Mtu unamuheshimu Kabisaaa lakini anatembea na mke wa mtu na anajua ni mke wa mtu.
Hivi unajisikiaje kuwa sehemu ya migogoro katika ndoa ya mwanaume mwenzako?,sawa inawezekana umejua kuwa ndoa ya huyo mwanamke ina tafrani, je migogoro ya ndoa ya mwingine ni ticket ya wewe kumtaka na kutengeneza mgogoro ktk ndoa yako kama unayo?.
Ok utakuta mume wa mtu lakini ana date na mke wa mtu tena kwa mahaba mazito, hivi unachukuliaje kuwa sehemu ya kuvunja moyo wa mkeo pindi atakapo tambua?.
unajisikiaje kuwa mzurumati wa amani na furaha ya ndoa yako mwenyewe?,
Ok sawa, tufanye unakosa Haki zako za msingi kutoka kwa mkeo, hivyo huna budi kutoka nje, sasa kwanini ukatembee na mke wa mtu kwani hakuna walio mali ya umma ?
Nikweli sisi wanaume tuna udhaifu lakini inawezekana kuuzuia ili tusiumize mioyo ya hawa wanawake ambao tayari ni wake zetu, tuwe walinzi wa ndoa za wengine kama vile tulindavyo zetu.
Kuna mwanamke anamume tena anajiheshimu ,lakini anamchepuko ambaye ni mume wa mtu, na ukimwambia wewe ni mke wa mtu anakwambia kwani mke wa mtu ni kitu gani?
Sawa inawezekana ndoa yako ina migogoro hivyo unaitafuta furaha nje, sasa upi ni ulazima wakuitafuta furaha kupitia mume wa mwanamke mwenzako?, au furaha nikuona ndoa yake inakuwa kama yako?
Huoni kwamba unahujumu amani na furaha ya ndoa ya mwanamke mwenzako?, sisi wanaume hatuna uwezo wakusambaza furaha na kupenda mwanamke zaidi ya mmoja ,ni mbwembwe tu, hivyo ukiona anakuoenda ujue amesha hamisha upendo kutoka familia na mke wake, hivyo kaacha maumivu Yale ambayo huyahitaji na kamuachia mwanamke mwenzake.
Unajisikiaje kuwa sababu ya kilio na maumivu kwa mwanamke mwenako??
Kama unaona ndoa yako haikupi thamani basi achana nayo ili utengeneze thamani yako nje ya ndoa, na kama ndoa inakupa thamani basi ilinde hiyo thamani.
TUJISAHIHISHE.
saa zingine kuna mistakes wanawake huzifanya kizembe sana na kuwadhalilisha wao wenyewe, waume zao na ndoa zao kwa ujumla π
nikiwa chuo kikuu nasoma, rafiki yangu moja alikua akifanya kazi ya kuuza magari, na hiyo ilimpa fursa ya kubadili magari ya kutembelea mara kwa mara ...
siku moja tukiwa pamoja barabarani, alimpigia honi binti moja mrembo sana, huku akipagi gari pembeni ya barabara ili mrembo yule apande garini. Mrembo akafika akapanda jamaa akadrive mpaka kazini kwa mrembo akamdrop nasi tukaendelea na mishe zetu.....
Bas,
Jamaa akaanza kunipa stori za yule mrembo sasa. Kumbe alikua ni mwalimu, ameolewa, ni mzazi, ana mume na watoto wa3, na pale tulipomkuta alikua akielekea kituo cha daladala ili apande kidala kuelekea kazini kwake....
Jamaa anasema wamezoena na kujuana humo humo barabarani tu. Anasema siku moja akamtongoza yule mrembo, lakini mrembo akagoma na kumtolea nje jamaa katu katu, kwa sababu kwamba anampenda na anamuheshimu sana mumewe na hawez kumsaliti hata sku moja. Lakini pia eti mumewe ni mkali mno, hata akiskia tu uvumi wa kutoka nje ya ndoa, itakua ni shida.
Mrembo akaendelea kumsanua rafiki yangu kwamba, pia, anawatoto analea na mumewe anamtimizia haja na kila kitu anacho hitaji π
Bas,
Jamaa akaendelea kunipigia stori, kwamba siku moja akamuomba mrembo walau watoke pamoja, waende walau kupata lanchi au kinywaji pamoja, na wazungumze vizur, na maana jamaa alimueleza mrembo kwamba, hakua anaelewa alivyokua anakataliwa kwasababu concentration yake ilikua zaidi kwenye kuendesha gari na hivyo hakuelewa sababu zaidi za kukataliwa penzi na mrembo Mwalimu.
Bas ,
Mrembo, Mwalimu na mke wa mtu akakubali ile offer, kwa sharti kwamba hawatafanya chochote wala kuelekea mahala pengine popote baada ya kula au kunywa.....
Basi,
siku ikafika. Jamaa anasema, mrembo si alisema mume wake ni mkali na ni mtu hatari sana? sasa nataka nimuonyeshe kwamba sisi ndio wakali wa hizi kazi π
muda ukafika,
akampitia mahali walipokubaliana kukutana, akasimamisha gari, mrembo akazama kwenye vogue, jamaa akadrive taratibu tu, mara waingie kona hii mara ile, mtaa waingie mtaa huu, mara ule, mara waingie barabara ya lami mara ya vumbi, hadi mrembo akaanza kujawa hofu, akawa anamuuliza jamaa tunaenda wapi sasa huku hata hapajui?π³
Jamaa akamwambia tulia best tumeshafika. Mara anaona vogue linaelekea direct hadi kwenye mlango wa geti la lodge, jamaa anapiga honi, geti linafunguliwa, vogue vogue linazama kwenye coumpaund ya lodge na linapaki ndani.
Jamaa anashuka, anaingia reception, anamaliza registration, anatoka nje anampungia mkono mrembo kwenye gari ashuke aje ndani na kwamba ndio tayari wamefika kwenye launch π€£
mrembo mrembo kukataa kushuka kwenye vogue hawezi, kugoma kushuka hawezi, kupiga kelele hawezi maana ni mtu mzima π
bilashaka,
alijiuliza maswali hamsini kidogo kichwani mwake bila kupata majibu......
Eneo hilo mrembo hapajui,
na hapo ni lodge saa5 asubuhi anatakiwa awe kazini na mumeo anajua yupo kazini, na hata akipiga kelele akasaidiwa, mume wake akijua atamuuliza ilikuaje uende mpaka lodge ndio uanze kupiga kelele ?
apige kelele watu wachukue video wasambaze mitandaoni, dunia ijue kwamba alileta fujo lodge, lakini pia ndoa yake ivunjike, au akubali kuzama lodge kwa upole, amani na bila matata amalizane na jamaa mambo yaishe kwa amani ili kunusuru kuvunjika kwa ndoa yangu anayoipenda sana?
kwa hakika,
mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe π
ladies and gentlemen,
You know what happened then,
nikipata muda nitakuja kumalizia, but lift sio nzuri π