Mtu yoyote aliyewahi kuishi na mwanamke/mwanaume na kuunda familia Hawezi kuwekwa katika Kundi la Kataa Ndoa

Mtu yoyote aliyewahi kuishi na mwanamke/mwanaume na kuunda familia Hawezi kuwekwa katika Kundi la Kataa Ndoa

Kwema Wakuu!

Vijana wa siku hizi wamechanganyikiwa mno. Hata vitu vidogovidogo kama maana ya maneno au dhana hawajui. Mathalani, Neno "Ndoa".

Kuishi na mwanamke au mwanaume kiunyumba kwa lengo la kuunda familia ndio tafsiri sahihi ya Ndoa. Ndoa ni makubaliano ya mwanaume na mwanamke kuishi pamoja katika kuunda familia. Hiyo ni ndoa. Nature inatambua hivyo.

Ndoa haihitaji ruhusa ya Wazazi, sijui taasisi ya dini gani huko, sijui serikali. Yaani serikali inaweza isiwepo lakini ndoa ikawepo, wazazi wanaweza wasiwepo lakini ndoa ikawepo, taasisi za dini zinaweza zisiwepo lakini Ndoa ikawepo. Hiyo tosha inatakiwa ikuonyeshe kuwa Maamuzi na makubaliano ya wawili(me na ke) ndio independent Factor. Hizo zingine ni dependent Factors.

Wengi hufikiri kuwa Ndoa ni kuchukua mwenza kumpeleka kwa wazazi, sijui kutoa mahari, sijui kwenda msikitini sijui Kanisani au serikalini ati huko ndio kufunga Ndoa. Jambo ambalo sio sahihi.

Wewe ukishaishi na Mwanamke au mwanaume pamoja, kwa lengo la kushiriki kuunda familia na kampani katika maisha hiyo tayari ni NDOA.
Haupo kwenye kundi la watu wanaokataa Ndoa.

Sheria za ndoa, mila na taratibu za kiutamaduni zilizowekwa kwenye ndoa zipo kwaajili ya kuzuia Uonevu, dhulma na uminywaji wa haki miongoni mwa wanandoa ambao tayari wamekwisha kuoana hata bila kuhusisha wazazi, taasisi za Dini, na serikali.

Wazazi, Taasisi za dini na serikali hazina haki ya kuingilia mambo ya familia yako isipokuwa tuu ikiwa kuna uhalifu, dhulma inafanyika.
Kisiasa na kiutawala Ndoa ni smallest Unit ya Mamlaka na Utawala. Ni kama Seli ya mwili kwa kiumbe hai.

Kuipinga Ndoa kwa viumbe wenye utashi haitawezekana kwa sababu itatafsiriwa kama Kupinga Mamlaka za kisiasa za juu kama Serikali.

Huwezi ongoza taifa ambalo robo tatu ya Watu ni wakataa Ndoa. Hiyo haiwezekaniki. Ni kama kuongoza taifa la mashetani ambalo mara kwa mara mapinduzi, tamaa mbaya, uchafu utakuwa ndio mila na desturi.

Ndoa ni familia, familia ndio msingi mkuu wa taifa na Dunia.

Wapinga ndoa wanahaki ikiwa watakuwa ni éxceptional na wachache. Lakini kupiga kampeni Watu wakatae Ndoa ni sawa na kupiga kampeni Duniani kusiwe na serikali yaani Watu waishi vyovyote watakavyo. Yaani Tanzania serikali ifutwe, Kenya na Dunia nzima kusiwe na serikali. Unafikiri nini kitatokea?

Moja ya mambo yanayowatofautisha binadamu na wanyama wengine ni pamoja na Ndoa.

Kama mwanadamu akipinga ndoa atazidi kufanana na wanyama wengine kama Mbwa, Paka, na wanyama wengine wasio na mfumo wa kifamilia. Na hii itafanya mwanadamu asitawalike na tabia zingine chafu na mbaya zitazidi kuibuka.

Unazaa watoto kama Mbwa alafu hujui wanaishije, wanalelewaje, lakini ndani ya ndoa lazima ujue wanaishije na wanalelewaje kwa sababu nawe utakuwa mhusika wa kujenga kizazi chako.

Kutuma pesa sio Malezi. Huwezi sema umemlea mtoto kisa ulikuwa unatuma pesa. Malezi yanahusu ushiriki wa moja kwa moja kwa mzazi kwa mtoto wake.

Mtoto akikaa kwa Bibi au kwa Mamaake au kwa Babaake alafu wewe ukawa unatuma pesa za matumizi. Haiwezi kutajwa kuwa Mtoto huyo Ulimlea.
Kuishi na mtoto ndio kumlea mtoto na hakuna tafsiri zaidi ya hiyo.
Kutuma matumizi ya mtoto haiwezi kutafsiriwa kama kufanya malezi.

Vijana, kampeni ya Kukataa ndoa haiwezi kuwa kwa mtu mwenye utimamu wa Akili. Ni aidha kuna athari za kisaikolojia au Historia mbaya kwa mtu husika.

Utapeli kwenye mapenzi upo.
Ubinafsi kwenye mapenzi na ndoa upo.
Unyanyasaji na ukatili kwenye ndoa unaweza kuwepo.
Lakini nani mwenye wajibu wa kupambana kukabiliana na mambo hayo kama sio wewe?

Jukumu lako kama mwanaume au mwanamke ni kusimamisha serikali yako(familia yako). Jukumu lako kama mwanadamu ni kutawala. Utawala unaanzia kwenye kizazi chako kisha mazingira na jamii.

Yaani upo serikalini ati unakataa serikali kisa ati kuna Waasi, sijui magaidi, sijui Watu wanaotaka kukupindua, sijui wala rushwa na wanaokuhujumu. Wewe utakuwa na akili kweli.

Kama mtawala(mfano wa Mungu) ni jukumu lako kupambana na kuhakikisha kizazi chako kinakuwa bora na kizazi bora hutoka kwenye familia BORA (mke na mume) na sio nje ya hapo.

Muhimu, unapaswa uwe makini katika kuchagua mwenza wa maisha ambaye utaenda kuanzisha nayè familia(serikali yenu).

Dhamiri ya kile kinachokufanya uchague mke au mume na vigezo ulivyoviweka ndio vitaamua serikali yako(familià yako) itakavyokuwa.

Ndoa na mapenzi sio Pesa. Hilo liweke Akili kabisa. Ukishaingiza mtazamo kuwa ndoa au mahusiano ni pesa jua kabisa wewe ni Tapeli na mbinafsi kabla hata ya huyo mwenza unayemtafuta.
Kwenye utawala au mamlaka pesa hutafutwa. Lakini uaminifu, upendo, haki uadilifu, umoja, kujitoa ndio misingi ya Utawala ikiwemo familia.

Acha Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Andiko bora kabsa... Kujifanya kukataa ndoa ni uhuni na uoga wa majukumu ni ujinga ni uzembe ni kutotimiza wajibu....

Kazia hapo hapo
 
Huwezi kukataa ndoa
Kataa utapeli kwenye ndoa. Au kataa hfulma kwenye Ndoa. Hiyo imekaa sawa.

Alafu kingine utapeli katika ndoa huanzia katika hatua za awali kabisa.
Kitendo cha kusema kuna mmoja anatakiwa sijui kumpenda mwingine zaidi na mwingine kumtii mwingine zaidi huo ndio utapeli wenyewé.

Kanuni ya ndoa(upendo) ni kile ambacho hutaki kufanyiwa usimfanyie mwenzako. Na kile ambacho unapenda ufanyiwe basi mfanyie mwenzako.
Neno NDOA lina maana nyingi kotokana na angle ambayo umeingalia hiyo ndoa yenyewe.

Tukisema tuweke quiz ya definition ya ndoa.

Majibu yatakuwa ni mengi sana.

Kwa maana uliyoitoa mwanzoni kabisa mwa andiko lako,sipingani na wewe katika kile unachokidai.

Shida ipo kwenye NDOA ambayo tafsiri yake ni maisha waishio wapendanao wawili baada ya kupewa baraka za kidini na kifamilia waishi pamoja.

NDOA HIZO ZIMEJAA UTAPELI SANA.
 
