Mtu yoyote aliyewahi kuishi na mwanamke/mwanaume na kuunda familia Hawezi kuwekwa katika Kundi la Kataa Ndoa

Andiko bora kabsa... Kujifanya kukataa ndoa ni uhuni na uoga wa majukumu ni ujinga ni uzembe ni kutotimiza wajibu....

Kazia hapo hapo
 
Neno NDOA lina maana nyingi kotokana na angle ambayo umeingalia hiyo ndoa yenyewe.

Tukisema tuweke quiz ya definition ya ndoa.

Majibu yatakuwa ni mengi sana.

Kwa maana uliyoitoa mwanzoni kabisa mwa andiko lako,sipingani na wewe katika kile unachokidai.

Shida ipo kwenye NDOA ambayo tafsiri yake ni maisha waishio wapendanao wawili baada ya kupewa baraka za kidini na kifamilia waishi pamoja.

NDOA HIZO ZIMEJAA UTAPELI SANA.
 

Kwenye maana ya msingi tunaangalia independent Factor.

Dini na Wazazi wanaweza wasiwepo ila wewe ukaoa bila shida yoyote.
Ndoa ni Watu Wawili.
Unapozungumzia baraka hapo Unazungumzia Imani.
 
kukataa ndoa ni kuonyesha uoga na ni kukataa uanaume na kukwepu wajibu
njoo tukupe mbinu za kiume za kusimamia ndoa
Sina haja hiyo kwa sababu nimekamilika kiasi kwamba naweza kuishi msituni miaka 100.

Nina watoto.
Ninauwezo wa kumpata mwanamke yoyote kwa wakati wowote.

NDOA YA NINI KAMA KUNA USALITI
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUCHEPUKA
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUUANA.
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUDHALILISHANA.

NDOA HALISI NA AMBAYO NINGEWEZA KUIINGIA KWAYO NI NDOA ZA WAZEE WETU.
NDOA ZILIZOJAA UPENDO,KUHESHIMIANA,KULINDANA,UADILIFU NA MENGINE MENGI.
 
Kwenye maana ya msingi tunaangalia independent Factor.

Dini na Wazazi wanaweza wasiwepo ila wewe ukaoa bila shida yoyote.
Ndoa ni Watu Wawili.
Unapozungumzia baraka hapo Unazungumzia Imani.
Kama umeamua kuishi na mwanamke au mwanaume mmoja kwa kigezo cha ndoa.
Kwanini usitulie na huyo ambaye umeingia naye kwenye hayo makubaliano ya kuishi naye kama mke/mume.

Kuna maana gani ya ndoa ikiwa unamuacha mke/mume ndani na kuchepuka nje ukimsaliti mwenza wako.

Kuna maana gani ya ndoa ikiwa unakula njama za kumfifiza au kumuangamiza mwenza wako sababu ya tamaa za mali.

Nini maana ya ndoa?
 

Upendo hauji kirahisi
Heshima, uadilifu na mengine mengi hayaji kirahisi.
Inahitaji kupiganiwa, kulindwa kwa nguvu na mwanaume au mwanamke shupavu.

Sasa kama unaoa alafu unataka mambo yaje na yaende kirahisi utakwama
 

Sasa wewe unazungumzia kitu kingine ambacho ni usaliti.

Sio kila ndoa inausaliti.
Na sio kila ndoa inakufifizwa
 
Upendo hauji kirahisi
Heshima, uadilifu na mengine mengi hayaji kirahisi.
Inahitaji kupiganiwa, kulindwa kwa nguvu na mwanaume au mwanamke shupavu.

Sasa kama unaoa alafu unataka mambo yaje na yaende kirahisi utakwama
basi ndoa haina huo umuhimu kama chanzo kikuu na msingi wake ni upendo
lakin kuupata huo upendo mpaka uupiganie HAPANA mzee
KATAA NDOA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…