Akili yako sio muongozo wa mungu fahamu Mungu ana mambo yake
Hili jibu linaitwa "deus ex machina".
Deus ex machina - Wikipedia
Wagiriki wa kale walikuwa wanapenda sana tamthiliya na maigizo.
Sasa wale waandishi wa tamthiliya, mara nyingine, walikuwa wanaandika tamthiliya ambazo zinajichanganya, wanashindwa kuzimaliza kimantiki.
Waingereza wanasema "they paint themselves into a corner".
Maana yake, unatoa maelezo ambayo unakuta hayawezi kuwa reconciled kimantiki. Inabidi upate namna ya kumaliza tamthiliya.
Sasa waandishi wakawa wanatumia habari moja kumaliza hadithi ambayo haielezeki.
Wakawa wana limungu lao la uongo linashushwa na mashine, linamaliza kila kitu.
Ukishindwa kuelezea kitu, unataka kumaliza hadithi, unalishusha tu hilo limungu likaja likamaliza hadithi.
Watu wawili wanapigana na jeshi la watu elfu thelathini, huna jinsi ya kuelezea watashindaje ikaeleweka kimantiki? Unalishusha tu hilo limungu la uongo kutoka juu, linamaliza mchezo vizuri kuliko movie yoyote ya Rambo.
Mpaka leo hii, muandishi akiambiwa kamaliza hadithi kwa "deus ex machina" ni shutuma mbaya kwamba hajamaliza hadithi yake kimantiki, amelazimisha mwisho kw akumshusha Mungu wa uongo.
Hizi habari za "Mungu ana mambo yake" "Mungu hapangiwi" "Mungu anafanya kazi kwa miujiza" si majibu.
Ni kukubali kwamba huna majibu. Unalazimisha "Deus ex Machina".
Siajsema Mungu hana mambo yake, nimekuuliza unipe sababu za Mungu kufanya hivi na si vile.
Kitu ambacho umeshindwa.
Kwa sababu, huyo Mungu, hayupo.
Deus ex machina - Wikipedia