TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 6,767
- 20,869
Ubishi mkubwa ndio hua unaanzia hapo.Kama vile nyumba isivyoweza kujijenga yenyewe bila fundi, vivyo hivyo dunia na viumbe vyote haviwezi kuwa vimetokea tu bila sababu ya msingi au chanzo cha asili. Hata wanasayansi wengi wanakubaliana kuwa kila kilichoanza kuwepo lazima kiwe na chanzo. Binafsi naamini chanzo hicho ni Mungu.
Ni kweli kabisa kwamba ni upumbavu kuamini kwamba nyumba inaweza kujijenga yenyewe. Yaani matofali yanaweza kujikusanya, yakajipanga, yakajipaua, n.k. Hii inaonyesha kabisa kwamba kuna mjenzi amehusika. Sawa.
Na hii pia inaonyesha kwamba huyo mjenzi lazima atakua "more complicated" kuliko hiyo nyumba aliyoijenga!
Sasa basi.. kama huwezi kuamini kwamba nyumba (ambayo ni less complicated) inaweza kutokea yenyewe bila fundi, unawezaje kuamini kwamba huyo fundi (ambae ni more complicated kuliko nyumba) yeye anaweza kutokea tu bila "sababu za msingi" au chanzo?