Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Hahaa...mtoto akiwa bright huhitaji kumpeleka mashule yenye majina makubwa sijui ada mil. 10. Mwache hapo hapo ila habari yake wataipata tu kwenye matokeo ya kitaifa. Mimi ilinigharimu niliposoma O-level private ambapo kila kipindi mwalimu anaingia, shida ikaja A-level mwalimu humwoni na material unajitafutia. Kwenye mazingira kama hayo ndo utamwona mwanafunzi ambaye ni kichwa.....
 
Nadhani serikali ijaribu kubuni mfumo mzuri utakaojengea wanafunzi ufahamu na uelewa wa kusoma na kuweza kutatua changamoto za mazingira yetu. Sio kusoma ma theory tu yaliyo solve nchi za ulaya na kusahau mazingira yetu na changamoto zake.
Pia sikuhizi primary hesabu ni mutliple choice, huko si ndo kufanya watoto wawe wavivu.
 
Mkuu punguza makali, shule za International kwa utawala wa huyu jamaa ni kazi
TRA hilo swali huwa wanauliza unasomesha watoto wako shule ipi?, sijui unakazi gani, Biashara nk takataka
busara ungesema shule za kulipia kuliko hizi za Kata walimu wana hasira zao wao bora liende
 
Hivi inamaana hatuwezi kubadilisha mitaala ya hizi shule zetu ziwe kama za kimataifa. Najiuliza tu. Kwani hatuwezi au ni nini shida
... kwa upande wa HR unahitaji kuondoa, kujengea uwezo, na kuajiri walimu zaidi ya 100,000 sio mchezo. Hao utakaowaondoa inamaanisha lazima "redundancy" ipite sasa malipo yake ndio balaa; piga hesabu hapo kila mmoja alipwe average 100,000,000 unazungumzia more than 10tr/- redundancy ya walimu halafu uanzishe ajira mpya ku-replace hao walioondolewa. Hiyo ni HR peke yake; njoo kwenye miundombinu; vitabu; n.k. Si mnataka ISO-certification?
 

Kwa Uandishi huu wewe huwezi kuwa umepita kwenye International Universities.

Unatudanganya.
 
Umenena mkuu. Siku hizi kila mwenye nafasi anapanga lake analodhani litamsaidia kulinda cheo chake au kupanda zaidi.

Kinachotafutwa hapo ni kuondoa sifuri kwenye wilaya au mkoa bila kujali anachopoteza mwanafunzi kwa kumuachisha baadhi ya masomo yale ya msingi.
 
Daah nilikutana na mtoto wa shule hizi nikamuuliza una ndoto ipi akaniambia I want to be a UN SECRETARY.
Nikasema hawa kweli wanawaza international level.
Hapo hata Mimi kanishinda asee
 
Umewaza kimaskini sana, hapo tulipo ndiyo tunaweza sisi kama sisi. kuna vipaji huko kwenye shule zetu hatare, tatizo la wabongo kuiga kila kitu hawaachi kupenda vya wenzeo, akibuni afisa Elimu mswahili wanaponda. akibuni mtoto wa kizungu nzuri hiyoo!

Viongozi sioni aliyesoma huko labda Dr Mwinyi lkn intern ship Muhimbili hakufanya vizuri hapo alipo usajili hana, labda apewe sasa kwa kujipendekeza, Asha Mahita amepata lkn bado mburura mweupe tu. alifanya nini cha maana TMK? siyo wote wanafanya vizuri,

Kumlea mwana changanya na Mungu akutunzie, na kukuzia uzuri, angalia sasa mzee Joseph Nyerere hakuna hata mtoto wake mmoja anayerindima katika Medani za kimataifa, hata kitaifa tu! walisoma huko!! sanasana aliyejitahidi, Cap. Makongoro lkn mlevi, Marehemu Andrew Nyerere alishindwa kuwa mbunifu kunako kazi yake ika muua.
 
