Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?


oooh my god!
 

nashukuru mkuu kwa mtazamo mzuri
 

nimekupata
mkuu habari hii ni muhimu kwangu
 
Nakuhakikishia ukikutana nae ghafla face to face yule mnyama atakuua tu hata akikupa nafasi ya kujitetea, mana hata ukijitetea yule mnyama hajui kiswahili. Labda utembee na bastola yenye risasi za kutosha muda wote.


Ahahahahahaaa mbavu zangu. Anajua lugha gani mkuu?
 
wanyama wote ni wakawaida sana ndio maana wanafugwa, mbaya ni binadamu ka alqued anakuua alau hakutumii, kama chakula. chui ni muoga kweli usikubali kumpa kisogo, akiruka kukudaka wahi mikono ya mbele, simba huyo muwahi ulimi kwani huwa hawezi kurudi nyuma anakua pale pale
 
tembea na kiberiti,,,,,pia hakikisha nguo zako zananuka petrol ili ukiiona simba au chui jipige kiberit....mwisho wa maneno....swali je ukikutana na chatu?
 
Hivi mmeshamuelekeza namna ya kujilinda na nyegere.......au mbuni.....?....porini kubaya jamani........
 
sala ni muhimu ila ishara za huyo mnyama sitaki anidhuru
Sala ni muhimu kwa kila kitu. Ishara gani tena mkuu unazungumzia!? Au Simba na Chui wakiwa wanakuja kukudhuru huwa wanaKUDIP (beep)!!??
Kama umeenda kuishi PORINI utakuwa umewafuata nyumbani kwao mkuu kwa hiyo huwezi kuwaepuka ni kuwa makini tu. Ni sawasawa na kwenda Bar ukaagiza mzinga wa Konyagi peke yako halafu useme Sitaki kulewa.
 
we chukua nguo kisha washa moto nasikia huwa wanatoka nduk cha muhimu ni kutembea na all sources of fire
 
Hivi mmeshamuelekeza namna ya kujilinda na nyegere.......au mbuni.....?....porini kubaya jamani........

Nishasikiaga habari za huyu nyegere kwamba ukiwa porini ukimtaja tu huyoo..tena wakaenda mbali zaidi wakadai wanapenda zaidi "HASHUA"..kwamba wanazinyofoa.
 
Hakikisha unamuakia...shkamooo uncle simba/chui...!baada ya hapo atakuona una nidhamu na kukuacha!!!haya kimbia sasa wahi huko porini tushakupa maujanja....

Jaman nimecheka kama mwehu hapa!! Mpaka machozi yametiririkaaaaaa......
 
Nishasikiaga habari za huyu nyegere kwamba ukiwa porini ukimtaja tu huyoo..tena wakaenda mbali zaidi wakadai wanapenda zaidi "HASHUA"..kwamba wanazinyofoa.

huyu mnyama nasikia ni rafiki sana na jinsia ya kiume...........bora ukutane na pride nzima ya simba kuliko nyegere mmoja.........kidudu kina kisasi kama binadamu vile...........
 

Unavyoongea utafikiri ushawahi kukutana na nyati vile!hebu kamsalimie pale mdonya -ruaha halafu jifanye uogopi,nenda selous kamtusi mama kiboko uone,pita serengeti kamshike ---- baba simba then uje tuambia kuwa ulisalimika kwa kuwa ulikuwa huwaogopi!hiyo siri yako baki nayo mwenyewe !hayawani ni hatari na wakalie mbali!
 

teh teh,we jamaa
 
Naanza na Chui; Ni mnyama anayependa kujitenga na muda mwingi anapenda kupumzika juu ya mti au chini ya vichaka vichaka vizito vizito/ambavyo havipitishi mwanga mpaka ndani. Kutembea kwake ni pale tu anapoenda kutafuta chakura/mawindo na hapendi usumbufu. Unapomuona Chui gafla na yeye hajakuona eye to eye contact we inamisha kichwa chako au angalia sehemu nyingine huku ukiendelea na safari yako. Pale mtakapogonganisha macho chakwanza akili mwake ni kujihami maana anajua umeenda pale kumuwinda yeye na anajua asipokuwa utamuwahi yeye. Chui ana asiri ya ufuatiliaji, akikuona na kama hujamuona anaweza kukufuatilia umbal wa hata 1km bila wewe kutambua kuwa nyuma yako anakufuatilia nia ni kujua huyu mtu ana nia mbaya nami au vip, akijiridhisha kuwa hawezi kupata madhara kutoka kwako anajiachia zake huyo.
Simba; Ni mnyama anayependa kutembea kimagrupu, ukimuona simba mmoja basi jua ndani ya mita 50 kuna simba mwingine au wengine. Mara nyingi hujigawanya pale wanapofanya mawindo maana wakiwa wanawinda hawapendi kukimbia umbari mrefu so wanajigawanya ili kupunguza usumbufu wa kupata windo lao hata kama windo litakimbilia upande flan basi hukuo kunakuwa na mwingine wa kumuinterupt huyo windo. Simba ana aibu sana mbele ya binadamu na ukikutana nae usioneshe uwoga wala kutetemeka wala usigeuke na kumpa kisogo simama mwangalie eye to eye contact mwishowe huyo atapotea zake. Nadhan nimekusaidia kidogo kwa nilichojifunza juu ya hawa wanyama.
 


Ndugu yangu nimepata darasa kubwa sana kwako, naweza kuamini usemacho maana kuna movie moja ya kisouth Africa inaitwa Mr. Bones, pale kuna sehem Vince Lee alikuwa anamuokoa mpenzi wake mbele ya simba, alichofanya jamaa ni kumkazia mimacho simba na kumtisha as if anaunguruma huku akijifanya anataka kumparamia, simba akawa kama anaona aibu akatimua mbio kwenda mapangoni. Hilo la chui nlikuwa sijua ndo nimepata darasa kwako kiongozi. JF unapata burudani (kwa comments ridiculous za baadhi ya watu), unacheka, na pia unapata darasa la kutosha, kila nikipitia nyuzi za humu natoka na kitu kichwani ambacho nilikuwa sijui. Viva JF.
 
Mkuu,
Hapo kwenye Red umenipoteza kidogo. Hao Simba wenye aibu wako pori gani mkuu? Au ni Simba wa kinyaturu?
Kuna binadamu gani,let alone MTANZANIA wa kuweza kumwangalia uso kwa uso au macho kwa macho!!??? Maana haya Mapaka ya huku uswahilini tu yanatutoa Jasho kuyaangalia machoni sembuse ukikutana na Simba mkuu.
Haya mambo ya Indiana Jones tuyaache kwenye sinema tu ndugu zangu. Asilimia 80 ukikutana na Simba ana kwa ana itakuwa ndio Ze Endi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…