Hicho ulicho post ndio mstari kwamba Wakristo wana Mungu zaidi ya Mmoja?
Dhana ya kufa na kufufuka kwa Yesu si mafundisho ya Mungu
Kwa kweli, zaidi ya masimulizi ya Wainjilisti na wanaadamu wengine kwa ujumla, hakuna kamwe mafundisho sahihi ya Mungu yanayothibitisha kufa na kufufuka kwa Nabii Isa au Yesu (a.s.).
Kinyume chake, tunaona maandiko mengi ya Mungu yanashutumu vikali tendo zima la mtu kusulubiwa kwa kutundikwa mtini, kama lile linalodhaniwa kufanyika kwa Bwana Yesu (a.s.)
Na ndio maana sambamba na kutoa amri ya Pasaka kabla ya kuzaliwa Yesu, tendo hilo (la mtu kutundikwa) mapema Mungu alilishutumu vikali kwa kusema:
"...kwa aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu..." (Kumbukumbu la Torati 21:22-23).
Aidha, kabla ya shutuma hiyo (ya Mungu) dhidi ya mtu aliyetundikwa (aliyesulubiwa), Mungu alieleza bayana wasifu wa laana kwa mtu, kwa kusema:
"Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizapo leo; na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine". (Kumb. 11:26-28)
Kuhusu laana, Mungu pia hakuacha kuelekeza mahali ambako laana yake hupatikana kama tunavyosoma maandiko yafuatayo:
"Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki". (Mithali 3:33).
Kwa shuhuda hizo, tunachojifunza hapa ni kwamba yeyote aliyetundikwa (aliyesulubiwa) basi anahesabika kuwa amelaaniwa, asiyesikiza maagizo ya Mungu na kukengeuka njia yake, mshirikina (anayemuabudu Mungu pamoja na miungu mingine) na kwa ujumla mtu huyo ni mwovu (rejea Mithali 3:33).
Zaidi ya hivyo, kwa maandiko hayo, yaonyesha wazi Mungu hafurahishwi na kwa ujumla hapendi tendo la mtu kusulubiwa. Kwa mantiki hiyo, ni dhahiri kuwa dhana ya kusulubiwa Yesu ingelikuwa sahihi iwapo tu Mungu asingelishutumu tendo la mtu "kusulubiwa" kwa kiwango hicho, hasa unapolinganisha shutuma hizo (za Mungu) na hadhi, utukufu na ucha Mungu kwa ujumla wa Bwana Yesu (a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu. Isitoshe, Mungu asingeacha kueleza tukio zito na 'muhimu' kama hilo kwa ufasaha, kwa uwazi na kwa maelezo ya kukinaisha.
Aidha, dhana hiyo ya kusulubiwa Yesu pia ingelikuwa ni sahihi na tendo la wokovu, iwapo tu Yuda Iskariote angeliitwa "mwokozi wa kwanza" kwa 'kuharakisha' wokovu wa walimwengu, kinyume na anavyoitwa mpaka sasa kwamba ni "msaliti" aliyemsaliti Yesu! (tazama Mathayo 26:25). Kwani inasimuliwa kuwa ndiye aliyewaonyesha maadui wamuue Yesu baada ya kuahidiwa fedha (tazama Mathayo 26:14-15). Ni ajabu watu wa timu moja wamshutumu mtoa pasi kwa mchezaji aliyeifungia goli timu yao!
Vile vile dhana hiyo (ya kusulubiwa Yesu) ingekuwa sahihi na tendo la "ukombozi" wa wanaadamu, iwapo tu Yesu asingemkemea mapema yule atakayemsaliti kwa kumwambia:
"...
Lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa". (Mathayo 26:24)
Kinyume na andiko hilo juu, dhana ya kusulubiwa Yesu ingekuwa sahihi na nzuri iwapo Yesu angelimpongeza yule atakayemsaliti, kwa kumwambia:
"
Heri yake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa vibaya kwake mtu yule asingezaliwa". n.k.
Na kubwa zaidi, masimulizi ya Mwinjilisti Mathayo ya kudai kuwa eti Yesu alipokuwa msalabani alisema: "... Eloi, Eloi, lamasabakhtani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" (Tazama Mathayo 27:46) yanapingwa vikali na mwenyewe Bwana Yesu (a.s.) kwa kusema:
"
Naye aliyenipeleka yu pamoja nami; hakuniacha peke yangu, kwa sababu nafanya siku zote yale yampendezayo". (Mathayo 8:29).
Kwa kauli hiyo peke yake ya Yesu inadhihirisha wazi kuwa yule aliyekuwa akilalamika kuachwa na Mungu hapo msalabani hakuwa Yesu. Yesu hawezi kuachwa na Mungu kwa sababu kama mwenyewe anavyoeleza katika andiko hilo hapo juu kwamba siku zote hufanya yanayompendeza Mungu.
Na kwa ujumla ukombozi wa wanaadamu kamwe haupatikani kwa njia ya laana (kusulubiwa) ambayo i katika nyumba ya waovu. (Mithali 3:33).
Na ndio sababu, kutokana na uzito wa shutuma za Mungu dhidi ya mtu anayesulubiwa (kama tulivyoona hapo awali), Mwenyezi Mungu katika Qur'an Tukufu akaeleza wazi kwamba:
"
Hawakumwua wala hawakumsulubu". (Qur. 4:158).
Kwa maandiko haya na mengine mengi ni dhahiri kuwa dhana ya kufa na kufufuka Yesu katu haimo katika mafundisho ya Mungu. Na kwa mantiki hiyo, Pasaka iliyofundishwa na Mungu haina uhusiano wowote na dhana ya kufa na kufufuka kwa Yesu hasa ukizingatia kuwa Pasaka hiyo (ya Mungu) imekuwepo kabla ya Yesu kuzaliwa, na pia kufa na kufufuka kwa Yesu ni jambo lililozuliwa na wanaadamu baada ya Yesu kuondoka