Mtu Mweusi [Mwafrika] sio uzao wa Adam na Hawa

Mtu Mweusi [Mwafrika] sio uzao wa Adam na Hawa

Awali ya yote ningependa kuwasalimu wanajamii wenzangu habari zenu, natumai ni wazima wa afya.

Nina maswali kadhaa ambayo ningependa kupata majawabu kutoka kwenu wana Jamiiforums yatakayo kuwa msaada na faida kwa jamii nzima na kubadili taswira na mtazamo wa jamii nzima juu ya asili ya mtu mweusi [ mwafrika ] na uwepo wake hapa duniani.

Maswali:
1. Je mtu mweusi[ Mwaafrika ] ni uzao wa Adamu na Hawa ?

2. Je Adamu na Hawa walikuwapo pekee duniani ? na Afrika kulikuwa hakuna watu?

3. Je uzao wa mtu mweusi ni kutoka ndani ya Afrika au nje ya Afrika ? Na Kama ni kutoka nje ni kutoka kwa nani watu wa bara la Ulaya [wazungu], watu wa Mashariki ya Kati, watu wa Asia ya mbali au watu wa bara la Amerika?

4. Je inawezekana mtu mweupe kwa mweupe [ mfano mzungu kwa mzungu ] kuzaa mtu mweusi?

N.b: Matusi na lugha za kuudhi hazitakiwi , pia unaweza kuongeza maswali yako kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
Hiyo dhana ya adamu na hawa ni uongo tu kutokana na ujinga wa binadamu. Na kuanzia hapo ndio kisa cha mtu mweusi kudhalilishwa kwa kuletewa imani za wageni.
 
Masela weusi hawa 😂😂
 

Attachments

  • black_dark_skinned_chinese_people_african_descent.jpeg
    black_dark_skinned_chinese_people_african_descent.jpeg
    31.8 KB · Views: 14
ishu ya Adam sijui Hawa ni conspiracy tu mkuu, zingatia mungu aliumba wanadamu kwa kuzingatia mazingira yaliyopo aliumba watu weupe,wekundu,weusi na,mchanganyiko kadili tunVyoingiliana tukaanza kuchanganya damu na kadharika.
 
Quran inasema mtu wa mwanzo duniani alikuwa mweusi,Science inasema mtu wa mwanzo katokea Afrika,..Afrika ni ya watu weusi

Hapo Dini na Science zimekubaliana, mazingira na chakula ndiyo yanayomfanya mtu abadilike
Mazingira na chakula yanambadilisha mtu? Mtoto wa kiafrika akizaliwa ulaya huwa anabadilika kuwa mzungu ee.
 
Mimi nilipoanza kujiuliza swali hili nilianza na wangapi walikua watoto wa Adam na Hawa? Je! Jina Hawa lilikua na maana ipi? Ukiangalia mukhtadha wa maswali yako lazima utarejea kwenye vitabu vya kiimani kulingana na dini uliyopo maana kote vitabu vimesimulia kila kitu ni wewe kusoma na kuelewa

Mfano: ukisoma kitabu cha Mwanzo ambacho kimeandikwa na Musa utapata kuona Adam na Hawa baada ya kutenda dhambi ya kufanya kinyume na maelekezo ya Mwenyezi-Mungu na kufukuzwa kwenye Bustani ya Eden walifanikiwa kupata watoto wengi na kati ya hao wanaosimuliwa kwa kuanzia ni wawili ambao ni Abeli na Kaini, baada ya Kaini kumuua nduguye basi Adam na Hawa walipata mtoto mwingine aitwaye Sethi na Sethi ndie aliendeleza uzao wa Adam pamoja na kwamba Adam na Hawa walikua na watoto wengine na ukisoma Bible inaeleza kwamba Adam alikua na watoto wapatao 80 wakati wa uhai wake, Sethi mwana wa Adamu ndie aliendeleza ukoo wa Adam mpaka kufika kwa Nuhu ambae alimpendeza Mungu na Nuhu akaendeleza mpaka kwa Abrahamu....

Maelezo ni mengi ukitaka kujua vizuri anzia kusoma kuhusu watoto wa Nuhu ambao ni Ham, Shem na Yafeti sasa soma kuhusu watoto wa Ham hapo utamkuta Kushi (Ethiopia) na Puti (Libya), hayo maeneo yameandikwa kwenye Bible jaribu kusoma utapata mwanga, kisha fuatilia kwa undani maana ya Cush (dark-skinned person of African descent) utapata mwanga zaidi
Unamaanisha seth alilala na ndugu zake?
 
ishu ya Adam sijui Hawa ni conspiracy tu mkuu, zingatia mungu aliumba wanadamu kwa kuzingatia mazingira yaliyopo aliumba watu weupe,wekundu,weusi na,mchanganyiko kadili tunVyoingiliana tukaanza kuchanganya damu na kadharika.
Ko Mungu aliumba Adam na Hawa wa Tunduma, akaumba Adam na Hawa wa Hong Kong, akaumba Adam na Hawa wa London, Adam na Hawa wa Chitoholi ama vipi?
 
Back
Top Bottom