Ni wanandoa wangapi wamezijenga ndoa zao tangia chini huku wakitumia rasilimali kama upendo,heshima,uadilifu,ukweli na mengineyo na kuzifanya zikawa imara.
By default baada ya wawili kukutana na kuendana.
Bond yao humaanisha mengi sana
Ndoa za sasa zimekuwa ni utapeli kwa sababu kila mmoja katika ndoa anatamani kuwa juu ya mwenzake.
Mwanaume anataka kuwa juu.
Mwanamke anataka kuwa juu vilevile.
Mwanaume ana sauti ndani ya familia vs mwanamke ana sauti ndani ya familia.
Unauonaje mtanange huu?
Unadhani utaisha kwa salama na amani.
Tukiacha yote bora huyo mwanaumwe awe na nguvu ya kipesa kuliko mwanamke.
Kinyume cha hapo ndiyo sababu ya watu wengi leo hii kuzikataa ndoa za kisasa.