Mtu ukikutana na simba au chui ghafla porini tahadhari ni ipi?


Kuna wadau wamesema bora ukutane na hao wanyama sio binadamu, majangili yana shabaha kishenzi, yakikulenga hutoki!!
 
Vua nguo zote ukae uchi wa mnyama

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tupe elimu ya nyoka hata kwa kuanzisha thread mi ni muoga wa nyoka balaa tena huyo koboko

Koboko ni nyoka mpole sana na anaetumia kasi yake kuepusha shari. Akishtukia watu wanapita karibu yake anasepa zake, akiwaona wakati nyie hamjamuona wala hawashtui, anauchuna tu. Lakini akiona anatishiwa, atashambulia kwa kasi ya ajabu na atakung'ata zaidi ya mara moja (nyoka wengi wanang'ata mara moja tu) hadi utulie! mg10-15 zinatosha kukuua lakini yeye anatoa dozi ya 50mg-150mg! Na jina la black mamba kapewa sio kutokana na rangi ya mwili wake, bali kutokana na rangi nyeusi mdomoni anayoionyesha akiona anatishiwa. Lakini kuna wasukuma inadaiwa wanatibu sumu yake na kuna askari wanyamapori alinieleza hivyo japo sijathibitisha. The good news ni kwamba watu wanaposogelea makazi yake yeye anasepa!
 
pori la selou kaka

Hilo halina shida sana, uzuri wa game reserves wanyama waki sense kuna mtu karibu au wakikuona wanakimbia kwa sababu wanawindwa sana tu, hadi tembo!! Tatizo mkifumaniana gaflagafla lazima ajihami kwani anajua wewe ni mwindaji. Hakikisha unakuwa karibu na askari mwenye silaha.
 
Kwani koboko ndiyo black mamba, siyo kweli. Black mamba (swira) ni nyoka mfala mfala tu ambaye unaweza mpigia kinanda ukamkamata.
 
Kwani koboko ndiyo black mamba, siyo kweli. Black mamba (swira) ni nyoka mfala mfala tu ambaye unaweza mpigia kinanda ukamkamata.

Mkuu jaribu kusoma kabla hujapost, just google black mamba utapata majibu, swila wako kwenye genus Naja na genus ina species nyingi tu. Wanaopigiwa filimbi ni cobras ambao wengi wanapatikana India, japo kuna wasukuma wanawatumia kwenye ngoma zao. Pia black mamba (koboko) harushi mate, lakini swila anarusha.
 
Tupe elimu ya nyoka hata kwa kuanzisha thread mi ni muoga wa nyoka balaa tena huyo koboko



Koboko (black Mamba) wapo kila shemu hapa Tanzania, ila sana wapo Kigoma, Tabora, na mikoa ya kusini mwa Tanzania. Waanapenda sana kukaa maporini na sehemu isiyokuwa na kelele kwani wao hawapendi kelele. Wanaishi mapangoni ama juu ya miti na kuna aina nne ya hao koboko ama jamii yake. Black mamba (koboko halisi kwa hapa kwetu) wapo sehemu zote za africa isipokuwa kaskazini na magharibi. Green mamba (eastern green mamba) wapo hapa kwetu na sehemu zingine hapa Afrika mashariki na kusini, nao ukaa juu ya miti haswa miembe na machungwa ama miti yenye wajusi na ndege wengi huko maporini (chakula chao). Kuna Jameson's mamba (green mamba) hawa ukaa sana misituni na kwenye miamba ama mapango wanakula sana popo, hivyo kama kuna sehemu unafahamu ina popo wengi usiende huko kwani sumu ya huyu nyoka inaathiri mapigo ya moyo na central nervous system. Chances are; unaweza kuingia pangoni akakuona lakini akugusi ila ukitulia anakufuata because wako very curious na movement na wako very smart. Mwisho ni western green mamba ambao wana same characteristics na Green mamba ila wao wako primarily huko afrika magharibi. Kwa jamii zote hizi za hawa koboko, koboko amabye yuko very aggressive ni huyu black mamba kwani yeye ndiye nyoka mrefu zaidi hapa afrika mwenye sumu na anayekimbia shinda binadamu wa kawaida at 16–20 km/h, 10–12 mph. Mara zote akiwa anatembea kwenye mawindo yake huwa anakuwa anasimamisha kichwa kwa ajili ya ku strike hivyo kwa bahati mbaya kama akiwa cornered na binadamu anasimama kutaka kuzichapa na ukiwa karibu yake zaidi ndipo anakugonga na kama ukimrushia fimbo ama jiwe anajuwa kuwa unataka kumuua ndipo yeye anakuja kwa kasi zaidi akuwahi wewe. Kwa kifupi huyu nyoka ana akili sana. Chatu hana issue na tena mi naomba kila kukicha nikutane naye....kwani chatu kwanza hana sumu ila ni mkabaji (constrictor). Akikukamata lazima akukabe ndipo akumeze kama umbo lako dogo ila chatu hata simu moja hawezi kumeza mtu mwenye shibe, ni uwongo na it's never been proved before ni hadidhi tu za watu. Mkuu ukielewa destruri za nyoka hutawaua ama kuwaogopa kwani we need them kwa sababu bila wao our eco system itakuwa messed up kujawa na popo, chura, panya, vijusi na wadudu wengine ambao ni nuisance kwetu.
 