Mkuu kuna world scholars kibao ambao hawajakanyaga hizo international schools na wanaheshimika kwenye field zao. Nafikiri hizo shule zimeanzishwa purposely kwa ajili ya watoto wa mabalozi kwenye nchi husika, hakuna jipya...

Si kweli. Tunaona changamoto sana kwa hawa waliosoma Kayumba na kubahatika kufika level za kimataifa kwenye kazi za kimataifa.
-
Wengine walifanikiwa kufika level hizo kwa Connection tu. Kwa mfano nafanya kazi na Mtanzania mwenzangu kwenye International Organizational nchini Nambia, huyu Mdada amepata kazi kwenye hiyo Organization kwa sababu tu Ndugu yake ni Balozi wa Namibia.
-
Imemlazimu kufanya short course kuanzia Lugha mpaka Communications Skills na nyinginezo kwa sababu yeye mwenyewe anajionea aibu.
-
Hizo International school zinawajenga watoto vizuri sana hata kwa KUFIKIRI na kujiamini na mzazi ukiwa msimamizi mzuri wa mtoto wako atafika mbali sana na atakuwa very presentable kwa fadhila za International Schools.
-
It is very serious issue sisi tulio kwenye International Organization tunaona mengi na tunaona changamoto ya Mfumo wetu wa elimu na Africa kwa Ujumla.
-
Ukiona Kayumba yupo kwenye hizi Organization na anafanya vyema ujue huyo kaji mix sana na anapenda kujifunza vitu mbalimbali au ana exposure ya maisha.
-
Kwanza sisi wabongo hata kuongea hatujui, sijui kwa nini ! Sio English wala Kiswahili, hatujui kuongea na wala hatufikirii tunachongea.
-
Ukitaka kuona hilo angalia wasanii wetu wanavyojibu maswali, angalia wachezaji mpira wakihojiwa akiwemo Samatha, zero kabisa, njoo kwenye ngazi za viongozi, zero kabisa, sio Kiswahili wala English.
-
Msanii anaejua kuongea vyema Kiswahili na English ni Sepetu na Vanesi na Kiongozi ni Mkapa na January tu.
-
Shida ipo sana eneo hili na ndio maana once it comes about International Interviews , yaani WATZD huwa ni wa mwisho na hapo unakuta mtu ana vyeti vizuri na pass Marks zake.
 
Lakini mbona kibongo talent nyingi zinatoka kwa watu ambao ni masikini na wasio na elimu kubwa
Mbona hatuoni hao international wakiongoza kwenye fani nyingi zinazotumia vipaji sana

Umetoka nje ya Mada.

Talent ni natural born thing wala hufundishwi na hakihitaji shule. Ukianza kufundishwa hiyo sio Talent bali unaweza kugundua Talent yako kupitia elimu na shule.

it is something you have never been taught. It comes out of the blue na ukiulizwa how did you know that , the honesty answer would be I don’t Know.
 
Mimi mwenyewe napenda mtoto wangu asome international school eeh mola nijalie, hizi shule zetu st kayumba mtoto GPA kubwa Ila exposure zero hata ufahamu

Okay ,na huyo Kwenye picha ni Wewe ?
 
Acha ujinga wako! Usijilinganishe na Wachina ambao hawasomi ktk Kiingereza. Kama mchina haongei Kiingereza ni sawa kwa vile anasoma ktk Kichina. Mama yako anasoma katika kiingereza sekondari mpaka anapata PhD halafu hawezi kuongea Kiingereza unamtetea nini?

Elimu mbovu. Acha kutetea ujinga wako na kujifariji. Kiingereza ni lugha kwa Mwiingereza ambaye anaweza kuongea bila kwenda shule. Mama yako huko Usukumani anaweza kuongea Kiingereza bila kwenda shule? Bichwa limetuna kwenye utosi kama Jiwe na mdomo umeanzia kwenye sikio na kuishia kwenye sikio lingine kama mkurugenzi wa NEC.
Lione hili nalo bichwa kama Lisu.

Kujieleza kwa kiingereza siyo kigezo cha kuelimika .

Kiingereza ni lugha tu kama kisukuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…