Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Boss unaona uislam unavo take point.

Maana yangu kukuuliza haya maswali najua majibu ya maswali ulio niuliza yamo humo.

Kwahiyo nauhakika kam kweli ww n msomi umeamua kuusoma uislam na umeelewa kwann nmekuuliza hayo maswali. Majibu umeyaona humo.

Sasa basi we nijibu hayo maswali mawili uone.
Haha

Hapo ndo majibu yapo. So we nijibu hayo maswali nkupe elim kabla sija lala bro
Simply huna majibu ya nani alishuhudia Muhamad akishushiwa quran
 
Suala la Yesu kutembea juu ya maji, suala la kubadilisha maji kuwa mvinyo na kujaza makombo ya samaki wawili wasiojaa hata robo ya kikapu kwenye vikapu kumi. Kisa cha Mussa kapiga maji kwa fimbo yakagawanyika, Joshua kusimamisha Jua ambalo halizunguki,YOTE HAYO ni miujiza.Sasa naomba kuuliza kuwa suala linaloongelewa na Muhammad mintarafu sula la Jua kuzama ni muujiza ndio ulikuwa unatokea?
Kwa hiyo Yoshua alisimamisha jua au alisimamisha dunia? Na kama alisimamisha jua jee kwanini MUNGU hakumwambia nabii wake kwambo kilichosimama sio jua bali ni Dunia?
 
Ni rahisi sana hoja yako,mfano hai kama wewe hapo,umepewa kila kitu na aliekuumba akakuacha huru umkubali au umkatae alie kuumba,lakini wewe umemkataa kwa makusudi alie kuumba kisha wewe unamlaumu yeye alie kuumba kwa kumkataa,inaingia akilini?
Kwamba aliyeniumba kaniacha huru si kweli.

Watu hata uhuru wa kuchagua watazaliwa nchi gani hawana.

Na wanaozaliwa Saudi Arabia kwa wazazi wa Saudi Arabia karibu asilimia mia wanakuwa Waislamu.

Na wanaozaliwa Nepal kwa wazazi wa Nepal karibu asilimia mia wanakuwa Buddhists.

Maana yake pahali ambapo unazaliwa na wazazi wanaokuzaa kwa watu wengi ndiyo vigezo vya dini zao.

Sasa kama mtu hawezi kuchagua atakapozaliwa, utasemaje ana uhuru?

Utasemaje nimemkataa muumba ambaye hata huwezi kuthibitusha kwamba yupo?

Kama yupo, kwa ninibkajiweka uwepo wake uwe na utata sana?

Mungu ambaye ana uwezo wote ea kujiweka wazi akijificha ficha awe na utata tusimwelewe, halafu tusipomwelewa na kusema hayupo, hapo sisi tutakuwa tumemkataa yeye au yeye katukataa sisi?
 
Ulileta maswali uliyoyaokota answering islam na nikakuwekea majibu ya maswali yako

Mbona hujatoa hoja hata moja kutokana na maswali yako ambayo yamejibiwa,unakuja unaruka ruka tuuu???

Hata hujasoma hata moja ukapata hayo majibu yako unayoyauliza , unakuja na habari za Mungu zina utata,

Si ndio Ukauliza ili uondoe utata au vipi ?? Na majibu umepata lakini kusoma hutaki unatafuta ubishi
Nipo njiani kwenye simu hapa. I cant dissect the minutia of that post.

Nimekuuliza hivi, unajua kwamba hoja ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuwa na utata tu inaonesha huyo Mungu hayupo?

Unaelewa kwamba huu mjadala wa kuuliza kama Mungu huyo yupo ninushahidi kwamba hayupo?

Unaelewa kwamba angekuwepo, kila kiumbe kingetambua hilo bila utata wowote na wala kusingekuwa na mjadala wowote kuhusu kuwapo kwa huyo Mungu?
 
Kuna aliyeweza kuthibitisha kwa namna yenye mantiki isiyopingika kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu yupo?

Akithibitisha mtu suala hili naomba mnijulishe.

Na kama hamjaweza kuthibitisha, habari za Mungu huyo zote ni hadithi tupu zisizo na uthibitisho.
 
