Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Katika ulivyo vitaja hapo nikipi kinacho kutesa?
Habari kwamba watoto wadogo wanakatishwa maisha yao hata kabla hayajaanza vizuri, mama zao wanasikitika sana kwa kutenganishwa na watoto hawa, inanitesa.

Huyu Mungu imekuwaje akaumba ulimwengu ambao watoto wadogo wanakufa, wengine kikatili sana, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna kifo, na watu wanaopendana hawatenganishwi kwa kifo?

Hujajibu swali hili.
 
Mkuu mimi ni mtu ninayejadili mambo kwa Logical Consistency.Leo niko na hoja ya Jua kuzama katika matope.Hili la kwako juu ya kwamba hakuna Omniscience,Omnipresence, Omnipotence, God with all Loving and with devine Mercy, nitayaletea uzi wake, siku yake pekee.Kwa hiyo usifikirie hizo hoja zako hazina hazina majibu.
Maswali yote yanahusu Mungu na logical consistency.

Utamshambuliaje Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency (kitu ambacho hata mimi nakiona) halafu hapo hapo nikikwambia hata Mungu wa Biblia naye hana logical consistency hivyo Quran na Biblia vyote vina ujinga ule ule wa Mungu asiye na logical consistency ukakimbia swali kuhusu logical consistency hiyo hiyo ya kumhusu Mungu?

Hapa unaonekana unapenda kumshambulia Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency, lakini, ukiulizwa habari hizo hizo za logical consistency kuhusu Mungu wa Biblia, unakimbia kujibu maswali.
 
Sasa unapomkataza mtoto asiangalie tv usiku si lazima uihamishe kutoka sebuleni uifiche chumbani,utategemea mtoto mwenyewe atafuata maelekezo yako ya kutoangalia tv muda huo uliomkataza,sasa utakapotoka ghafla usiku kwenda sebuleni ukamkuta amekaidi amri uliyompa ukamuadhibu hatakuuliza kwanini umenikataza halafu TV umeiacha mpaka nkashawishika kuingalia ilhali umenkataza,hivyo ndivyo navyoilewa falsa ya dhambi,kwamba kwanini kitimoto kimekatazwa,alafu nguruwe wapo,au kwanini umekatazwa usile mke wa mtu alafu mwenzio alafu huyi mke akawa mzuri na anayetamanisha balaa.

unadhani kuna logic gani ya kuwepo magonjwa alafu kukawa na dawa na mitishamba yanayotibu magonjwa hayo,logical consistency iko wapi hapo.iweje napata mafua,alafu nkinywa tangawizi na asali au salimia,kinapona.hii system imetokea wapi?
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao dhambi haipo kabisa na haiwezekani kufanyika?
 
Mleta mada inaonyesha una kichwa kigumu kama nazi ya kilwa. Sasa hapo haujaelewa nini kwamba Dhul-Qarnain aliliona jua likizama kwenye tope kwa upeo wa macho yake?

Ni sawa ni Dhul-Qarnaini aliliona Jua likizama kwa kadri ya upeo wake.Swali ni kwamba Mungu alikuwa akimuelezea Muhammad kisa hicho cha Dhul-Qarnaini ili kumfundisha nini hasa na wewe muislamu wa leo unajifunza nini hasa kutokana na hicho kisa cha Dhul-Qarnaini?
 
Wanajukwa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.

Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?

2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?

3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?

· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?

· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
Umeelezea mengi sana lakini Kwanza tujue je sayansi inatambua uwepo wa Mungu? Ukinipa jibu basi naweza kuendelea na mada yako.
 
Kwa hiyo, ina maana hata ile nakala ya Mungu kule Mbinguni, nayo bado ina hilo fundisho kwamba Jua linachwea kwenye matope meusi licha ya kwamba Sayansi imeshathibitisha kwamba sio kweli hicho Kurani inachokiongelea? Ikiwa bado nakala ya Mungu inayo hiyo aya hiyo, Mungu anajisikiaje, kwa sababu sasa ni kama ameumbuka na wanadamu wataanza ku-doubt?
Qur'an ina nakala mbinguni?
 
Maswali yote yanahusu Mungu na logical consistency.

