Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Picha ya kwanza na ya tano nikiwa namsimulia mtu jinsI nilivyoliona jua linazama nikamiambia nimeliona jua linazama kwenye maji nitakua namaanisha linazama kwenye maji kweli au ndivyo nilivyoona kwa muono wangu? VipI kuhusu picha ya pili Jua si naliona linazama ardhini? Na picha ya tatu utamuelezeaje mtu kwamba unaliona jua linazama vipi? Nikisema nyuma ya mlima nitakosea? Picha ya nne nikisema jua limezama kwenye mawingu meusi je?

Nadhani hata huyo anaesimuliwa katika Qur an anasema aliliona jua linazama katika matope meusi kwa muono kama huo hapo juu.View attachment 814741View attachment 814742View attachment 814743View attachment 814744View attachment 814745
THIS IS VIVID EXAMPLE
 
inawezakana ikawa sio yeye anayehitaji kitabu kuelezewa bali sisi ndio tunavihitaji kumuelewa,kama tunavyohitaji vitabu kuelewa elimu nyengine kama biolojia fizikia etc.
Mungu huyo angekuwepo, asingetupa gharama isiyo na lazima ya kuhitaji kitabu kumuelewa.

Angetuumba ubongo tayari umesha download habari zote za kitabu kumuelewa.

Ukiona unaambiwa kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote, halafu habari zake zimeandikwa katika kitabu, jua huyo aliyeandikwa kwenye kitabu si huyo Mungu anayesemwa.

Kwa sababu Mungu mjuzi hivyo, mwenye uwezo hivyo na upendo hivyo angetupa yote yaliyo katika kitabu katika vichwa vyetu tusingehitaji kuhangaika kujifunza lugha nyingine, kutafsiri, kubishana kuhusu tafsiri na uhjinga mwingine mwingi.

Kwa nini atupe kazi ya ziada viumbe wake anaotupenda wakati ana uwezo wa kurahisisha mambo hayo kwa kutupa kila kitu kichwani?
 
Hili jibu linaitwa "deus ex machina".

Deus ex machina - Wikipedia

Wagiriki wa kale walikuwa wanapenda sana tamthiliya na maigizo.

Sasa wale waandishi wa tamthiliya, mara nyingine, walikuwa wanaandika tamthiliya ambazo zinajichanganya, wanashindwa kuzimaliza kimantiki.

Waingereza wanasema "they paint themselves into a corner".

Maana yake, unatoa maelezo ambayo unakuta hayawezi kuwa reconciled kimantiki. Inabidi upate namna ya kumaliza tamthiliya.

Sasa waandishi wakawa wanatumia habari moja kumaliza hadithi ambayo haielezeki.

Wakawa wana limungu lao la uongo linashushwa na mashine, linamaliza kila kitu.

Ukishindwa kuelezea kitu, unataka kumaliza hadithi, unalishusha tu hilo limungu likaja likamaliza hadithi.

Watu wawili wanapigana na jeshi la watu elfu thelathini, huna jinsi ya kuelezea watashindaje ikaeleweka kimantiki? Unalishusha tu hilo limungu la uongo kutoka juu, linamaliza mchezo vizuri kuliko movie yoyote ya Rambo.

Mpaka leo hii, muandishi akiambiwa kamaliza hadithi kwa "deus ex machina" ni shutuma mbaya kwamba hajamaliza hadithi yake kimantiki, amelazimisha mwisho kw akumshusha Mungu wa uongo.

Hizi habari za "Mungu ana mambo yake" "Mungu hapangiwi" "Mungu anafanya kazi kwa miujiza" si majibu.

Ni kukubali kwamba huna majibu. Unalazimisha "Deus ex Machina".

Siajsema Mungu hana mambo yake, nimekuuliza unipe sababu za Mungu kufanya hivi na si vile.

Kitu ambacho umeshindwa.

Kwa sababu, huyo Mungu, hayupo.

Deus ex machina - Wikipedia
Unaamin hizo story za wagiriki wa kale?
 
Hilo fundisho linaitwa Predestination.Linafundishwa hivyo na Kurani,Ellen White (Sabato) na waprotestanti wengineo.Jambo la kushangaza hawasemi hao ambao destination yao iko coded ni akina nani na kama kweli mambo yako hivyo ni kwa nini bado wanahubiria watu makasani waokoke maana kama kuna watu tayari wameandikiwa fungu la kukosa au la kupata ni kupoteza nguvu tu maana kunakuwa hakuna cha kubadilika.
Dini yoyote inayofundisha Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uuwezo wote na kaumba kila kitu mwanzo inafundisha predestination.

Hii inajumlisha Ukristo wote, si hayo madhehebu uliyoyataja tu.
 
Hahaha naona wewe ndio ushapata mlango wa kutokea kwa kutafuta kuhamisha mjadala , si umeona sasa nilikusihi kwenye paragraph ya mwisho na hukunielewa.. hahaha eti ili Muhammad apate picha gani, kumbe hata hujui hiyo habari ya Dhil Qarnain ilianzaje mpaka ikafikia hapo, eti 300 BC ndo umeona ajabu, na ya manabii wengine yaliyozungumzwa kwenye Qur'an kina Adam, Noah, Idriss, Daud, Solomon, Ibrahim, Musa mbona hujajiuliza ilikuwa B.C ngapi ? Yaani hapo ndo umedhihirisha uko mtupu kwenye masuala haya... Mkuu bora utafute mada nyingine ya kujadili, hii itakuwa too big for you my dear bro..
Wengine huwa ni mashabiki tu. Maada ikishawekwa hata kama haijui ataingangania ndio maana hawezi leta mfano mwingine tofauti ili kusuport wazo lake
 
Mungu huyo angekuwepo, asingetupa gharama isiyo na lazima ya kuhitaji kitabu kumuelewa.

Angetuumba ubongo tayari umesha download habari zote za kitabu kumuelewa.

Ukiona unaambiwa kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote, halafu habari zake zimeandikwa katika kitabu, jua huyo aliyeandikwa kwenye kitabu si huyo Mungu anayesemwa.

Kwa sababu Mungu mjuzi hivyo, mwenye uwezo hivyo na upendo hivyo angetupa yote yaliyo katika kitabu katika vichwa vyetu tusingehitaji kuhangaika kujifunza lugha nyingine, kutafsiri, kubishana kuhusu tafsiri na uhjinga mwingine mwingi.

Kwa nini atupe kazi ya ziada viumbe wake anaotupenda wakati ana uwezo wa kurahisisha mambo hayo kwa kutupa kila kitu kichwani?
Unapenda mambo mteremko kiasi hiko
 
Unaamin hizo story za wagiriki wa kale?
Siamini.

Najua kwamba muandishi anayeshindwa kumaliza story logically anaweza kutumia "deus ex machina" kumaliza hadithi.

Hii hapa hadithi fupi inayotumia "deus ex machina".

Willy Janja alikuwa jasusi wa Tanzania aliyefika Pretoria kukusanya nyaraka za makaburu ili kujua mipango yao ya ulinzi dhidi ya ANC.

Tatizo, nyaraka zilikuwa zinalindwa na ulinzi mkali, katika jengo lenye kuta tatu na walinzi mia tatu.

Willy Janja akawa anakuna kichwa, ataingiaje humo ndani.

Pale pale radi kubwa ikapiga, ikavunja kuta zote tatu na kuua walinzi mia tatu, ikafungua vitasa vya jengo, ila haikuunguza nyaraka.

Wwily Janja akachukua nyaraka zote na kutokomea nazo kurudi nazo Tanzania.

Mwisho

Katika utunzi wa hadithi, hadithi hii ina mapungufu makubwa sana.

