Mtu huyu akisimama na mgombea wa CCM mwaka 2025, ni lazima CCM tuangukie pua

Hili la kupewa vyeo baada ya kuunga mkono juhudi nafikiri CCM wameiga au wamejifunza kutoka upinzani.

Kumbuka Lowasa alizawadiwa nafasi ya juu kabisa ya kugombea uraisi kabla ya kufikisha hata miezi 3 ndani ya chama na kumtosa mkongwe aliekipigania chama kwa jasho na damu mh dr Wilbord Slaa ambae alikuwa ameshakipambania chama hicho kwa zaidi ya miaka 7. Pia kina Sumaye, Nyalandu, nk walipendelewa kwa kupewa nafasi mbali mbali ndani ya chama huku wakongwe wa chama hicho wakiishia kufanywa wapiga makofi tu mikutanoni. So nafikiri CCM iliamua kulichukua hilo kutoka Chadema na kulitumia.
 
Mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania walio wengi huko vijijini.huko Hadi mtendaji wa kata ni kama rais.wakipewa kofia na t-shirt wanaridhika.only that
Sio mtaji wa ccm, ulitakiwa kusema mtaji wa wanasiasa. Si unaona wenyeviti wote wa upinzani kila mmoja na muda wake, wamekwenda kuonana na mama wakalambishwa asali na kufunga midomo yao.
Sasa hivi ni mwendo wa ndio mama, hata ile mizunguko ya kudai katiba mpya iliyokuwa inafanywa na mwenyekiti fulan wa upinzani imezimika ghafla mara baada ya kutoka ikulu. So ukitaka kujua kama mtaji wa wanasiasa wote ni ujinga wa wafuasi wao. Mpaka leo hakuna mtu aliefunua kopo lake kuhoji kuhusu ukimya huu wa viongozi wao pamoja na zile safari za ikulu.
Labda nikuulize wewe ambae unajiona sio mjinga, je ushawahi kuhoji lolote kuhusu safari za wenyeviti wenu kule ikulu na ukimya wa harakati zao walizozianzisha kabla ya kwenda kulamba asali zimeishia wapi?
 
Nchi yoyote ikiwemo Tanzania huwa na makundi matatu ya kuamua mustakabali wa nchi kupitia demokrasia. Makundi hayo ni 👇
Naona unajaza tu maneno kwenye mada yako yasiyokuwa na maana yoyote.
Hiyo "demokrasia" inatoka wapi wakati CCM imehodhi kila kitu?

Hivi unapoandika haya mambo unaweka fikra kweli kwa unayoyaandika?

Nimechoka kusoma hayo mengine uliyoweka huko chini.
 
Naona unao muda mwingi sana wa kupoteza.
 
Naona unao muda mwingi sana wa kupoteza.
Haya mkuu yameisha. Kila mtu na akili yake, msimamo wake, na maamuzi yake.

Acha wanaotumiwa kama daraja na hawa wanasiasa uchwara watumiwe.
Na wale waliochoka kutumiwa au kukataa kutumiwa kama daraja kwa faida ya hawa wanasiasa uchwara pekee na familia zao waendelee na maamuzi yao ya kutotumiwa.

Shukran sana kwa uchangiaji wako ambao naamini kuna waliojifunza kupitia yale uliyochangia kweny mada. Na kuna waliojifunza kupitia yale niliyochangia pia kwenye mada.
Ubarikiwe sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…