Utamshambuliaje Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency (kitu ambacho hata mimi nakiona0 halafu hapo hapo nikikwambia hata Mungu wa Biblia naye hana logical consistency hivyo Quran na Biblia vyote vina ujinga ule ule wa Mungu asiye na logical consistency ukakimbia swali kuhusu logical consistency hiyo hiyo ya kumhusu Mungu?

Hapa unaonekana unapenda kumshambulia Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency, lakini, ukiulizwa habari hizo hizo za logical consistency kuhusu Mungu wa Biblia, unakimbia kujibu maswali.

Mimi kama umenifuatilia muda wote nimekataa kuingia katika derailing.Huwezi kunitoa katika hoja ya msingi kwa kutaka kunichomekea hoja zingine? Na ndio maana kuna vitu vingi tu vimeingizwa katika mjadala huu ambavyo havihusiki na nimekwepa au nimeacha kushughulika navyo.Kwani hoja kwamba Mungu hayupo ni mfano katika hoja iliiyopo mezani au unajaribu kupenyeza hoja mpya kabisa katikati ya mjadala?>
 
Ni sawa ni Dhul-Qarnaini aliliona Jua likizama kwa kadri ya upeo wake.Swali ni kwamba Mungu alikuwa akimuelezea Muhammad kisa hicho cha Dhul-Qarnaini ili kumfundisha nini hasa na wewe muislamu wa leo unajifunza nini hasa kutokana na hicho kisa cha Dhul-Qarnaini?
Endelea mbele ya aya zinazofuatia utaona kisa cha Dhul-Qarnaini kinafundisha nini. Pia, kama bado utakuwa ujaelewa, tafuta hats video za youtube maelezo ya mafundisho ya Surah Kahf kiujumla utaelewa zaidi.
 
Nikafungue video Youtube? Hiyo video nayo Mungu ametia ufunuo wake kama ilivyo katika Kurani? Mimi naamini Kurani, kwa sababu hicho Kitabu alichokipokea Muhammad na siyo Youtube Application software.Youtube imekuja juzi juzi tu hapa na imefanyikia katika Computer na asili yake ni Coding na wala haikutengenezewa katika pango la Mlima Hira,kule Makka kama ilivyo kwa Kurani.
 
Sasa unapomkataza mtoto asiangalie tv usiku si lazima uihamishe kutoka sebuleni uifiche chumbani,utategemea mtoto mwenyewe atafuata maelekezo yako ya kutoangalia tv muda huo uliomkataza,sasa utakapotoka ghafla usiku kwenda sebuleni ukamkuta amekaidi amri uliyompa ukamuadhibu hatakuuliza kwanini umenikataza halafu TV umeiacha mpaka nkashawishika kuingalia ilhali umenkataza,hivyo ndivyo navyoilewa falsa ya dhambi,kwamba kwanini kitimoto kimekatazwa,alafu nguruwe wapo,au kwanini umekatazwa usile mke wa mtu alafu mwenzio alafu huyi mke akawa mzuri na anayetamanisha balaa.

unadhani kuna logic gani ya kuwepo magonjwa alafu kukawa na dawa na mitishamba yanayotibu magonjwa hayo,logical consistency iko wapi hapo.iweje napata mafua,alafu nkinywa tangawizi na asali au salimia,kinapona.hii system imetokea wapi?
Kwa nini Mungu wako ajitekenye na kucheka mwenyewe?

Kwa nini awezeshe ugonjwa uwepo na dawa badala ya kukataza ugonjwa usiwezekane kabisa?

Na vipi kuhusu magonjwa ambayo hayana dawa?
 
Qur'an ina nakala mbinguni?

Kwani wewe hujui kama Mungu ana nakala yake Mbinguni? Wewe hujui kuwa Mungu alianza kuandika Kurani Mbinguni na ndio kisha akampa Muhammad kupitia Malaika Gabrieli ili awe anakili hayo ambayo Mungu alishaaandika? Sasa katika mazingira kama hayo inakosekanaje nakala ya Mungu?
 
Wanajukwa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.

Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?

2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?

3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?

· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?

· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.

GONGA HAPO CHINI

Did the Noble Quran really say that the sun sets and rises on earth?
 
Huyu Mungu imekuwaje akaumba ulimwengu ambao watoto wadogo wanakufa, wengine kikatili sana, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna kifo, na watu wanaopendana hawatenganishwi kwa kifo?
Nani anaewaua kikatili hivyo? Je wakifa wanaenda wapi?
 
