Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani?

Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani?

Corona haiwezi kuja Tanzania kwa kupiga magoti na kuomba kwamba Corona njoo, never. Corona itakuja tu Tanzania kama kuna "Epidemiological link" kwa hiyo aliyesema anaomba Corona iingie nchini ametia Lugha hiyo kufikisha ujumbe kwa aliyekusudiwa juu ya hali ilivyo kwa wapinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal Mayalla kwa hizi ID's fake hapa sidhani kama ni sahihi kumlaumu Mtu,

Huwezi jua pengine Umem-quote Baba wa Saanane au yoyote ambaye ameumizwa na serikali hii ya Jiwe Kama Kina Lissu. Ni Mfano tu.
 
Najua P Mayalla una lengo la kuwa expose wengi zaidi. Hujaacha kile ulichomfanyia Kabendera.

Lengo lako ni comments kama hizo zitiririke hapa upeleke file huko.

Una roho mbaya sana, ila watu tu hawakujui.
kweli huyu jamaa anapepo la ukiherehere lenye nyota ya roho mbaya....
 
Mkuu P

Agiza tu kajikombe cha kahawa ukunywe mwanawane, utajipa msongo wa mawazo bure na haya mandondocha ya Dj. Aikael

Wamemuazima common senses zao Dj. Aikael wao wamebaki na ile pombe pendwa aina ya komoni kichwani na vinywani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasco umeona watu walivyo kosa uzalendo??? Hii yote ni kwasababu ya viongozi wetu wanayoyafanya kukandamiza/kuumiza/kuua/kuteka/kutesa kwa kisingizio Cha uzalendo.

Chuki imefika pakubwa umoja na mshikamano kwa Tanzania unazidi kufifi toka awamu ya tano imeingia madarakani.
Hao ni kama tone kwenye bahari na kamwe watu vibwengo na wenye akili mgando kama hao hawakosekani kwenye nchi aina yeyote ile duniani.

Ukienda kwenye page za Trump katika mitandao unaweza kuhisi yule rais muda wowote kinanuka raia wanamtoa kwa nguvu.

Kwahiyo hawa wajinga wachache humu mitandaoni wasikupumbaze..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ni kama tone kwenye bahari na kamwe watu vibwengo na wenye akili mgando kama hao hawakosekani kwenye nchi aina yeyote ile duniani.

Ukienda kwenye page za Trump katika mitandao unaweza kuhisi yule rais muda wowote kinanuka raia wanamtoa kwa nguvu.

Kwahiyo hawa wajinga wachache humu mitandaoni wasikupumbaze..

Sent using Jamii Forums mobile app
Naam, hao wajinga wachache wa kwa Trump nao wanatekwa na kupotezwa?
 
Huyo boya ayeombea corona ni wa kupuzwa. Stress za maisha zinamtesa. Anadhani hata asipoombea ikijia yeye na ndugu zake watabaki salama?
 
Wanabodi

Japo kwa kawaida usiku ni wakati wa kulala na kupumzika, ila kwa watu ma jobless wakiwemo kada yangu ya watu wa "mishe mishe", moja ya usiku ngumu sana, huwa ni usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu ambayo umeipitisha weekend kwa mazabe mazabe, halafu blue Monday inakuja!, usingizi huwa unakata mapema sana, by saa 9:00 usiku, usingizi umekata, hivyo huna jingine lolote la kufanya zaidi ya kushuka JF, ndipo unakutana na taarifa za Corona, usingizi unakata kabisa unakuwa full awake!, hivyo kushuka na makala hii "Kwa Maslahi ya Taifa".

Hii ni thread ya swali tu linalohusu uzalendo na kutanguliza mbele maslahi ya taifa, nikiuliza, hivi mtu kama huyu ni binadamu mwenzetu au shetani? Anaombeaje ugonjwa wa Corona ufike nchini kwetu Tanzania ili kuikomoa serikali? Mtu kama huyu ni mzima kweli au ni mwendawazimu? Kuiombea nchi yako majanga, sio ni zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani huu?!

Hivi kweli kuna Watanzania wenzetu wenye akili zao timamu kabisa, kwa vile wao sio CCM hivyo wana chuki ya ajabu na serikali ya Magufuli mpaka kufikia hatua ya kuiombea nchi yetu majanga kwa kuomba janga la ugonjwa wa Corona litue nchini mwetu ili kuikomoa serikali kwa kuona jinsi itakavyo kabiliana nalo?!

Corona ikija, atakayeteseka ni serikali au ni mwana CCM pekee?!

Swali hili ni kufuatia nilikuwa nafuatilia thread fulani humu JF, nikakutana na mchango wa ajabu sana wa mwana jf fulani


Duh...!. Kweli is this what you wish for your beloved country Mama Tanzania?.

Huu sio zaidi ya uendawazimu? huu sio ni ushetani kabisa huu?

Pamoja na vitendo vya kiendawazimu na vya kishetani wapinzani wanavyotendewa na serikali yetu, kweli tumefikia kiwango cha Watanzania wenzetu kukosa utu na kugeuka wanyama kwa kuombea majanga yalikumbe taifa letu eti kwa sababu tuu kuna wendawazimu fulani serikalini wanafanya vitendo vya kiendawazimu na kishetani kwa wapinzani, hivyo sasa kuombea ushetani huu utokee kwa serikali yetu kuadhibiwa na janga la ugonjwa wa Corona? Hivi hii Corona ikiingia, atakayeathirika ni serikali ya CCM au ni Watanzania wote akiwemo mwendawazimu huyu?

Nasisitiza ule wito wangu wa siku zote kwenye hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", kwenye issues za kitaifa yakiwemo majanga mbalimbali, Watanzania tusimame pamoja kwa uzalendo, umoja, upendo na mshikamano na serikali yetu kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, regardless political affiliations zetu, sisi Watanzania lets pray and stand as one against Corona.

Mungu tuepushie mbali hili janga la ugonjwa wa Corona.

Mungu Ibariki Tanzania.

Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
Rejea
Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!

Uzalendo wa ajabu wa watanzania, unafurahije wakati nchi yako imepata majanga. Hawa ni ma nunda, ma sadist or what?
'Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo'
'Spare the rod and spoil the child'
 
Kwahiyo wew ulitakaje, serikali yako iendelee kutesa upinzani na kuwavunja mikono.. Si bora uje ili hao police na serikali yako iogope kuwashika upinzani na ipambane na corana na ikiwezekana watu Wa ccm waupate huo ugonjwa ili waache kuwatesa na kuwavunja mikono wapinzani.. Tena na wewe ulivyo mnafiki uupate ili uache unafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
 
Pascal Mayalla,
P.
Umetikisa kibuyu kilichojaa nyongo na pilipili kuwa mvumilia nyongo itapikwapo harufu yake inaweza kumtapisha Anae uguza pia,
Hasira zetu hazichagui Neno bora wewe umeanzisha Mada ya kututapisha nyongo zetu acha tutapike tu.
Hakikaa kumbe Taifa limefikia hapa...?!!Nani anatufanya tuwe wamoja tena??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Turnkey, Shenz kabisa , hujui kwamba Corona inathili watu wa umri wote.
Pili hata ukipona kunauwezekano wa kuaribika kwa Baadhi ya organs za mwili kama figo na ini.
Unajua siyo tu kupata Corona bali athali zinazotokana na CODIV 19

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona povu....ukiona hivyo hii comment sio kwa ajili yako..nimekaa nchi za Magharibi kwa miaka mingi...wakati wa baridi
wazee wengi wanakufa sana ..mbona hawatangazagi
 
Kwa hiyo izo nchi ambazo corona imesha ingia wameomba.watu sijui mmekula maharage ya wapi,kama imepangwa kufika itafika hata watanzania wote tukakeshe nyumba za ibada.
mnakaa kuandika uupuuzi tu.eti uzalendo mbona ukimwi uliingia wazalendo mlikuwa wapi kuomba usiingie...haya nyinyi wazalendo mmejiandaaje kupambana huu ugonjwa usiingie au ma dj kutoa tangazo katikati ya show..mnaogopa kufa kamaipo ipo tu.SHARUBATI....!!!!!$€¥₩₩😡😡😡😡😡😡😡
 
Back
Top Bottom