Pre GE2025 Mtu kama huyu anawezaje kusimamia uchaguzi CHADEMA wakapata haki yao?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna vyama gani vingine vya upinzani hapa nchini? Vingine si matawi ya CCM yale? CHADEMA ndio wapinzani pekee hapa nchini!
Hata ndani ya CHADEMA wapinzani ni wachache mno, yaani wa kuwahesabu

Ukitaka kujua hili na kwamba Watu hawatarget Ruzuku tu, angalia kama watasusia Uchaguzi Mkuu wa Mwakani kama walivyosema

Juzi Katibu Mkuu alisusa kuendelea na kikao kwasababu Nchimbi wa CCM hakuwepo, Je Uchaguzi kwa Tume hii hii atasusia?
 
Hao chadema wenyewe mbona hata kwenye chaguzi zao za ndani mbona hawakuwa fair to each other? Au wewe hukusikia mizengwe ya wazi iliyofanywa kwenye chaguzi za wenyeviti wa Kanda, hususani kanda ya nyasa?
Wazee wa maporini upo? Huko maporini mnafanyaga nini ndugu DC?
 
Wazee wa maporini huko kuchakata matokeo mpo??

Daah Mungu kawashika vibaya mno.
 
CHADEMA kwenye chaguzi zao tu kuna rushwa na mizengwe kibao. Wangeshughulika na mambo yao kwanza. Nchi inaendeshwa kisheria na sio mihemko. Hakuna sheria iliyovunjwa na huyo mama kwa yeye kuwa mwanaCCM
 
CHADEMA kwenye chaguzi zao tu kuna rushwa na mizengwe kibao. Wangeshughulika na mambo yao kwanza. Nchi inaendeshwa kisheria na sio mihemko. Hakuna sheria iliyovunjwa na huyo mama kwa yeye kuwa mwanaCCM
Hebu jibu swali hili kimantiki.

Simba na Yanga ziwe zinacheza mechi yao ya mwisho ya ligi. Yanga ikiishinda Simba inakuwa bingwa na Simba inashuka daraja ama Simba ikiishinda Yanga inakuwa bingwa na Yanga inashuka daraja.

Refarii wa hiyo Mechi awe Ahmed Ally au Ally Kamwe. Unadhani Simba itakubali mechi ichezeshwe na Ally Kamwe ama Yanga nayo itakubali ichezeshwe na Ahmed Ally?

Simba au Yanga unavoona wewe wataelewa kuwa hao watu watafuata Sheria 17 za Mpira bila ya upendeleo?
 
CHADEMA na vyama vingine vya siasa mkiendelea kushiriki uchaguzi chini ya usimamizi wa uvccm, UWT, na makada wengine wa CCM! Msahau kushika dola. Mkijitahidi sana mtaishia kupewa ubunge na udiwani.

Binafsi mwisho wangu wa kupiga kura ilikuwa ni 2015! Baada ya hapo niliapa sitokuja kushiriki kwenye maigizo yanayoitwa uchaguzi.
 
Sasa njia ya kufanya ni nini ndugu yangu. Maana Kila watu wakienda mahakamani ili mahakama itende haki mahakama inapata kigugumizi kutenda haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…