Kwenye maana ya msingi tunaangalia independent Factor.

Dini na Wazazi wanaweza wasiwepo ila wewe ukaoa bila shida yoyote.
Ndoa ni Watu Wawili.
Unapozungumzia baraka hapo Unazungumzia Imani.
 
kukataa ndoa ni kuonyesha uoga na ni kukataa uanaume na kukwepu wajibu
njoo tukupe mbinu za kiume za kusimamia ndoa
Sina haja hiyo kwa sababu nimekamilika kiasi kwamba naweza kuishi msituni miaka 100.

Nina watoto.
Ninauwezo wa kumpata mwanamke yoyote kwa wakati wowote.

NDOA YA NINI KAMA KUNA USALITI
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUCHEPUKA
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUUANA.
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUDHALILISHANA.

NDOA HALISI NA AMBAYO NINGEWEZA KUIINGIA KWAYO NI NDOA ZA WAZEE WETU.
NDOA ZILIZOJAA UPENDO,KUHESHIMIANA,KULINDANA,UADILIFU NA MENGINE MENGI.
 
Kwenye maana ya msingi tunaangalia independent Factor.

Dini na Wazazi wanaweza wasiwepo ila wewe ukaoa bila shida yoyote.
Ndoa ni Watu Wawili.
Unapozungumzia baraka hapo Unazungumzia Imani.
Kama umeamua kuishi na mwanamke au mwanaume mmoja kwa kigezo cha ndoa.
Kwanini usitulie na huyo ambaye umeingia naye kwenye hayo makubaliano ya kuishi naye kama mke/mume.

Kuna maana gani ya ndoa ikiwa unamuacha mke/mume ndani na kuchepuka nje ukimsaliti mwenza wako.

Kuna maana gani ya ndoa ikiwa unakula njama za kumfifiza au kumuangamiza mwenza wako sababu ya tamaa za mali.

Nini maana ya ndoa?
 
Sina haja hiyo kwa sababu nimekamilika kiasi kwamba naweza kuishi msituni miaka 100.

Nina watoto.
Ninauwezo wa kumpata mwanamke yoyote kwa wakati wowote.

NDOA YA NINI KAMA KUNA USALITI
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUCHEPUKA
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUUANA.
NDOA YA NINI KAMA KUNA KUDHALILISHANA.

NDOA HALISI NA AMBAYO NINGEWEZA KUIINGIA KWAYO NI NDOA ZA WAZEE WETU.
NDOA ZILIZOJAA UPENDO,KUHESHIMIANA,KULINDANA,UADILIFU NA MENGINE MENGI.

Upendo hauji kirahisi
Heshima, uadilifu na mengine mengi hayaji kirahisi.
Inahitaji kupiganiwa, kulindwa kwa nguvu na mwanaume au mwanamke shupavu.

Sasa kama unaoa alafu unataka mambo yaje na yaende kirahisi utakwama
 
Kama umeamua kuishi na mwanamke au mwanaume mmoja kwa kigezo cha ndoa.
Kwanini usitulie na huyo ambaye umeingia naye kwenye hayo makubaliano ya kuishi naye kama mke/mume.

Kuna maana gani ya ndoa ikiwa unamuacha mke/mume ndani na kuchepuka nje ukimsaliti mwenza wako.

Kuna maana gani ya ndoa ikiwa unakula njama za kumfifiza au kumuangamiza mwenza wako sababu ya tamaa za mali.

Nini maana ya ndoa?

Sasa wewe unazungumzia kitu kingine ambacho ni usaliti.

Sio kila ndoa inausaliti.
Na sio kila ndoa inakufifizwa
 
Upendo hauji kirahisi
Heshima, uadilifu na mengine mengi hayaji kirahisi.
Inahitaji kupiganiwa, kulindwa kwa nguvu na mwanaume au mwanamke shupavu.

Sasa kama unaoa alafu unataka mambo yaje na yaende kirahisi utakwama
basi ndoa haina huo umuhimu kama chanzo kikuu na msingi wake ni upendo
lakin kuupata huo upendo mpaka uupiganie HAPANA mzee
KATAA NDOA
 
Back
Top Bottom