We mi nakuuliza maswali mawili ukiyajib bas nakupa habari zote za kuthibitisha mungu yupo.

1. Bina dam wa kwanza ni nani?
2. Nani kaileta hii dunia tunayoish?

We hujashituka tu.mungu kakuongoza na ndo maana anataka umjue.

mi naamin utamjua na utamtumikia vzr sana kulikon ata sisi tusie na shaka nae
1. Habari ya bin adam ni uongo. Bin Adam maananyake ni mwana wa Adam.

Adam hakuwahi kuwepo. Ni hadithi tu.

Kwa hivyo habari nzima ya "Bin Adam wa kwanza" imejengwa katika msingi potofu.

2. Swali la "nani" kaileta dunia hii lina assume kuna mtu/ Mungu/ dubwana lenye nafsi na kuweza kuitwa nani. Swali hili ni potofu. Ni kama kuuliza "rangi ya wimbo wa taifa ni rangi gani?". Swali limeanza kwa ku assume wimbo wa taifa una rangi. Wrong assumption. Wrong question.

Maswali yako yote yameulizwa kwa wrong assumptions.

Thibitisha Mungu yupo na wewe.
 
Kuna aliyeweza kuthibitisha kwa namna yenye mantiki isiyopingika kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu yupo?

Akithibitisha mtu suala hili naomba mnijulishe.

Na kama hamjaweza kuthibitisha, habari za Mungu huyo zote ni hadithi tupu zisizo na uthibitisho.
Tuwekee Ushahidi Mungu anaongea na Muhammad!
hoja yako iko wap
 
Wanajukwaa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.

Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?

2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?

3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?

· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?

· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
Swali la msingi la mtoa mada limejibiwa sasa aya mengine sijui hakuna Mungu mara mohamad sijui kaongea na mungu yafunguliwe uzi mwengine pia tutayajibu hakuna matata
 
Ameshindwa kujibu swali la kwa nini anashambulia uongo wa Quran, halafu anakubali uongo wa Biblia.

Nimemwambia yuko sawa kusema Quran ina uongo (kwa sababu ina uongo kweli) lakini, kama kweli hataki uongo, akubali kwamba hata Biblia nayo ina uongo.

Anakimbia swali hilo.

Kwa sababu nia yake si kukataa uongo.

Nia yake ni kushambulia Quran.
Ahahahahahahahhhaha awez fanikiwa hoja yake imekufa wako wengi humu mtu anatoa mada kama great thinker kumbe ni mfia dini
 
kule jabar hilla muhammad alikabwa na hakujua nani aliye mkaba, hadi anakuja fahamishwa Akiwa kwake kwamba aliye mkaba ni gibril aliye mtokea issa na Musa hivyo muhammad anaelekezwa na Waraga ajibashirie mwenyewe kwamba yeye ni Mtume Wa Umma huu...ndio sababu nina Hakika allah na muhammad hawaja wasiliana popote hadi amemtuma kuwa mtume, labda walete Ushahidi!
Fungua uzi tutakujibu bila shaka kuhusu dhul qarnaini limekwisha ndio maana mnarukaruka
 
Kwa nini unanikataza kukikosoa kitabu kama kina uongo?

For starters, anza na Feynman's Lectures on Physics. Cha Richard Feynman. Series ya Lectures ina vitabu vitatu. Pitia vitatu vyote. Fanya na mazoezi yake.

Halafu nenda kwa Roger Penrose. Soma " The Road To Reality: A Complete Guide To The Laws of The Universe".

Hicho unaweza kusoma polepole huku ukipozea na "A Brief History of Time: From The Big Bang To Black Holes" cha Stephen Hawkings.

Halafu uje tujadili hapa.

Not that havina makosa, but the worldview is quite above the bullshit in the Quran and Bible. Plus it does nit clain to be beyond reproach. You can get a Nobel in Physics for improving this outlook.

Unlike the Bible or Quran.

Soma halafu tujadili.
Bahati mbaya zaidi baada ya miaka kadhaa kupita navyo vitaonekana ni uongo kama vinavyoonekana vingine. MATERIALISM BELIEVED IN THEIR OWN PROVED FACTS NOT FROM OTHER.
 
Sema tu hujui brother. Unachokisema hakipo hivo.
Hakupokea akiwa pekeake broo.
Kasome vzr.

Uislam si din ya kusoma juu juu ukaja apa kuandika comment.

Unahitaj deep investigatio na intesive reading ndo utaweza bro.

Mtaaibika jmn. Uislam kila kinachoandikwa mule dunia inafanya research mpka leo wana prove n kwel.

Mkuu nataka kujua mashuhuda akina nani siamini saana dini za watu weupe
 
Mimi na wewe tunaweza kufahamu hivyo lakini ushahidi wetu ni upi juu ya hilo? Kwa mjibu wa Kurani,Mungu ndiye alimuona Alexander the Great (Dhul-Qarnaini) akiliona Jua likizama katika matope.Sasa mwenzangu mimi na wewe tuna ushahidi gani au ubavu gani wa kupingana na Mungu?
Ha matope gani juu lizamie?
Kisayansi maji ni H2o sasa maji yakikaribia jua molecules za hydrogen na oxygen zina separate through evaporation .
Jua ina composition kubwa ya hydrogen na oxygen ikiongozeka combustion (burning) ina take place

Huo ndio ushahidi wangu
Huo wa kuzama kwenye tope ni mawazo ya kitoto na ya kijima
 
UKIWEZA KUJIBU HAYA MASWALI UTAJUA MTUME MUHAMAD ANAKUPA SAYANS HALISI SIO UBABAISHAJ WA KIZUNGU.

1.Swali la kujiuliza n kwamba ulisha liona jua halizami????
na kama halizami huwa linaenda wap!!!

2.Je mchana likipungua makali huwa linakuwa limezama au yanaenda wap?

3.kwannn asubuhi jua ni moderate.mchana ni kalisana na usiku halipo?

Jiulize kama lingekuwa halizami bas kwann ukali wa jua la asubuh si mkali kama mchana?

Kwann yote yasiwe the same kwa ukali?

Hahaa sasa naona u get my point kwann rasul(saw) anakufunulia sayans isiyo na mashaka ndan yake.

4. TAMBUA TU: jua kutozama cjui dunia kujizungusha katika muhimili.
HIZI NI THEORY TUU SIO KWAMBA NDO UKWELI ULIVYO. HILI NI JOPO LA WAZUNGU LILIKAA CHINI LIKABUNI HIVYO .NENDA FORM ONE UKAANGALIE HIZI HABAR KOTE WAMEKUAMBIA THEORY TU HZ.

ukiweza kujib haya maswal naweza kukupa details kiundan sasa.

Then nkakujibu na maswal mengine ulo uliza
Uki North Pole jua halizami miezi sita na ukiwa South Pole hivo hivo ukiwa kwenye space (anga za juu )jua hali zami daima inaliona iko sehem1 tu
 
Hiyo aya mbona imekaa kama 'code' na sio km inamaanisha ivo ulivyo tafsiri wew mtoa uzi. Kwa uelewa wangu " chemchem yenye matope meusi ndipo alipotakiwa kwenda (destination) huyo aliyepewa njia za kila ktu (Dhul Qarnain) na kuzama kwa jua kweny matope meusi ilikuwa ndo km inamwongoza kufika pale alipohitajika. Itakapofikia unaona jua linazama kweny matope meusi basi hapo ndipo unapotakiwa kuwepo. Au sio hivyo!?
 
Wanajukwaa:

Dunia yetu inaendelea kushika kasi katika suala la Sayansi na Tekinolojia.Kwa siku za hivi karibuni,wanasayansi wamegundua kuweza kutengeneza Moyo kwa kutumia stem cells,ikiwa ni hatua katika kuelekea kutengeneza moyo wa binadamu,hali ambayo itasaidia katika kukabiliana na matatizo ya Moyo yanayowakabili wanadamu,kwa kiasi kikubwa, yale ambayo uhusisha mwanadamu kupoteza maisha, kwa sababu tu Moyo wa mgonjwa husika hauna repair au hauwezi kubadilishwa.Miaka kama kumi hivi iliyopita,wanasayansi walikuwa wamefanikiwa kutengeneza Moyo wa panya kwa kutumia hizo stem cells.

