tuwekee mashahidi. 3 kama alicho ongea baba kasimu ni kweli [emoji117]
View attachment 870626 amezoea uongo ili kuridhia wakeze [emoji53] Ndipo nikajiuliza au kwa mujibu wa uisilamu Maneno haya ya MUNGU [emoji117]
View attachment 870629View attachment 870630 ni Msamaha [emoji47] [emoji47] [emoji53]
Pili, kwa kujaribu kutatua tatizo la Adamu kwa kutoa shauri ya kuwa dhambi inahamishwa kwa vizazi vijavyo ambavyo vinairithi
tangu kuzaliwa, msingi wenyewe unabomolewa ambao juu yake imani ya 'Dhambi na kafara' imejengwa.
Kama Mungu ndiye mwadilifu halisi, basi upo wapi uadilifu katika kuwahukumu wazao wote wa Adamu na Hawa kwa dhambi yao waliyotenda mara mmoja tu na kisha wakatubu pia?
Kwa vyovyote, hiyo ilikuwa dhambi ambayo waliadhibiwa vikali kwa sababu yake na wakafukuziliwa mbali katika Pepo kwa
fedheha kubwa .
Ni aina gani ya uadilifu ya kwamba baada ya kuwaadhibu Adamu na Hawa sana sana kupita kiasi kwa sababu ya dhambi yao, bado hamaki ya kujilipiza kisasi haijapoa na akawahukumu wanadamu wote wapate fedheha ya kuzaliwa tayari wamerithi dhambi?
Nafasi gani wanayo wazao wa Adamu kuikwepa dhambi?
Kama wazazi wanafanya kosa, kwa nini watoto wao wasiokosea wasumbuke daima kwa sababu ya kosa la wazazi wao?
Kama ni hivyo, basi batilifu iliyoje maana ya uadilifu anayojidaia Mungu na kuifurahia ikiwa Yeye anawaadhibu watu
waliopangiwa kutenda dhambi hata wakichukia dhambi namna gani?
Dhambi ikafanywa sehemu ya maana sana ya maumbile yao. Hamna kabisa sasa nafasi kwa mtoto wa Adamu kubaki
katika hali ya kutokuwa na dhambi. Kama dhambi ndiyo jinai basi ni jinai ya Mwumbaji siyo ya viumbe.
Basi, uadilifu gani ungetaka kuwaadhibu wasiokosea kwa jinai za wengine?
Tangazo la Kurani Tukufu ni tofauti kabisa na ufahamu wa Kikristo wa dhambi na matokeo yake. Kurani Tukufu inatangaza:
Hakuna mbebaji atakayebeba mzigo wa mwingine. (35: 19)
Mungu haikalifishi nafsi yoyote zaidi ya uwezo wake. (2:287)
Tangazo hilo la Kurani kwa kulinganisha na imani ya Kikristo kuhusu Dhambi na Kafara ndiyo taratibu halisi ya kuituliza roho.
Sasa tugeukie maelezo ya Biblia kuhusu yaliyotendeka hasa wakati Adamu na Hawa walipotenda dhambi, na matokeo
yaliyofuata nyuma ya wao kuadhibiwa.
Sawa na mafunzo ya Mwanzo, Mungu alikubali nusu-nusu udhuru wao na wakapewa adhabu ya kudumu milele inavyoelezwa hapa chini:
Wanadamu walikuwapo muda mrefu sana kabla hawajazaliwa Adamu na Hawa. Wanasayansi wa magharibi wenyewe
waligundua mabaki ya watu wengi waliokuwepo ardhini katika zama za kale sana na wakawapa majina mbali mbali ya
kupambanua. Neanderthal - mtu pengine ndiye anayejulikana zaidi miongoni mwa hao.
Wa-Neanderthal waliishi zaidi katika Yoropa,Mashariki ya Karibu na Asia ya Kati, baina miaka 100,000 na 35, 000 mpaka sasa. Maiti ya mtu mkamilifu imenguduliwa ambaye mtu huyo aliishi ardhini miaka 29,000 kabla Adamu na Hawa hawajaanza safari yao fupi huko Peponi.
Katika zama hizo wanadamu kimaumbile walikuwa kama sisi na waliishi katika Yoropa, Afrika na Asia, na baadaye mnamo zama za Theluji (Ice Age) walienea hadi Marekani pia. Vilevile huko Australia historia thabiti ya utamaduni wa Waaborijini (Aborigines) inaonesha ulianza miaka 40,000 iliyopita kutoka leo. Waaborijini ni watu wa asili ya Australia.
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto, na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo kwa hiyo ulitwaliwa kwa maana u mavumbi wewe nawe mavumbini utarudi (Mwanzo 3:16-19)
Kwa kulinganisha na zama za hivi majuzi, mifupa yote ya mwili ikiwa pamoja, ya mwanamke, imepatikana huko Hedar katika Ethiopia ambayo mifupa hiyo ni ya tangu miaka milioni 2.9. Sasa kwa kulingana na matukio ya historia yalivyoelezwa katika Biblia, Adamu na Hawa waliishi karibu miaka 6,000 tu tangu leo.
Mtu aweza kuangalia nyuma kwa mshangao taarifa ya historia ya wanadamu, ama Homo Sapiens wanavyoitwa katika istilahi
ya Kisayansi