Mimi nilipoanza kujiuliza swali hili nilianza na wangapi walikua watoto wa Adam na Hawa? Je! Jina Hawa lilikua na maana ipi? Ukiangalia mukhtadha wa maswali yako lazima utarejea kwenye vitabu vya kiimani kulingana na dini uliyopo maana kote vitabu vimesimulia kila kitu ni wewe kusoma na kuelewa
Mfano: ukisoma kitabu cha Mwanzo ambacho kimeandikwa na Musa utapata kuona Adam na Hawa baada ya kutenda dhambi ya kufanya kinyume na maelekezo ya Mwenyezi-Mungu na kufukuzwa kwenye Bustani ya Eden walifanikiwa kupata watoto wengi na kati ya hao wanaosimuliwa kwa kuanzia ni wawili ambao ni Abeli na Kaini, baada ya Kaini kumuua nduguye basi Adam na Hawa walipata mtoto mwingine aitwaye Sethi na Sethi ndie aliendeleza uzao wa Adam pamoja na kwamba Adam na Hawa walikua na watoto wengine na ukisoma Bible inaeleza kwamba Adam alikua na watoto wapatao 80 wakati wa uhai wake, Sethi mwana wa Adamu ndie aliendeleza ukoo wa Adam mpaka kufika kwa Nuhu ambae alimpendeza Mungu na Nuhu akaendeleza mpaka kwa Abrahamu....
Maelezo ni mengi ukitaka kujua vizuri anzia kusoma kuhusu watoto wa Nuhu ambao ni Ham, Shem na Yafeti sasa soma kuhusu watoto wa Ham hapo utamkuta Kushi (Ethiopia) na Puti (Libya), hayo maeneo yameandikwa kwenye Bible jaribu kusoma utapata mwanga, kisha fuatilia kwa undani maana ya Cush (dark-skinned person of African descent) utapata mwanga zaidi