Kumbe,kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali duniani,ama ardhini au angani,zote zinalenga katika kuboresha maisha ya mwanadamu na hata kuongeza siku za kuishi kwake.Historia inao watu wengi sana ambao wamejihusisha na Sayansi kwa nyakati tofuati tofauti.

Leo,ninataka tumuangalie Mtume Muhammad kwa namna alivyoweza kujihusisha na suala la Sayansi kwa kile kinachosemwa ni kwa msaada wa Mungu.Kurani neno la Mungu;maneno ambayo Mungu akiisha kuyaandika huko Mbinguni, alikuwa anampatia Malaika Gabriel na malaika Gabriel akampatia Mtume Muhammad katika Nyakati tofauti tofauti na Muhammad kuyaweka katika maandishi,lakini kwa namna ya pekee,kwa mara ya kwanza kabisa ikiwa ni katika Pango lililoko katika Mlima Hira, Jabal an-Nour,huko Makka,ambako inadaiwa Mtume Muhammad alipokea ufunuo huo, kwa matatizo sana kwa sababu ya kutojua kwake kusoma na kuandika,Malaika Gabrieli alijikuta anamkaba.

Kwa njia ya ufunuo wa Kurani,tunafunuliwa mambo mengi ya Kisayansi ambamo Muhammad anatujuza jinsi mambo yalivyo.Kwa leo, ninawaletea jambo moja tu.Nalo ni juu ya namna Jua linavyokuchwa na kadri Mungu atakavyotujalia tutayaangazia na mambo mengine.

Kurani kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Wakati Muhammad akiwa ametupasha ukweli huo ambao aliandikiwa na Mungu, Ukweli wa kisayansi umebainisha kwamba Jua ni kubwa zaidi na lenye joto kali kuliko dunia.Na ikitokea kwamba Dunia inakaribiana na Jua,basi dunia itayeyuka kutokana na joto kubwa la Jua.

Ukweli mwingine,ambao pia Sayansi imetupatia ni kwamba Jua halitembei bali sayari mbalimbali ndio hulizunguka,ikiwemo Sayari yetu ya Dunia. Historia inaonyesha kwamba mtu wa kwanza kugusagusa habari za kuwa Jua lilikuwa halizunguki alikuwa ni Aristarchus (310-230KK).

Aristarchus alikuwa ni mwana-Astronomia wa Kigriki.
Yeye aliamini dunia ilikuwa katikati ya Mfumo wa Jua(Solar system) na sayari zingine (ikijumuishwa na nyota ambazo zilikuwa zimefungwa katika nafasi fulani) ndio zilizokuwa zikilizunguka Jua.

Hata hivyo, baadaye mwanasayansi,Aristarchus, alikuja kugundua kuwa sio dunia iliyokuwa katikati ya Mfumo wa Jua, bali ni Jua na hivi kwamba ni Dunia na sayari zingine ndizo zilikuwa zikilizunguka Jua.Ugunduzi wa namna hii ulipatikana miaka mingi sana (takribani karne tatu hivi) kabla hata ya Yesu Kristu kuzaliwa na karne tisa kabla ya Muhammad kuzaliwa.

Mwanasayansi mwingine pia aliyekuja na mtizamo tofuati na wa Muhammad (kwa kadri ya ufunuo kutoka kwa Mungu) ni Jean Buridan (1300-1359/61). Huyu) anafahamika kama Mwanafalsafa Mashuhuri sana katika Ufaransa.Buridan alikuwa Mwalimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Paris kwa kupindi chote cha maisha yake ya kitaaluma akimakinika hasa hasa katika masuala ya Logiki (Logic) na kazi za mwanafalsafa Aristotle.