Huyu ndiye koboko halisi na tulimkamataga kwa ajili ya study huko Iringa in 2010 ila tukamwachia. For secuirty reasons siwezi bandika picha yangu niliyomkata huyu nyoka ila kama usemavyo mkuu, huyu nyoka hana shari na watu ila ije itokee umemziba njia na yuko mawindoni ama akihisi unamuwinda, ita Mungu wako na uishie kwa kusema Amen kwani you will NEVER be a live akikustrike kwa sababu sumu yake inaua mapigo ya moyo na kukufanya uchanganikiwe kabla hujafa. Yaani unachanganikiwa kwa sababu mapigo ya moyo yanashuka na unakuwa na kiu ya hajabu sana huku ukitokwa na povu mdomoni. Yaani huyu nyoka ni balaa ni sawa tu na king cobra wa India ila King cobra ndiye kipenzi changu kwani yuko aggressive zaidi na anakula nyoka wenziwe (wa aina yake) kwa kuwawinda kwani ni chakula chake.
 
Ni jambo jepesi sana. Ukikutana na wanyama hao mnyooshee mikono juu MOLA wako kwa maombi ya sekunde za mwisho za kuishi duniani ili usisikie maumivu wakiingiza meno yao kwenye mwili wako.
 

Ndomana nikasema uoga wako umetengenezwa na maisha ya mjini ambapo huko ulipo hawawezi kufika hata kwa kuota kwenye ndoto tu. Ndomana kwako ni rahisi kumuogopa paka wa usiku uswahilini. Siku ukikutana na chui au simba nadhani utafariki mwenyewe kabla ya hata huyo mnyama kuunguruma haha.
Sio mbaya kujua tabia za wanyama mbali mbali hata kama hauishi porini ila yawezakuwa ni hali yakutaka kufahamu mengi kuhusu wanyama. Nakushauri waweza kukuatana na watu wanaosomea mambo ya ETHOLOGY [The studies of wild animal behaviors] au hata hawa tour guides watakueleza mengi na ukafurahia elimu hii na jinsi unavyoweza kujiepusha na hatari za kina viboko, tembo, simba, chui n.k maana unawaogopa sana maaskari wa wanyama pori hahaha. Umenifurahisha uliposema watakuchukulia kama jangiri haha.
 

Ako Kwaang wewe ni wa kwetu kule dongobesh na tlawi?
 
Wakuu huenda nikaenda kuisha mazingira ya porini na nimekua nikisikia kuhusu wanyama wa kali ni hatari je hatua zipi nichukue kukabiliana na majanga tofouti tofauti nikiwa huko?

Haya mimi narudi kwenye topic.
Hii mbinu unaweza kuitumia kwa cat /dog types wote, nilipewa na mtaalamu mmoja, sijapata fursa ya kuitumia kwenye simba na chui (na siombei nipate hiyo fursa)

ukimuona tu simama kama vile umesimama mguu sawa (miguu pamoja, mikono to your side) halafu uangalie chini - strait to your feet... usi move... jamaa likianza kukusogelea anza kupiga makofi hatakugusa, akiona hubehave kama normal pray huyoo ataondoka zake hata kama ana njaa, (huwa hawali mnyama ambaye anabehave strangely) ....

usiplay dead nasikia wanajua jinsi ya kusikiliza pumzi na napigo ya moyo...
 
tembea na kiberiti,,,,,pia hakikisha nguo zako zananuka petrol ili ukiiona simba au chui jipige kiberit....mwisho wa maneno....swali je ukikutana na chatu?

Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaa
 

Mkuu,
Mbona unataka kutupeleka wenzio tukaliwe na Simba :shocked:. NIMESHASEMA SIENDI PORINI. HAYO NI MAKAZI YA WANYAMA. Kwa hiyo ukienda huko tegemea lolote. Mnyama wa Porini hazoeleki Kama huamini ukamuulize Siegfried and Roy Chui waliomfuga tokea akiwa mtoto (cub) alifanya nini ?


Mkuu,
Hizi zote ni Theory tu....Practically ni vigumu sana ukikutana na Simba au Chui umpigie makofi! Kwa lipi haswa zuri au jema alilokutendea!?
 


Yani Hawa black mamba sisi kwetu tunawakimbiza Kama mjusi na wanakimbia akipanda kwenye mti unampandie mpaka anajitupa huko Na akiingia kwenye mashimo chini ardhini unamfukua mpaka uumpate au akitokea upande mwingine akimbie! Na ukimshika anafata vile unavotaka!
Chezea Msukuma wewe!?
 
baba yangu mdogo alikuwa anatabia ya ulevi uliopindukia ,sasa siku moja usiku wa manane alikutana na chui,hakuangaika nae ,yule chui alimfuata 3kms mpaka anaingia ndani kwake nae akageuza akaondoka .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…