazo, kujilaumu, na kuwa na maisha yasiyo na furaha ya kweli. Moyo wake hukosa amani na hatimaye huishi maisha ya kujitenga au ya kukataliwa.

5. Watoto wasipotunzwa, wanapitia maisha yenye mateso makubwa: njaa, ukosefu wa elimu, kukosa makazi bora, na hata kuingizwa kwenye tabia hatarishi kama wizi, ujambazi na utumiaji wa madawa ya kulevya. Hii inazalisha kizazi kibaya kinachoweza kukudhuru na kukujeruhi wewe mwenyewe.
 
Mtu asiyejali wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko asiyeamini. Hata hivyo Mungu bado anamwita amrudie:

Isaya 55:7
"Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa."

Rejea kwa Mungu leo – rehema zake bado ziko wazi kwa wote wanaotubu kwa moyo wa kweli. Na ukiishatubu dhambi hiyo ya kutowatunza wa nyumbani mwako, anza sasa kuwatunza kwa hali na mali.
 
Kwa andiko hili la 1 Timotheo 5:8 kama huwatunzi watoto uliowazaa - hata kama unasali; hata kama unatoa sana sadaka; hata kama wewe unajiita Mtumishi - unahesabika kuwa umeikana imani. Ni mtu mbaya kuliko Atheist.
 
Kumbuka hutadumu kuwa kijana. Kuna wakati utakuwa mzee. Kwa kuacha kuwatunza watoto wako uliowazaa, unajitengenezea uzee wenye upweke na majuto. Watoto uliowatelekeza, wakija kufanikiwa, itakuwa vigumu kwao kukusaidia utakapokuwa mzee usiyejiweza.

Mithali 11:29
"Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo..."
 
Mbele za Mungu, Atheist ni mtu mbaya kwakuwa haamini kwamba kuna Mungu. Ndio sababu katika Zaburi ya 53:1 Atheist anaitwa mpumbavu(Zab 53:1).
Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu watakao mwamini yeye yupo siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?

Huyo Mungu yeye ndio mpumbavu.
Sasa mtu asiyetimiza wajibu wa kuihudumia familia yake, Mungu anamhesabu mtu huyo kuwa ni mbaya kuliko Atheist.
Mungu ambaye alishindwa kuumba dunia yenye watu wema badala yake akaruhusu uovu na waovu wawepo, Mungu huyo ndio hafai kabisa. Anastahili kufurushwa huko alipo.
 
Sahihi kabisa...kama uwezo anao
Nakumbuka kuna binti fulani alikuwa anadai haki yake kwa wazazi wake: wamtunze, wamsomeshe. Baba yake alikuwa anajitetea kwamba hana pesa, hana uwezo. Binti akamhoji: "Kama mlijua hamna uwezo wa kunitunza, kwanini mlinizaa?" 🙂
To yeye ungekuwa wewe ndio umeulizwa swali hilo ungemjibuje huyo binti
 
"Hakika upumbavu WA Mungu Una hekima kuliko akili za binadammu"😹😹😹😹
 
Katika comments 11 saba ni we mwenyewe

Basi sawa.....
Zangu sio comments. Ni mwendelezo wa mada. Watu humu ni wavivu wa kusoma, wanapenda mada fupi fupi, ukiandika gazeti hawasomi, wanaruka.
Umenipata Kambaku ?
 
Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.
mbona mada ina vitu vingi ila ulichoona ni hicho mkuu mbona unakuwa subjective, ndio tunajua wewe ni atheist hata akisema nini huwezi kukubaliana naye, haina haja ya kila thread kusema neno lile lile
 
Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.
Mimi nakupenda,Infropreneur kwa sababu, hoja zako huwa hazina matusi kama Atheists wenzako.
Mimi naamini kuwa wanyama, maua, milima, bahari.. vyote hivyo vinaonyesha wazi kuwa kuna Muumbaji. Angalia jua linavyowaka, dunia inavyolizunguka jua na kusababisha mchana na usiku. Angalia jinsi mfumo wa mwili wa binadamu ulivyo. Jinsi mtoto anavyozaliwa na kutambua mara moja kunyonya maziwa! Mambo haya hayawezi kuwa yalitokea kwa bahati tu kama Atheists mnavyoamini. Lazima kuna akili ya juu iliyotengeneza sheria za asili na mifumo hiyo. Akili hiyo ni ya Mungu.

Kama vile nyumba isivyoweza kujijenga yenyewe bila fundi, vivyo hivyo dunia na viumbe vyote haviwezi kuwa vimetokea tu bila sababu ya msingi au chanzo cha asili. Hata wanasayansi wengi wanakubaliana kuwa kila kilichoanza kuwepo lazima kiwe na chanzo. Binafsi naamini chanzo hicho ni Mungu.

Albert Einstein, mwanasayansi mahiri, ingawa hakuwa Mkristo, aliamini kwamba kuna Intelligent Designer wa universe. Sikiliza alivyosema:
"The more I study science, the more I believe in God."
Akasema pia:"God does not play dice with the universe."

Allan Sandage ni Mwanahisabati na mtaalamu wa nyota aliyesaidia kuthibitisha kuwa ulimwengu una mwanzo na alikiri kuna Mungu. Alisema:
"It was my science that drove me to the conclusion that the world is much more complicated than can be explained by science."

Antony Flew
Alikuwa mmoja wa waandishi mashuhuri wa falsafa waliopigania atheism, lakini katika uzee wake alibadilika na kusema kuwa lazima kuna akili ya juu behind life. Sikiliza anavyosema:
"A super-intelligence is the only good explanation for the origin of life and the complexity of nature."

Nakuombea. Naamini iko siku na wewe utamwamini Mungu, na utakuwa Mwinjilisti mzuri sana.
 
mbona mada ina vitu vingi ila ulichoona ni hicho mkuu mbona unakuwa subjective, ndio tunajua wewe ni atheist hata akisema nini huwezi kukubaliana naye, haina haja ya kila thread kusema neno lile lile
Atheist asiyeamini ktk Mungu.
Heathen mshenzi.
Secular tourist .mtalii WA kiulimwengu asiye na dini.

Secular tourist is our identity ✓ not atheist
 
Katika jamii yoyote yenye maadili mema, jukumu la kuwahudumia na kuwatunza watu wa nyumbani ni la msingi sana. Biblia katika 1 Timotheo 5:8 inasema: “Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.”

Mbele za Mungu, Atheist ni mtu mbaya kwakuwa haamini kwamba kuna Mungu. Ndio sababu katika Zaburi ya 53:1 Atheist anaitwa mpumbavu.

Sasa mtu asiyetimiza wajibu wa kuihudumia familia yake, Mungu anamhesabu mtu huyo kuwa ni mbaya kuliko Atheist.

Kwahiyo watoto uliowazaa katika ndoa na nje ya ndoa ni wa kwako. Unapaswa kuwatunza. Kama umewatelekeza, wewe ni mtu mbaya kuliko Atheist.

Jiulize: umewapa mimba wasichana wangapi na wanawake wangapi tangu uanze uasherati na uzinzi? Inawezekana kabisa watoto waliozaliwa kwa mbegu zako hadi sasa ni 100+. Wote hao unapaswa kuwatunza. Kama hujui wako wapi, anza sasa kuwatafuta uwatunze.

Kuwatunza watu wa nyumbani mwako ni kuwahudumia kwa mali zako. Ni kuhakikisha wanapata malazi, chakula, mavazi, elimu na kuwa na afya njema hadi watakapoweza kujitunza wenyewe. Pamoja na hayo unapaswa kuwa karibu nao kihisia. Uwaonyeshe upendo na moyo wa kuwajali. Kama hufanyi hayo, tambua leo kuwa wewe ni mtu mbaya, na madhara ya kuwa mtu mbaya yatakupata.
Si kweli. Kama hao unaomaanisha si watoto au wasiojiweza, kila mtu anapaswa ajitunze. Je wao watamtunza lini? Jitahidini wanangu kuacha utegemezi bila ulazima.
 
Back
Top Bottom