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao dhambi haipo kabisa na haiwezekani kufanyika?
Hakushindwa kama aliweza kuumba wa dizaini hii tulionao na complixity/sophistication zake,sasa kwanini kauumba wa dizaini hii Uislamu ndio unakupa jibu wewe mdadisi kuwa kaumba mfumo ukiwa hivi ili awajaribu nyinyi aliewaumba kama mutafuata haki na kutenda wema ama mutakengeuka na kufanya mabaya,then wote mtakufa na kufufuka tena kwakuwa roho ambayo ni energy huwa haifi kwa mujibu wa wanasayansi bali hubadilika au kuhama kutoka kwenye medium moja kwenda nyengine,kwahyo ili kumake sense ya haya yanayoendelea lazima uamini kwanza kuwa kuna kufufuliwa ambapo wema watakuwa rewarded na wabaya wataadhibiwa na kisha wale waliodhulumiwa watalipwa kile walichozulumiwa.
Na ukiniambia huamini kuwa kutakuwa na kufufuliwa nitakujibu kuwa kama ardhi inaweza kuwekwa mbegu ikatoa mti wenye matundo na huoni ajabu kwanini uone ajabu binaadamu kufa,then akafufuka tena.

Kuhusu kwanini watoto wadogo wanakufa bila hatia na watu kuumwa nakuteseka duniani nitakueleza kuwa dunia na mfumo wake mzima ni challenge/mtihani ndio maana hata kutokea kwake kulianza na big bang.ndo maaana ukiwa siberia ama sehemu nyengine yoyote yenye sub zero temperature usipovaa mavazi ya kuzuia baridi utakufa kwa baridi na ukivaa hutakufa kwa baridi,ndio maana hata porini wanyama wanawindwa haijalishi kama aliyewindwa alikuwa mkorofi au la.ndio maaana hata ukilima kuna baadhi ya mazao yatamea na mengine yatakufa.Mungu kaicha dunia ijiendeshe kwa mfumo huo.
 
Mimi kama umenifuatilia muda wote nimekataa kuingia katika derailing.Huwezi kunitoa katika hoja ya msingi kwa kutaka kunichomekea hoja zingine? Na ndio maana kuna vitu vingi tu vimeingizwa katika mjadala huu ambavyo havihusiki na nimekwepa au nimeacha kushughulika navyo.Kwani hoja kwamba Mungu hayupo ni mfano katika hoja iliiyopo mezani au unajaribu kupenyeza hoja mpya kabisa katikati ya mjadala?>
Hija ya msingi unaikwepa halafu unasema nataka kukutoa katika hoja ya msingi?

Unaelewa kwamba ukishakubali kwamba unatafuta logical consistency, Mungu wa Biblia kashindwa mtihani wa logical consistency na hivyo hutakiwi kumuandama Mungu wa Quran kwa sababu hana logical consistency, halafu hapo hapo ukamkubali Mungu wa Biblia ambaye naye hana logical consistency?

Unaelewa hiyo ni contradiction?

Unakataa kula mavi ya muarabu kwa sababu unasema hutaki kula mavi.

Halafu unakula mavi ya Myahudi bila tatizo.

Halafu bado unadai hutaki habari za kula mavi?
 
Nikafungue video Youtube? Hiyo video nayo Mungu ametia ufunuo wake kama ilivyo katika Kurani? Mimi naamini Kurani, kwa sababu hicho Kitabu alichokipokea Muhammad na siyo Youtube Application software.Youtube imekuja juzi juzi tu hapa na imefanyikia katika Computer na asili yake ni Coding na wala haikutengenezewa katika pango la Mlima Hira,kule Makka kama ilivyo kwa Kurani.
Kuna walimu watakufundisha humo. Kwani humu jamiiforums imekuja yenyewe bila coding?
 
Nani anaewaua kikatili hivyo? Je wakifa wanaenda wapi?
Kokote watakakwenda au kama hakuna wanapokwenda, kumtenganisha mtoto mchanga na mama yake aliyemzaa na anayependa kuwa naye mpaka anakua mtu mzima, kama una uwezo wa kuzuia utenganishi huu, ni ukatili.

Ndiyo maana watu wanasikitika na kulia kwenye misiba.

Swali la msingi hujajibu.

Mungu alishindwa kuumba dunia hi ikiwa haina na haiwezekani kuwa na utenganishwaji huu?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom