Mtu mwenye degree anapoenda kujifunza kazi ya waliokosa Elimu ni ujumbe gani tunapata kuhusu Elimu yetu?

Acha porojo wewe kwa elimu hii ya kukariri slides.... Kongole kwa mpwa kuamua kujikwamua na kutumia fursa ambayo kaiona
 
Mahitaji ya dunia yanabadilika sana, Inatakiwa mshonaji ambae anaweza kumudu vitu kama lugha na matumizi bora ya mtandao namna ya kumudu masoko kidigitali zaidi kumpa huduma bora mteja ni ujuzi mwingine ambao hauji tuu ila kwa kipawa binafsi au elimu,na kucheza na soko linahitaji nini.

Atashona nguo lakini kwa kutumia elimu aliyonayo, na asiangalie kushona nguo tu afanye kwa malengo elimu iko pale kumsaidia kuongeza ujuzi wa hiyo biashara ndani ya miaka mitatu anaeza akawa tofauti kulinganisha na aliowakuta kwenye game au akapata mafinikio ya haraka hata kama si makubwa kiviile.

Issue ni kufanya hichohicho kitu kinachoonekana kawaida kwa namna tofauti ambayo huitwa ubunifu kwa lugha nyingine na ubunifu huanzia tangu mteja anapoingia hadi anatoka eneo la biashara na akitumia maarifa ya elimu aliyonayo ita msaidia zaidi.

kwa mwenye degree lazima ana ujuzi wa kompyuta basi eneo lake anaweka pc wateja wakija hata wanapata email za maendeleo ya nguo walizompelekea kutumia pinterest kucompare mishono ni vitu vya ubunifu tu si kazi rahisi .

Mteja ni kucheza na saikolojia yake, dunia inapobadili mweleko na wewe unageukia hukohuko hakuna namna.
 
elimu sio njia ya mafanikio ila elimu ni mwongozo wa kila binaadamu kwenye uso wa dunia unaposoma kuna vitu vingi sana atapata kuvielewa ambavyo ni msaada tosha kwenye maisha ya binaadamu wenye elimu wengi ni masikini duniani na wenye elimu ya kati ambayo haina msaada wowote duniani lakini ndo matajiri mkuu hivyo basi tuache tabia ya kuchukulia kwamba ukiwa na elimu basi lazima upate pesa au kazi nzuri tabia hii mbaya sana pia unaweza kuwa darasa la saba ila ukapata kazi nzuri sana na yenye mafanikio makubwa sana wengi tunao kwenye jamii zetu tukae tukitambua elimu ni chanzo cha maarifa tu na si chanzo cha mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mpe hongera,amebadilika kulingana na mazingira.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufikiri wa jamii, na wewe ukiwemo ndio shida, hakuna kazi za walioelimika na wasioelimika, shuleni huwa tunaenda kusoma ili kupanua mawazo yatakayo tusaidia katika kuendesha maisha yetu.

Sasa hizi degree tunasomea, mengi ni mambo ya utawala, ndipo unajikuta umesomea, utawala wa biashara, au maendeleo ya jamii, lakin, ni biashara gani unayoitawala? skills za hiyo biashara hauna, Au maendeleo ya jamii, je jamii inajihusisha na kazi zipi? hauna hiyo elimu.

