Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MTU KUMSIKILIZA MCHUNGAJI AU SHEIKHE ZAIDI NI DALILI YA KUKOSA BABA AU KUWA NA BABA DHAIFU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Hii ndio sababu wewe kijana wa kiume unatakiwa upambane Sana sio kiuchumi tuu Bali Kimwili, Kiroho na kiakili.
Kama Baba unahitajika ujue mambo mengi Sana. Mambo Mengi Sana tena Sana kwaajili ya kukamilisha ule utukufu wa Ubaba.
Baba sio kumwaga tuu mbegu kwa mwanamke akazaliwa mtoto.
Baba ni kuwa Legendary, Role model kwa kizazi utakachoenda kukianzisha.
Na ndio maana wanawake wengi wenye Akili za kianamke na sio kisichana wanahitaji mwanaume Halisi ambaye anaakili, ujuzi na maarifa ya kutosha, awe na nguvu za Kimwili kumaanisha ajue mapigano ya hapa na pale kwa kujihami na kulinda familia yake na pia awe na uchumi imara.
Lazima ujue kuwa ili watoto wakuheshimu na kukuona Role model wao au legendary wao. Ni lazima mwanamke uliyezaa naye yaani Mama yao akuone katika lile jicho la mwanaume Halisi. Akuheshimu na kujivunia.
Masuala yote basics na elimu na ufahamu wa kawaida lazima mwanaume uwe nao. Uwezo wa kuchambua na kufafanua mambo lazima uwe nao kwa Sababu wanawake huamini mtu anayeweza kuchambua na kufafanua mambo kwa ufasaha huyo ndiye mwenye AKILI.
Ukiona Mkeo anamsikiliza mchungaji kuliko anavyokusikiliza wewe, anamuamini mchungaji au Sheikhe kuliko anavyokuamini wewe. Ujue tayari unatatizo la MSINGI.
Hii sio hiyari. Ni lazima uhakikishe Mkeo akuone wewe uko smart(unaakili Sana) yaani aamini kuwa unajua mambo mengi Sana. Kiasi kwamba kwenye maswali yake kumi basi anauhakika maswali Nane utajibu kwa ufasaha.
Hasa Yale maswali ya reasoning.
Mwanaume hutakiwi Kutafuta huruma Kwa mtu yeyote kwa Sababu kutaka kuonewa huruma ni dalili ya kuwa wewe ni dhaifu.
Wanawake wakati mwingine hujitia hamnazo. Huigiza kama hawajui lolote na kujifanya watoto wakikuuliza uliza maswali ya hapa na pale mengine maswali ya KITOTO au yakijinga Kabisa.
Maswali hayo yanamaana kubwa Sana kwao hasa Kipindi cha mwanzo cha mahusiano yenu.
Wakati mwingine sio kama hawajui Majibu ya maswali waliyouliza. Hujizima Data Kwa lengo la kutaka kujua ufahamu na akili ya Mwanaume aliyenaye.
Mwanamke akuzidi yote lakini sio AKILI.
Kwa sababu ni akili ndiyo hutumika kumtawala mwanamke tofauti na wengi wanaofikiri kuwa Pesa ndio inatumika.
Pesa ni muhimu Sana katika mahusiano lakini kama huna Akili ya kutosha mwanamke anaweza kukuendesha kama gari bovu na asikuheshimu kama hauna Akili kumzidi.
Kumbuka mwanamke hujua kupanga formation na kujua ni wakati gani wa kukushinda hasa ukiwa na akili mgando.
Lakini ukiwa very smart mwanamke hujua Kabisa wewe ni smart na unajua namna ya kumkabili bila kupata madhara.
Kijana lazima ujifunze haya ili uwe mwanaume na Baba Bora na legendary na Role model kwa wanao;
1. Lazima ujifunze maarifa,ujuzi na ufahamu wa mambo mengi.
Yaliyopita, yaliyopo na yatakayokuja.
Uanaume sio Kazi ndogo.
