Tatizo lako ni kama la wengi TZ. Unajifanyanyisha na nchi tajiri. TZ sio Ujerumani wala China. Ni LDC. Huwezi kufananisha ili ujifiche nyuma ya pazia yao. Na narudia, "official language" status inatulazimisha tujue Kiingereza sio Kireno wala Kichina kama lugha ya pili ya nchi.
Kutaka sijui nijue kireno kwa kuwa niweze kuwasiliana na Waangola na Wareno ni point ya kijinga. Mazingira yangu ndio yaliyonipa access ya kujua Kiswahili na Kiingereza, Ninaishi Japan, nimejifunza Kijapani. Ningeishi Ureno ningejifunza Kireno. Nimeenda Lisbon na sijapata shida ya kuwasiliana na watu. Biashara kubwa ya kitalii inawalazimisha watu wengi kujua lugha za kigeni pamoja na Kiingereza kwa manufaa ya uchumi wao. Nimeishi Marekani, lugha ya Kihispanic ni ya pili baada ya Kiingereza. Nimejifunza chuoni kwa kuwa somo langu linahitaji lugha ya kigeni.
Nimeishi nchi tano za kitajiri na kutembea zaidi ya nchi 45 kwa kazi na likizo. Sijapata usumbufu wowote wa mawasiliano kwa kuwa Kiingereza ni lugha ya kimataifa. Ukifika Singapore, kuna arrival cards kwa lugha 10 kwa wageni kujaza, sijaona ya Kiswahili bado. Sasa jaribu kutumia Kisukuma au Kiswahili kama watakuelewa immigration! Hapo ndio utajua umuhimu wa kujua lugha ya kimataifa.
Swali. Kama wewe ukija Japan na lugha yako ya Kiswahili tu, na mimi nimekuja Japan na lugha ya Kiingereza na Kiswahili , nani kati yetu atapata ajira tukienda kuomba kazi pamoja? (assume tuna elimu sawa)