Imetumia "deus ex machina" ya radi iliyopiga, ambayo imevunja kuta tatu, imeua walinzi mia tatu, imefungua vitasa, haijamuua Willy Janja, haijaunguza nyaraka, na imempa ushindi kiubwete Willy Janja.

Hadithi hii haina "believability".

Habari ya kuwapo kwa Mungu wako ni sawa na hiyo "deus ex machina" ya Willy Janja.

Haina believability.
 
Mungu huyo angekuwepo, asingetupa gharama isiyo na lazima ya kuhitaji kitabu kumuelewa.

Angetuumba ubongo tayari umesha download habari zote za kitabu kumuelewa.

Ukiona unaambiwa kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote, halafu habari zake zimeandikwa katika kitabu, jua huyo aliyeandikwa kwenye kitabu si huyo Mungu anayesemwa.

Kwa sababu Mungu mjuzi hivyo, mwenye uwezo hivyo na upendo hivyo angetupa yote yaliyo katika kitabu katika vichwa vyetu tusingehitaji kuhangaika kujifunza lugha nyingine, kutafsiri, kubishana kuhusu tafsiri na uhjinga mwingine mwingi.

Kwa nini atupe kazi ya ziada viumbe wake anaotupenda wakati ana uwezo wa kurahisisha mambo hayo kwa kutupa kila kitu kichwani?
Sasa mkuu wewe unataka kumpangia namna gani aendeshe vile alivyoviunda na system nzima ya universe,yeye ndo kaamua iwe hivyo,hayo unayoleta ni mawazo yako ya jinsi mambo yangetakiwa yawe, sasa na yeye anamaono yake.Hujawahi kujiuliza kwanini kuna baadhi ya viumbe wanaweza kuogelewa bila kufundishwa,na sie binaadamu hatuzaliwi na uwezo huo mpaka kujifunza.?

Tuachane na hayo naomba nkuulize swali,hivi ukiuangalia mwili wa binaaadamu na system nzima ya binaadamu ,uchakataji chakula,mfumo wa fahamu,ubongo na mifumo mingine ilivyo sofistiketedi,unaamini ni vitu vilivyotokea tu kwa bahati mbaya au kuna dizaina?
 
Unapenda mambo mteremko kiasi hiko
Siyo mimi ninayependa mambo mteremko.

Mungu wako ndiye hana logical consistency.

Ameandikwa kama Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Hana sababu ya kutowapa viumbe wake mteremko. Asiwape mteremko kwa nini?

Uwezo anao, upendo anao, ujuzi anao.

Sasa kama tunaona maisha hayana mteremko, tukiuliza kwa nini Mungu hajatupa mteremko si kwa sababu tunapenda mteremko.

Ni kwa sababu tunahoji kama huyo Mungu yupo, kama yupo, mbona anajipinga mwenyewe?

Inakuwaje baba mwenye uwezo, ujuzi na upendo anawafanyia uchoyo wanawe anaowapenda?

Hujajibu swali hili.
 
Nimejibu aya inanasema 'dhul qarnaini aliliona' sasa ww uelewi nn muonaji ni dhul qarnaini kwa upeo wa macho yake

Ni sawa ngoja tuelewe hivyo kwamba ni Dhul-Qarnaini (Alexander the Great) ndiye aliyeliona Jua likizama katika matope.Sasa tunajiuliza hivi Dhul-Qarnaini alizaliwa mwaka 356 na kufariki mwaka 323 kabla ya Kristu kuzaliwa na kabla ya Muhammad kuzaliwa.Je,yeye Muhammad kwa nini hakumuuliza Mungu ni kwa nini Dhul-Qarnaini aliweza kuliona Jua likizama katika matope wakati sio kweli? Mbona kwa mjibu wa aya hiyo inaonekana Muhammad alikuwa ameenda kuwashitakia kwa Mungu baadhi ya watu waliokuwa wanamuuliza Muhammad habari za Dhul-Qarnaini? Ilishindikanaje, Muhammad kumhoji Mungu juu ya ukweli wa hicho alichokuwa Mungu anamueleza kumuhusu Dhul-Qarnaini?
 
Sasa mkuu wewe unataka kumpangia namna gani aendeshe vile alivyoviunda na system nzima ya universe,yeye ndo kaamua iwe hivyo,hayo unayoleta ni mawazo yako ya jinsi mambo yangetakiwa yawe, sasa na yeye anamaono yake.Hujawahi kujiuliza kwanini kuna baadhi ya viumbe wanaweza kuogelewa bila kufundishwa,na sie binaadamu hatuzaliwi na uwezo huo mpaka kujifunza.?

Tuachane na hayo naomba nkuulize swali,hivi ukiuangalia mwili wa binaaadamu na system nzima ya binaadamu ,uchakataji chakula,mfumo wa fahamu,ubongo na mifumo mingine ilivyo sofistiketedi,unaamini ni vitu vilivyotokea tu kwa bahati mbaya au kuna dizaina?
Hapana, si kwamba nataka kumpangia.

Naonesha kwamba yeye mwenyewe hana logical consistency, anajipangia, halafu anavuruga alivyojipangia.

Anaumba, anaruhusu dhambi, halafu anajua dhambi itatokea, halafu ikitokea anakasirika na analeta mafuriko.

Tena mafuriko yanaumba mpaka viumbe wasio na hatia.

Kwa nini? Huyu ndiye Mungu wa haki kweli?

Huyu Mungu yupo kweli au ni uongo tu?
 
Watu wanakufa wanatengeana na wapenzi wao, familia zao marafiki.

Wwatu wanaumwa magonjwa.

Wwanapatwa na majanga, matetemeko, vita, moto, mafuriko, tsunami, wana umasikini, ujinga etc.

Mungu wako mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, alishindwa kuumba ulimwengu ambao yote hayo hayawezekani?
Katika ulivyo vitaja hapo nikipi kinacho kutesa?
 
Yaani kuna wakati huwa nawaza sana, jamii forum inasifika kwa kuwa na wanachama wanaojitambua na wenye bongo fikirishi (zisizokuwa na mipaka ya kufikiri) lakini unakuta mtu "anaropokwa" na maneno mpaka unashangaa hivi hawa ndo great thinkers wa nchi hii au ni kinyume chake...?.

Lipi limekufikirisha hivyo, mkuu?
 
Mungu sio mjinga kumwandikia.mtu aseyejua kusoma na kumwandikia uongo

Unamaanisha kwamba kwa kuwa Muhammad hakujua kusoma wala kuandika, basi Mungu asingaliweza kumfanyia roho mbaya ya hivyo ya kumuingiza chaka? Kama ndivyo,sasa umegundua nini katika aya hii ya Jua kuzama katika matope? Huoni kwamba tayari Muhammad aliingizwa chaka kwa kupewa hadithi ya jambo ambalo halipo?Na huoni tayari kwa kutojua kusoma kwa Muhammad kumemharibia CV yake?
 
Sasa mkuu wewe unataka kumpangia namna gani aendeshe vile alivyoviunda na system nzima ya universe,yeye ndo kaamua iwe hivyo,hayo unayoleta ni mawazo yako ya jinsi mambo yangetakiwa yawe, sasa na yeye anamaono yake.Hujawahi kujiuliza kwanini kuna baadhi ya viumbe wanaweza kuogelewa bila kufundishwa,na sie binaadamu hatuzaliwi na uwezo huo mpaka kujifunza.?

Tuachane na hayo naomba nkuulize swali,hivi ukiuangalia mwili wa binaaadamu na system nzima ya binaadamu ,uchakataji chakula,mfumo wa fahamu,ubongo na mifumo mingine ilivyo sofistiketedi,unaamini ni vitu vilivyotokea tu kwa bahati mbaya au kuna dizaina?
hivi unaelewa mantiki ya msamiati" muweza wa yote",na mwenyewe upendo kwa wote",.. utajisikiaje baba yako atakapo kwambia kuwa anauwezo wa yote na upendo kwa wote" kisha akapeleka nyama na mchele kwa bimkubwa "(mkewe WA Kwanzaa) halafu kwa bimdogo (mkewe wa pili ) ambaye ndiye mama yako akawalaza na njaa", tokana na ukosefu wa kuwepo kwa chakula nyumbani ""??

tunaposema muweza wa yote na upendo kwa wote huwa tunataka muelewe kwanza mantiki ya misamiati hiyo miwili""
 
Ni sawa ngoja tuelewe hivyo kwamba ni Dhul-Qarnaini (Alexander the Great) ndiye aliyeliona Jua likizama katika matope.Sasa tunajiuliza hivi Dhul-Qarnaini alizaliwa mwaka 356 na kufariki mwaka 323 kabla ya Kristu kuzaliwa na kabla ya Muhammad kuzaliwa.Je,yeye Muhammad kwa nini hakumuuliza Mungu ni kwa nini Dhul-Qarnaini aliweza kuliona Jua likizama katika matope wakati sio kweli? Mbona kwa mjibu wa aya hiyo inaonekana Muhammad alikuwa ameenda kuwashitakia kwa Mungu baadhi ya watu waliokuwa wanamuuliza Muhammad habari za Dhul-Qarnaini? Ilishindikanaje, Muhammad kumhoji Mungu juu ya ukweli wa hicho alichokuwa Mungu anamueleza kumuhusu Dhul-Qarnaini?
heheee heeehee
 
Mleta mada inaonyesha una kichwa kigumu kama nazi ya kilwa. Sasa hapo haujaelewa nini kwamba Dhul-Qarnain aliliona jua likizama kwenye tope kwa upeo wa macho yake?
 
Dini yoyote inayofundisha Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uuwezo wote na kaumba kila kitu mwanzo inafundisha predestination.

Hii inajumlisha Ukristo wote, si hayo madhehebu uliyoyataja tu.

Mkuu mimi ni mtu ninayejadili mambo kwa Logical Consistency.Leo niko na hoja ya Jua kuzama katika matope.Hili la kwako juu ya kwamba hakuna Omniscience,Omnipresence, Omnipotence, God with all Loving and with devine Mercy, nitayaletea uzi wake, siku yake pekee.Kwa hiyo usifikirie hizo hoja zako hazina hazina majibu.
 
Hapana, si kwamba nataka kumpangia.

Naonesha kwamba yeye mwenyewe hana logical consistency, anajipangia, halafu anavuruga alivyojipangia.

Anaumba, anaruhusu dhambi, halafu anajua dhambi itatokea, halafu ikitokea anakasirika na analeta mafuriko.

Tena mafuriko yanaumba mpaka viumbe wasio na hatia.

Kwa nini? Huyu ndiye Mungu wa haki kweli?

Huyu Mungu yupo kweli au ni uongo tu?
Sasa unapomkataza mtoto asiangalie tv usiku si lazima uihamishe kutoka sebuleni uifiche chumbani,utategemea mtoto mwenyewe atafuata maelekezo yako ya kutoangalia tv muda huo uliomkataza,sasa utakapotoka ghafla usiku kwenda sebuleni ukamkuta amekaidi amri uliyompa ukamuadhibu hatakuuliza kwanini umenikataza halafu TV umeiacha mpaka nkashawishika kuingalia ilhali umenkataza,hivyo ndivyo navyoilewa falsa ya dhambi,kwamba kwanini kitimoto kimekatazwa,alafu nguruwe wapo,au kwanini umekatazwa usile mke wa mtu alafu mwenzio alafu huyi mke akawa mzuri na anayetamanisha balaa.

unadhani kuna logic gani ya kuwepo magonjwa alafu kukawa na dawa na mitishamba yanayotibu magonjwa hayo,logical consistency iko wapi hapo.iweje napata mafua,alafu nkinywa tangawizi na asali au salimia,kinapona.hii system imetokea wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom