Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Alphonce mawazo Yuko wapi??nani alimuua Mwangosi??Tume huru ya Uchaguzi Iko wapi??nani alizuia Mali za Lowasa na kuzitoza Kodi kubwa??nani Alivuruga Uchaguzi 2019/20??kwa nini wakiunga mkono juhudi,lazima wapewe vyeo??senseless person will not and never see oppression for opposition
Hili la kupewa vyeo baada ya kuunga mkono juhudi nafikiri CCM wameiga au wamejifunza kutoka upinzani.

Kumbuka Lowasa alizawadiwa nafasi ya juu kabisa ya kugombea uraisi kabla ya kufikisha hata miezi 3 ndani ya chama na kumtosa mkongwe aliekipigania chama kwa jasho na damu mh dr Wilbord Slaa ambae alikuwa ameshakipambania chama hicho kwa zaidi ya miaka 7. Pia kina Sumaye, Nyalandu, nk walipendelewa kwa kupewa nafasi mbali mbali ndani ya chama huku wakongwe wa chama hicho wakiishia kufanywa wapiga makofi tu mikutanoni. So nafikiri CCM iliamua kulichukua hilo kutoka Chadema na kulitumia.
 
Mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania walio wengi huko vijijini.huko Hadi mtendaji wa kata ni kama rais.wakipewa kofia na t-shirt wanaridhika.only that
Sio mtaji wa ccm, ulitakiwa kusema mtaji wa wanasiasa. Si unaona wenyeviti wote wa upinzani kila mmoja na muda wake, wamekwenda kuonana na mama wakalambishwa asali na kufunga midomo yao.
Sasa hivi ni mwendo wa ndio mama, hata ile mizunguko ya kudai katiba mpya iliyokuwa inafanywa na mwenyekiti fulan wa upinzani imezimika ghafla mara baada ya kutoka ikulu. So ukitaka kujua kama mtaji wa wanasiasa wote ni ujinga wa wafuasi wao. Mpaka leo hakuna mtu aliefunua kopo lake kuhoji kuhusu ukimya huu wa viongozi wao pamoja na zile safari za ikulu.
Labda nikuulize wewe ambae unajiona sio mjinga, je ushawahi kuhoji lolote kuhusu safari za wenyeviti wenu kule ikulu na ukimya wa harakati zao walizozianzisha kabla ya kwenda kulamba asali zimeishia wapi?
 
Nchi yoyote ikiwemo Tanzania huwa na makundi matatu ya kuamua mustakabali wa nchi kupitia demokrasia. Makundi hayo ni 👇
Naona unajaza tu maneno kwenye mada yako yasiyokuwa na maana yoyote.
Hiyo "demokrasia" inatoka wapi wakati CCM imehodhi kila kitu?

Hivi unapoandika haya mambo unaweka fikra kweli kwa unayoyaandika?

Nimechoka kusoma hayo mengine uliyoweka huko chini.
 
Nimekuelewa vizuri mkuu. Lakini hili ni wazo lako pengine na wenzako, sio wazo la watanzania wote including myself.

Nchi yoyote ikiwemo Tanzania huwa na makundi matatu ya kuamua mustakabali wa nchi kupitia demokrasia. Makundi hayo ni 👇
1) Kuna kundi ambalo huwa upande wa chama tawala. Lenyewe humpigia kura mtu aliepitishwa na chama chao ili agombee uraisi, ubunge, udiwani nk, haijalishi mgombea ana sifa nzuri au mbaya.
2) Kuna kundi ambalo huwa upande wa vyama vya upinzani. Kundi hili nalo pia huwapigia kura watu waliopitishwa na vyama vyao ili wagombee uraisi, ubunge, udiwani nk. Haijalishi wagombea hao wana sifa nzuri au mbaya.
3)Kundi la mwisho hili halina chama au linachama lkn huwa linamchagua mtu kwa kufuata tu sifa za mtu alie katika kinyang'anyiro cha uraisi, ubunge, udiwani nk.

Sasa unaposema kuwa CCM inahitajika kutoka hata sasa hivi bila kujali chama au mtu atakaeingia baada ya CCM kutoka madarakani, sikupingi maanake huo ni mtizamo wako wewe na wenzako. Ila kuna mtizamo wangu mimi na wenzangu ambao baada ya kuangalia aina ya upinzani uliopo nchini, na sifa, matendo au tabia za wagombea mbali mbali wa uraisi, ubunge na udiwani waliopitishwa na vyama vyao kugombea nafasi hizo nchini. Sisi kwa mtanzamo wetu tunaona ni afadhali mara 70 CCM iendelee kubaki kuliko wao kuingia ikulu. Maana tabia zao hazina tofauti na zile za CCM au pengine ni zaidi ya zile za CCM. So huwezi kusema kuwa mimi siipendi harufu ya mkojo nyumban kwang, lkn wakati huo huo unaona sawa tu kuishi katika nyumba ambayo nyuma ya dirisha kuna shimo la choo linalotema harufu ya kinyesi. So hapo ndio tunapopishana. Katika CCM kuna mafisadi, waongo, wachumia tumbo na wanafiki, na katika upinzani vyama vyote kuna mafisadi, waongo, wanafiki na wachumia tumbo.
Naona unao muda mwingi sana wa kupoteza.
 
Naona unao muda mwingi sana wa kupoteza.
Haya mkuu yameisha. Kila mtu na akili yake, msimamo wake, na maamuzi yake.

Acha wanaotumiwa kama daraja na hawa wanasiasa uchwara watumiwe.
Na wale waliochoka kutumiwa au kukataa kutumiwa kama daraja kwa faida ya hawa wanasiasa uchwara pekee na familia zao waendelee na maamuzi yao ya kutotumiwa.

Shukran sana kwa uchangiaji wako ambao naamini kuna waliojifunza kupitia yale uliyochangia kweny mada. Na kuna waliojifunza kupitia yale niliyochangia pia kwenye mada.
Ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom