Uchaguzi 2020 Mtu timamu hawezi kushangilia matokeo haya

.
 
Natumai wapinzani (naamanisha wapinzani halisi, sio wale wengine) wataandaa taarifa yenye ushahidi na maelezo ya kina ya faulo zote zilizotawala zoezi zima la "uchaguzi" kwa ajili ya ushahidi na kumbukumbu, kwa matumizi ya sasa na ya baadae.
 
Mimi huwa nasema huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia uovu wa CCM na Serikali yake
Twaweza walifanya utafiti wakaja na hitimisho lisemalo" wanaoshabikia ccm ni mbumbumbu".
 
Karatasi zilizobambwa ni "Genuine" kabisa, ndo kusema kua Tume walichapisha na karatasi za ziada wakawapa CCM.
Ndiyo karatasi zilichaoishwa pale Jamana Printing Company. Ambayo Mnyika aliwahi kuilalamikia kwenye press moja hivi.
 
Wanaojiita wana akili timamu wameshindwa na wanaoitwa hawajitambui!
Upande wa wasomi wakubwa wa nchi hii umeshindwa na wa la saba, wazee, watu wa vijijini na wasojua mambo!
Wasomi walisema safari hii wamedhibiti wizi wa kura kwa sababu walikua na wataalamu wakubwa wa IT sijajua waliteleza wapi wakafungwa magoli yote hayo.
Ni yeye ndo imeisha hivyo.
 
Hahah!

Kwanini ukugomea mwanzo kabla ya kampeni?

Ndio maana nawaona mnaigiza tu
 
Watanzania tunapenda sana utani ktk kuteua wagombea,
Ghafla inatokea tu Salumu Mwalimu kawa makamu wa Raisi!
Nilijua mapema sana kua ni utani huu maana haikua inawezekana!
 
Upinzani mnatakiwa msifanye maandamano ili muwakomeshe polisi na jeshi kwa sababu wamefanya mazoezi kipindi kirefu,
Mkiacha kufanya maandamano maana yake watakua wamejichosha bure na wasipate watu wa kupiga na marungu Yao mazito.
 
Watanzania ukishaonyesha dalili za ushari, dalili za kuleta uvunjifu wa Amani au ukajinasibisha na Mababeru, au ukasingiziwa Mambo hayo, basi sisi Watanzania tunachofanya, tunakukwepa tu.
 
Ni aibu sana kilichofanywa na tume haiwezekani nyaraka nyeti zipatikane mtaani
 


CCM B nao wameanza kutoka hadharani kulia maumivu! Tunawasubiria wale walio ahidiwa kuwa chama kikuu cha upinzani
 
Sasa nawewe hebu kawaulize Viongozi wako kuwa Kama walijua uchaguzi hautakuwa wa huru na haki kwanini walishiriki uchaguzi?

Kwani isingewezekana kususia Kama walivyosusia kwenye serikali za mitaa?
Tulia wewe kima, wapinzani walikuwa wawili tu: Tundu Lissu na Maalim Seif wengine wote walikuwa mapandikizi ya nyoka wa kijani. Tumeingiza timu uwanjani kuwazuia na hayo mapandikizi yasije yakahalalisha huu uchafuzi uliofanywa. Wakati mwingine muwe mnajaribu kuficha ujinga wenu!
 
Kama nchi tumejuabisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…