Ni Bridan aliyeanzisha wazo juu ya kiitwacho Copernican Revolution katika Ulaya.Hili ni fundisho lililoleta mwangaza kutoka kuamini kwamba dunia ilikuwa imesimama sehemu moja katika ulimwengu na kwamba Jua ndio lilikuwa linaizunguka dunia (Geocentrism) hadi kueleweka kwamba kumbe Jua ndilo limesimama wakati dunia na sayari zingine zikilizunguka (Heliocentrism).

Kumbe, sasa kwa uchache,kwa mawazo ya hao wanasayansi wawili,tunapata picha kwamba Muenendo wa Jua kuchomoza na kutua sio jambo lililoanza wakati wa Muhammad.Na kama suala la Sayansi ya Mfumo wa Jua lilianza mapema kabla ya Yesu na Muhammad kuzaliwa, yeye Muhammad alipopewa ufunuo na Mungu, hakuweza kujiuliza iwapo ufunuo huo wa Mungu inakuwaje unapingana na ukweli wa mambo?Katika kutafakari ufunuo huu wa Mungu kwa Muhammad, nimejikuta nina maswali yafuatayo,ambayo naomba yatuongoze katika kujadili suala hili.Ni muhimu kujadili kwa sababu pengine Dunia inatufundisha vitu ambavyo havipo.Hivi kweli Mungu anaweza kumueleza Muhammad mambo ya uongo?Maswali mengine ambayo bila shaka hata wewe unaweza kujiuliza ni haya:

1. Hiyo Chemchemi ya matope mazito na meusi iko hapa duniani?Na kama haipo hapa duniani iko angani? Na kama iko angani iko sehemu gani?

2. Huyo Dhul-Qarnaini alikuwa ni kiumbe wa namna gani huyo aliyepewa uwezo wa kuona Jua linavyotumbukia katika matope?

3. Pamoja na kwamba wakati wakati wa Muhammad, labda Sayansi ya kwamba Jua halizunguki, isipokuwa dunia ndio hulizunguka Jua, ilikuwa haijafika katika maeneo ya ardhi ya Arabia, bado hata vizazi vya zamani sana havikupata kuwa na uelewa kama huo wa Muhammad kuwa Jua lilikuwa linatua matope meusi! Je,ilikuwaje katika Vizazi vyote hivyo hapo katikati(ikiwemo na Yesu mwenyewe ambaye Muhammad anamuelezea kama aliyekuwa na uwezo wa kufinyanga wanasesere na kuwapulizia uhai na wakawa ndege kamili), kabla ya Muhammad, akakosekana mtu mwenye uelewa wa kuliona Jua likizama katika matope meusi tofauti? Hivi wewe kwa sayansi hii ya Muhamma juu ya Jua kuchwea katika matope meusi haikupelekei kujiuliza yafuatayo:

· Je, Muhammad kusema mambo ambayo hakuwa nayo uthibitisho ilikuwa ni kutafuta tu kuonekana kwamba Mungu amempa ufunuo wa kipekee juu ya ulimwengu?

· Je, vizazi ya Kiarabu na dunia kwa ujumla baada ya kugundua kwa tafiti za kisayansi, ambazo zimethibitisha kuwa Jua huzungukwa na sayari mbalimbali, ikiwemo Sayari yetu ya dunia, vimuoneje, Muhammad na Uislamu kwa ujumla?

· Je,wanadamu wa vizazi vyote vinavyofahamu kuwa Jua halijawahi kuzama katika matope ama meusi,bluu au meupe, visimuamini Muhammad katika mambo mengine aliyoyasema au vimuchukulie kama mtu aliyekuwa anajaribu kupiga ramli ya jinsi mambo yalivyo?

Lakini swali la mwisho kabisa ambalo nitaomba ujiulize ni hili:Je,Ni kwa nini hadi leo baada ya kugundulika kuwa Jua halizami na wala halizunguki,ni kwa nini hadi sasa aya hiyo iko imesalia katika Kurani?Je,ni nani anasema uongo kati ya Mungu na wanasayansi juu ya suala la Jua?

Karibu kwa mjadala ili tupate kujua ukweli kwa faida ya maendeleo ya Dunia yetu.
Marehemu Muhammad sijui alikuwa anapuliza Cha Arusha?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom