Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?
Nadhan hujui maana ya elimu hivyo hata wewe nadhan ni mjinga tu
 
Mdogo wangu alipomaliza certificate ya udactari(ACO) akaniambia dada nataka kufanya biashara sitaki kurudi nyumbani.Bahati nzuri wakati huo nilikua na kwenye office ambayo inaajiri watu kwa muda na wanalipwa laki moja kwa siku ,nikamuunganishia akapata siku 10 akanunu anguo za mtumba akaanza kutembeza.biashara haikua nzuri sana wengi walikopa hawakurudisha .baadae okatokea Tena ile kazi akapata siku Saba akanunua belo la nguo za watoto akafungua na frame.baada ya happy wazungu wanasema the rest is history.sasa hivi duka linaenda vizuri amefungua maabara kubwa tu haombi Tena hela na mara pengine nikikwama huwa ananivusha amekua msaada sana kwa wazazi Ni Kati ya wadogo zangu najivunia sana na najifunza mengi toka kwake.Juzi kapata nafasi ya kuendelea na diploma akawaomba walimu atokee nyumbani ili iwe rahisi kusimamia biashara zake wamemkatalia
Kwanza wanajua mambo yake wanamuonea wivu hata cheti cha certificate walificha wivu tu amekipata baada ya mwaka.
 
Asipuuzwe anaweza kufanya ufundi cherehani wa kiwango kikubwa kutokana na exposure amepata shuleni. Kufundishwa na darasa la saba sio issue maana mwanzo mdogo huwa haudharauliwi.

Changamoto ni pale ukiona anaanza kuridhika kuishi maisha ya cherehani kimoja miaka yote, hapo atahitaji msaada ila kwa sasa, apewe full support

Sent using Jamii Forums mobile app
 
me nauza samaki barabarani Mabungo Moshi nina degree ya elimu nlishafundisha kwa miaka mitano ila maendeleo nliyonayo kwa mwaka mmoja nlofanya biashara ni sawa na miaka mitano nlofanya kaz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana ameamua kujifunza cherehani ili alete cha tofauti na kumfanya akue maradufu kuliko mwalimu wake sababu ya elimu na uwezo wa kufikiri aliouongeza shuleni,
Sioni kama ni jambo baya ila inategemea ataamua kuifanya kazi yake kwa njia ipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uyo sema hana connection tu Lakin trust me iyo ni bonge moja la course yani. NGOs ndo wanawahitaji watu kama hao...tena upate masters yake ndo kabisa yan....unajua kuna baadhi ya kozi kama community development, child protection sijui ukiwa na connection tu ..yani unakuwa unazurura na wazungu tu
 
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.

Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?

Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!

Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.

Tunakwama wapi?

Kumbuka kuwa elimu ni ufunguo wa maisha, sasa amepata ufunguo anahitaji akaanze maisha.
Kwa kifupi elimu yetu haitupi ujuzi wa moja kwa moja au haitupi mbinu za kutumia kwenye jamii moja kwa moja kutatua changamoto za maisha.

Mfumo huu unhitaji ubadilishwe, kinachohuzunisha ni kwamba sioni mchakato ukianza. Tunahitaji tuufumue wote na kuanza upya.

Mwache akaanze huko alikoona, huo ni mwanzo tu, akianza ataunga na vingine huko mbeleni.
Pia usimdharau wa darasa la saba, inawezekana ana elimu ya maisha kuliko wengi wenye degree na masters. Mtazamo wako hauakisi kwenye maisha halisi ya jamii tunayoishi hivyo changanua tena halafu mpe dogo mashine akashone nguo, mengine yatajiset hukohuko.

Ahsante
 
Back
Top Bottom