Mtu wa namna hii aachwe kuwa kiongozi kwakuwa alipata kura nyingi?

Kuna Siku nimekaa nikatafakari, Et Akina Nape, January ,Mwigulu , ndio ambao watatuchagulia Rais kupitia CCM?. .......

Bwana DOLA, embu tuweni serious kidogo basi Kuna Sheria na Kanuni ni LAZIMA VIVUNJWE KWA MSILAHI MAPANA YA NCHI "
Shida inaanzia kwako kw akujidanganya kwamba Bwana Dola yeye si miongoni mwa hao hao.

Hapo tayari umekosa relavance ya hoja yako.
 
Makosa ya ccm na mifumo yake unayoita wewe dola unataka kusingizia wapinzani?

Wewe naye ni wale wale tu unapigania tumbo tu😆😆
 
Mbona hii Rais Hayati Magifuli alifanya akaja na wale wale tena wabaya zaidi.
Kinachokuuma wewe ni kwamba watu wako hawamo na wale waliomo huna uhakika kama watarudi lakini kimantiki huna hoja mpya zaidi ya Ule uccm wa siku zote.
 

Kama kweli unapenda nchi basi pigania katiba mpya yenye demokrasia na sio kuongelea personality za watu na mafumbo yasiyo na maana. Unaongea vitu ambavyo havipo mambo ya mashoga badala ya kuongelea vitu vya maana ambavyo vinaweza kuleta mabadiliko ya kweli kama katiba ya nchi. Bila kubadilisha katiba mtaishia
Kuongelea watu badala ya mifumo kila siku. Watu wanakuja na kuondoka lakini mifumo ndiyo tatizo. Mfano mkataba wa bandari wa miaka 25 walio sign wanaondoka miaka 5 na mkataba ni wa siri sasa ukimleta Raisi mwingine atarekebisha vipi haya? Hivyo sheria ndiyo muhimu sio kutafuta watu wa kanda fulani , kabila fulani au unafikiri akija dikteta ndiyo shida zimeisha je akifa na kumwachia dikteta mbaya!

Magufuli ubaya wake mmoja tu hakujenga taasisi badala yake aliongoza nchi kama yeye ni Mungu tatizo yeye hakuwa Mungu.
 
Hii ndio comment bora kuliko hata Uzi wenyewe.

Hawa wengi wana ccm wanalalamika wakishaona mtu wao au watu wao hawamo.

Lakini akili zao ni zile zile.

Yaani hapa anapiga chapuo kwenye personality za mtu badala ya Mfumo.

Asichojua anatoa mfano wa China na CCM yake.

China na ccm are far apart 10000miles.

Ni Bunduki na Asali havifanani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…