Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu watakao mwamini yeye yupo siku zote na wakati wote?Mbele za Mungu, Atheist ni mtu mbaya kwakuwa haamini kwamba kuna Mungu. Ndio sababu katika Zaburi ya 53:1 Atheist anaitwa mpumbavu(Zab 53:1).
Mungu ambaye alishindwa kuumba dunia yenye watu wema badala yake akaruhusu uovu na waovu wawepo, Mungu huyo ndio hafai kabisa. Anastahili kufurushwa huko alipo.Sasa mtu asiyetimiza wajibu wa kuihudumia familia yake, Mungu anamhesabu mtu huyo kuwa ni mbaya kuliko Atheist.
Nakumbuka kuna binti fulani alikuwa anadai haki yake kwa wazazi wake: wamtunze, wamsomeshe. Baba yake alikuwa anajitetea kwamba hana pesa, hana uwezo. Binti akamhoji: "Kama mlijua hamna uwezo wa kunitunza, kwanini mlinizaa?" 🙂Sahihi kabisa...kama uwezo anao
Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.Warumi 9:20
"Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwa nini umeniumba hivi?"
mbona mada ina vitu vingi ila ulichoona ni hicho mkuu mbona unakuwa subjective, ndio tunajua wewe ni atheist hata akisema nini huwezi kukubaliana naye, haina haja ya kila thread kusema neno lile lileHakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.
Mimi nakupenda,Infropreneur kwa sababu, hoja zako huwa hazina matusi kama Atheists wenzako.Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.
Atheist asiyeamini ktk Mungu.mbona mada ina vitu vingi ila ulichoona ni hicho mkuu mbona unakuwa subjective, ndio tunajua wewe ni atheist hata akisema nini huwezi kukubaliana naye, haina haja ya kila thread kusema neno lile lile
Si kweli. Kama hao unaomaanisha si watoto au wasiojiweza, kila mtu anapaswa ajitunze. Je wao watamtunza lini? Jitahidini wanangu kuacha utegemezi bila ulazima.Katika jamii yoyote yenye maadili mema, jukumu la kuwahudumia na kuwatunza watu wa nyumbani ni la msingi sana. Biblia katika 1 Timotheo 5:8 inasema: “Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.”
Mbele za Mungu, Atheist ni mtu mbaya kwakuwa haamini kwamba kuna Mungu. Ndio sababu katika Zaburi ya 53:1 Atheist anaitwa mpumbavu.
Sasa mtu asiyetimiza wajibu wa kuihudumia familia yake, Mungu anamhesabu mtu huyo kuwa ni mbaya kuliko Atheist.
Kwahiyo watoto uliowazaa katika ndoa na nje ya ndoa ni wa kwako. Unapaswa kuwatunza. Kama umewatelekeza, wewe ni mtu mbaya kuliko Atheist.
Jiulize: umewapa mimba wasichana wangapi na wanawake wangapi tangu uanze uasherati na uzinzi? Inawezekana kabisa watoto waliozaliwa kwa mbegu zako hadi sasa ni 100+. Wote hao unapaswa kuwatunza. Kama hujui wako wapi, anza sasa kuwatafuta uwatunze.
Kuwatunza watu wa nyumbani mwako ni kuwahudumia kwa mali zako. Ni kuhakikisha wanapata malazi, chakula, mavazi, elimu na kuwa na afya njema hadi watakapoweza kujitunza wenyewe. Pamoja na hayo unapaswa kuwa karibu nao kihisia. Uwaonyeshe upendo na moyo wa kuwajali. Kama hufanyi hayo, tambua leo kuwa wewe ni mtu mbaya, na madhara ya kuwa mtu mbaya yatakupata.