Ni kweli kuna kashida kadogo kwenye mfumo wa elimu wetu, nao ni hako ka kuto incoroprate vocational training kwenye mafunzo yetu. Dogo kasoma, kaona anahitaji kujifunza cherehani, ili labda sasa aje atumie elimu yake ya chuo kikuu, kuendesha biashara ya cherehani, kwanza apatie mtaji,kisha ajikite huko. Wazo ambalo ni jema sana, na namuunga mkono 100%. Amini amini nakuambia, kwa moyo ambayo huyo dogo anaonesha, kuna kitu amekiona kwenye huo mchoro wake, na ndio manufaa ya elimu hayo. mwache aende, 5 years anaweza kuwa na story ya tofauti kuliko huyo fundi anaemfundisha? Je Haukusoma habari za mafundi vyerehani waliobahatika kutoka nchini mwetu hapa? Akina Speshoz, na Wengine, Kama Speshoz ni ana had masters kabisa, kaanza na kushona pia ila leo ana biashara kubwa ya fashion na sports. Sasa kwa nini kijana wa miaka 30, ndio anamikataba ya jezi kwa timu mbalimbali nchini, na ndo anaivalisha stars na Wasanii kama Diamondplatunuzm, anashina suti za harusi kwa bei karibu na mshahara wa miezi mitatu wa mwalimu mwenye degree? ni kwa sababu hakuwa fundi cherehani wa kawaida, nini kilimfanya asiwe fundi cherehani wa kawaida, ni Elimu yake ya masters. Na unajua ni kwa nini kwanini sio wote wenye elimu ya masters na hata wengine maprof hawaingizi mkwanja mrefu kama anaongiza yeye saivi? ni kwa sababu yeye nje ya Elimu yake ya mastars ana ujuzi, huo ujuzi ambao wewe unadhani dogo kapotea kuutafuta saivi. Ujuzi wa kushona.

So muache dogo afanye anachoona, na hayo ndiyo matumizi ya elimu.
 
Nyie mliokuwa mnanicheka mimi nilipofungua kibanda cha soda pale uhindini mbeya sasa ndo Mnaelewa. Wajinga waliobahatika kuajiriwa wakadhani maisha walionayo ni akili, kumbe ni bahati ya kuajiriwa tu, la sivyo mimi niliwazidi kwa kuwa niliendesha maisha bila kumtegemea mtu wala ajira. USHAURI. kwa maisha ya leo, ukiweza kumsadia mtu aliyemaliza chuo, msaidie, na hasa nyinyi mliobahatika kuajiriwa, maana si kwamba wewe una akili bali umebahatika tu.
 
Kuna jamaa mmoja ana masters ya sociology anauza nguo,ukiingia kwake anakuangaliaa akiona hufanani na nguo zake anazouza ana kushit.Nilikwenda kumnunulia mtu ila nikamkuta jamaa yuko busy na mteja wa design ya nguo zake,akani ignore ijapo nilikuwa na laki moja nilitaka kununua kitu hapo.Ilibidi niondoke tu.
Nilipouliza watu huyu jamaa ana shida gani!Ndipo nikaambiwa ni msomi kazi yake imebaki kutamba tu kuwa ana masters ijapo alipewa mtaji na ndugu yake ila biashara inataka kumshinda.
Amebakiza majigambo tu na jamaa kumbe wana mchoraa hajijui.

Naamini degree bado itakupa nafasi ya kutambia wanaume mtaani na kukupa nafasi ya kutukana na ukasikilizwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
YAANI WATANZANIA WANAIONA ELIMU KAMA HAISAIDII CHOCHOTE KWA SABABUBYA MIAKA HII MINNE TU AMBAYO AJIRA NYINGI ZIMESITISHWA. WAMEISAHAU KABISA MIAKA AMBAYO AJIRA ZILIKUWA NYINGI.

jamani tuwe wapole, mfano: kitu nilichosomea mimi kabla ya mwaka 2016, ajira zilkuwa zinatoka 50+ kila mwaka na ilikuwa inachukua watu wa course mbili ambazo zilikuwa zinazalisha si zaidi ya 25 graduates per year. Lakini october mwaka 2015 tuliingia chuo watu zaidi ya 40 kwenye course yangu tu na wenzetu walikuwa 20 na tume maintain hiyo trend mpaka leo, ingawa tangu 2015 ajira zinatoka si zaidi ya 5 kwa mwaka.

Sasa hapa tatizo ni kwamba ajira zimesitishwa ndio maana watu wanalazimika kufanya kazi yoyote.
Lakini mkumbuke kwamba ni kipindi tu, mda utafika mambo yatakuwa tofauti tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karatasi ya thamani ni pesa bro..hivyo vyeti sijui madegree ni uchafu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…