Sio ukae kivivu na kizembezembe na kuleta visingizio visivyo na kichwa Wala miguu.
2. Lazima ujue na ujifunze kujilinda na mapigano.
Mwanaume lazima ujue kujilinda, maloganyna kutumia silaha.
Hivi utoto wako wote ulikuwa unafanya nini.
Hata tufanye mazingira ya utoto ulikuwa unaamuliwa. Sasa umekuwa kijana nini kinakuzuia kujifunza Mapigano, kujilinda na kutumia silaha.
Hivi unajua wewe ni mwanaume?
3. Lazima uwe mtafutaji na uhakikishe unaweza kujimudu kiuchumi.
Hupaswi kumtegemea yeyote Yule isipokuwa Mungu wako.
Lazima ufanye Kazi na sio kudharau Kazi.
Kazi ni Kazi ila kitakachokupa kipato kizuri ni namna unavyoifanya hiyo Kazi.
Ukishakuwa sio mtafutaji uanaume wako unaanza kuingia dosari. Lazima Tabia za kikekike zikuingie.
Kujikombakomba kwa Watu. Kujiliza Liza na Kutiatia huruma mbele za watu.
Hivi kama sio mchakarikaji hata huo uanaume wako utaonekana Kweli?
Uanaume ni uchakarikaji.
Angalia hata wanawake wachakarikaji huanza kuwa na hulka ya kiume. Kwa sababu ya kujiamini kunakosanabishwa na uwezo wa kujitegemea wao wenyewe.
4. Lazima ujifunze utamaduni, Mila na desturi zako zikukae vizuri.
Lugha yako lazima uijue.
Dini yako lazima uijue vilivyo.
Historia ya familia na ukoo na kabila au taifa lenu lazima ulijue vizuri.
Mwanaume asiyejitambua unakuta hajui mambo ya msingi yanayomhusu yeye mwenyewe.
Ni jukumu Lako kama Baba na mwanaume kujua yote hayo maana baadaye utakuwa Mwalimu na role model kwa Mkeo, watoto na kizazi chako.
Sio unakalia vitu havieleweki. Huna focus, huna vision Wala mission.
5. Mwanaume lazima ushiriki kwenye jamii yako.
Lazima uwe na Tija.
Uanaume ni kuwa na Tija kwenye jamii yako.
Lazima uwe na mchango iwe wa kifedha, kiujuzi, kihuduma au Jambo lolote kwenye jamii unayoishi.
Watoto wako, Mkeo na Wazazi wako wanakuwa very Proudly kuwa na kijana kama wewe ukiwa na Tija kwenye jamii yako.
Tija sio lazima iwe Fedha maana kuna watu wenye Akili ndogo ambao watasema sasa kama Sina fedha nitachangia Jambo gani kwenye jamii.
Kila mtu anakitu cha kuchangia kwenye jamii yake.
Kama jina pesa basi unakipaji Fulani, au Una ujuzi Fulani, au unatoa huduma Fulani au unaweza kutumia nguvu zako za Mwili kuisaidia jamii yako.
Uanaume ni Tija.
Mwanaume huwezi kupendwa burebure.
Anayependwa burebure ni mwanamke. Yaani kupendwa burebure ni kupendwa kwa kuonewa huruma.
Moja ya dalili ya kuwa umependwa burebure au unataka kupendwa burebure ni kuogopa kuachwa na mwanamke.
Wewe mtu mwenye thamani uliwahi kuona wapi akaogopa kuachwa?
Hiyo itakuwa hasara kwa anayemuacha.
Ni jukumu letu Sisi kama vijana kuyazingatia mambo haya.
Ninafahamu Dunia ya Leo imebadilika kwa kiwango Fulani. Mfumo uliotengenezwa na binadamu kuhusu ajira ndio umeleta kitu kinachoitwa Ukosefu wa Ajira.
Lakini kiasili hakuna janga la ukosefu wa ajira kwani Kazi zipo nyingi na Dunia ipo kwaajili ya kuhudumiwa na kuhudumia maisha ya watu (yako).
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam q