Ila ANAWEZA KUWA Kijinga cha moto [emoji15] [emoji4] mnaangamia kwa kutojua kusoma hadi hamumjui Mwenyezi unamsujudia popo bawa [emoji12]
Ushuhuda mwingine wa kuhakikisha kuwa Yesu alikuwa bado hai wala hakufa ndiyo ufuatao: Baada ya siku tatu, mchana na usiku, watu wa kawaida hawakumwona isipokuwa wanafunzi wake tu. Au tuseme akijitokeza mbele ya wale tu aliowategemea.
Yeye hakuonana nao katika mwanga wa mchana bali katika giza la usiku.
Mtu anaweza kutambua kutokana na maelezo ya Biblia ya kuwa Yesu anataka kuondoka katika hali ya hatari haraka sana na kwa kujificha.
Pana swali hapa: Kama yeye alikuwa amejaaliwa uhai mpya wa milele baada ya kifo chake cha kwanza wala asingeweza kufa tena, kwa nini alijificha asionekane mbele ya maadui, yaani wajumbe wa serikali na watu wa kawaida?
Ilimpasa kujitokeza mbele ya wajumbe wa serikali ya Kirumi na Wayahudi pia na kuwaambia:
'Nipo hapa nikiwa na uhai wa milele. Jaribuni kuniua tena kama mtaweza, lakini hamtaweza kamwe'.
Lakini alihitaji kujificha.
Siyo kwamba rai ya kujitokeza hadharani hakupewa; bali kinyume chake alishauriwa waziwazi ajidhihirishe kwa ulimwengu, lakini akakataa na akaendelea kwenda mbali ya Uyahudi ili mtu yeyote asiweze kumsaka:
Yuda (siye Iskariote) akamwambia, Bwana imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? (Yohana 14:22)
Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kamaanataka kuendelea mbele. Wakamshawishi wakisema, kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana umekwisha. Akaingia ndani kukaa nao. (Luka 24:28-29).
Hilo linahakikisha ya kwamba yeye alikuwa mtu mwenye kufa asiye mbali na kufikiwa na mauti ama majeraha. Hiyo inayonesha
tu ya kwamba Yesu alikuwa hajafa katika maana hii ya kwamba akaondolewa ule ubinadamu uliokuwamo ndani yake, bali akabaki kabisa kama alivyokuwa wala kifo hakikutokea kumtenganisha na mwili wa zamani na kumpa mwili mpya. Ndiyo kusema
kwamba aliendelea kuishi pasipo kufa.
Roho inayohusikana na ulimwengu mwingine kabisa haitendi jinsi alivyotenda Yesu wakati alipokutana na marafiki na wafuasi wake kisiri saa za usiku katika giza.
Suala la Yesu kuwa roho limekataliwa katakata na Yesu mwenyewe. Yeye alipojidhihirisha kwa baadhi ya wanafunzi wake, hao wanafunzi hawakuweza kuficha hofu yao kwani walimwamini kwamba huyo siye Yesu mwenyewe bali ni roho yake.
Yesu Kristo akitambua tatizo lao akafutilia mbali hofu yao kwa kukataa kwamba yeye siye roho bali yu Yesu yuleyule aliyekuwa amesulubiwa, hata akawakaribisha wachunguze wenyewe majeraha yake ambayo bado yalikuwa mabichi (Yohana 20:19-27).
Kudhihirika kwake kwa wanafunzi na wengineo hakuhakikishi kwamwe ya kwamba yeye alifufuka katika wafu.
Kilichothibitika ni kwamba yeye alipona katika uchungu wa mauti.
Yaonekana ili kuwaondolea shaka waliyokuwa nayo bado nyoyoni mwao, yeye akawauliza walikuwa wanakula nini. Na alipoambiwa kwamba walikuwa wanakula mikate na samaki, akawaomba apewe yeye pia kwani alisikia njaa na akala (Yohana
24:41-42).
Hilo pasipo shaka yoyote ndilo hakikisho dhidi ya yeye kufufuka katika wafu, yaani kurejea ile hali ya asili ya mtu aliyekwisha kufa na kuhuika tena. Matatizo yazukayo kutokana na kuhuika huko yatakuwa mara dufu.
Kama Yesu bado alikuwa kitu kama mungu-mtu, jinsi inavyodaiwa alikuwa kabla ya kusulubiwa, basi alikuwa bado hajaepukana na 'mtu' ndani yake.
Hilo linazusha hali ngumu ya kutatanisha. Kifo kilimfanya nini ama kiliwafanya nini, yaani yule 'mtu' ndani ya Yesu na yule 'mungu' ndani yake?
Je, roho za wote wawili, 'mtu' na 'mungu', zilitoka na zikarejea ndani ya mwili huo huo wa udongo, baada ya kukaa katika jahanamu ile ile pamoja, ama hiyo ilikuwa roho ya mungu ndani ya Yesu iliyorejea katika mwili wa kibinadamu bila ya kufuatana na roho ya mtu?
Roho hiyo ya mtu ilipotea wapi?
Mtu anashangaa. Je, safari yake kwenda katika jahanamu iliishia mumo humo pasipo kurejea, ilhali roho ya mungu ndani yake ilikaa tu humo kwa siku tatu mchana na usiku?
Na Je, Mungu alikuwa baba wa Yesu-mtu ama Yesu mwana?
Suala hilo linapaswa kutatuliwa kwa kutupatia picha safi. Je, mwili wa Yesu ulikuwa nusu wa Mungu na nusu wa mtu?
Fikara kumhusu Mungu tunayopata kutokana na Agano la Kale na Agano Jipya ni kwamba hana mwili, tena ameenea mahala pote, dhati yake siyo ya kiwiliwili.
Tukiisha zingatia hiyo, hebu sasa tugeukie nyuma kumwangalia Yesu ambapo alikuwa anapita katika hali mbalimbali za kukua akiwa mimba ndani ya tumbo la uzazi la Mariamu. Kitu alichoumbika nacho Yesu kilitolewa chote na mama wa kibinadamu, hata sehemu sawa na punje ya haridali haikutolewa na Mungu Baba.
Naam, Mungu angeliweza kumwumba kimuujiza. Lakini kulingana na maoni yangu, kiumbe ni kiumbe tu hata akiumbwa kikawaida ama kimwujiza. Twaweza kumkubali mtu kuwa baba wa mwanae hapo tu mwana huyo anapoumbika kutokana na mwili wa baba na mwili wa mama kwa usawa au kwa uchache sehemu walau ndogo sana wa mwili wa baba ipatikane katika uumbaji wa mwana.
Kutokana na maelezo hapo juu inapaswa kubainika kwa msomaji ya kwamba Mungu hakufanya kazi yoyote ya baba kabisa katika mimba kushikwa. Na kiwiliwili kizima pamoja na taratibu kuhusu moyo, kupumua, na utaratibu wa mwanzo na kuhusu ufa katika ini, mpango wa seli na taratibu ya neva, vyote hivyo viliumbika kutokana na mama wa kibinadamu pekee bila ya kusaidiwa na mwingine yeyote awaye.
Basi iko wapi sehemu ya 'Uana' katika Yesu ambaye alikuwa ni chombo cha kuwekea roho iliyoumbwa na Mungu tu?
Ufahamu huo mpya wa uhusiano baina ya Mungu na Yesu unaweza kuelezwa kiakili kwa namna lakini siyo kama uhusiano wa baba na mwana.