Mtume Muhammad: Jamii isipotoshwe; Jua huzama katika Chemchemu ya matope Meusi na Mazito

Status
Not open for further replies.
Ukijibiwa bado utauliza kwanin kawafanya wengine matajiri na wengine maskini badala ya wote kuwa sawa
 
Ukijibiwa bado utauliza kwanin kawafanya wengine matajiri na wengine maskini badala ya wote kuwa sawa
Matajiri na maskini wapo kwa sababu Mungu hayupo.

Angekuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kila mtu angekuwa tajiri na umasikini usingejulikana.
 
Je sio kwamba kifo kipo kwa ajili ya kubalansi dunia!!!! To create life a life must be taken
 
Yap atleast ni hvyo ukiwa pwani ya bahari nyeusi muda wa machweo ya jua kwa mtu asiejua rotation anaona kama linazama kwenye hayo maji meusi na ndo lengwa kuitwa matope meusi
 
hahaaa " na kwanini ashike upanga kwani walkuwa wanakwnda vitani ?
 
Je sio kwamba kifo kipo kwa ajili ya kubalansi dunia!!!! To create life a life must be taken
Mungu alishindwa kuumba dunia ambayo haina kifo na haikosi balance?

Tatizo moja ninaloliona hapa ni kwamba watu wanajifunga katika ulimwengu uliopo.

Wakati habari za Mungu zinasema ana uwezo wote.

Sasa kama ana uwezo wote, maana yake aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna kifo na una balance.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo (ambao hau contradict nature yake ya upendo) akaumba huu ambao una vifo vingi sana, vingine vya kikatili kwa watoto wadogo (hili lina contradict nature yake ya upendo).

Huyo Mungu kwa nini mkatili na anajipinga mwenyewe nature yake hivyo?

Yupo kweli?

Au katungwa na watu tu?
 
Je hujui kuwa sehemu yoyote ambayo hakuna sheria na taratibu ujue hakuna maisha pia
Unaelewa kwamba sikatai sheria. Nakataa Mungu kujipinga nature zake za msingi?

Unaelewa kwamba dhana ya Mungu anayejipinga nature zake za msingi pia inavunja sheria ya logical consistency?

Unaelewa kwamba ukishasema Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakuna sababu yoyote iliyo na logical consistency na natures zake hizo ya Mungu huyo kuumba dunia anbayo mabaya yoyote yanawezekana?

Unaelewa kwamba kuwezekana kuwepo kwa mabaya yoyote katika ulimwengu huu kunaonesha Mungu huyo hayupo?
 
Umeandika maneno mengi lakin pumba....kinachokusumbua wewe na wengine wengi ni tafsiri kaa ukijua kiswahili ni lugha ambayo hajajitosheleza kwa maneno kuna vitu vingi hajitafsiriwa inavyotakikana kutokana na uchache wa kisamiati sio Quran tu hata kwenye bible...sasa kilichopo kwenye hiyo sura Allah ametumia neno maghirib...maghrib linamaana ya kuchwea, au kuelekea mwisho wa kitu au kureflect....maana zote zinafit kwa alichokisema Allah kuwa Dhur alifika eneo muda jua kutuama likiwa lina reflect miale yake kwenye tope sio jua kuzama kwenye tope maana ya hapa Allah alizungumzia nyakati...halafu ni mtu tu umeamua kujitoa akili ni Aya ngapi Quran imezu gumzia jua na muzunguko yake had ambayo sayans mwanzo ilituambja jua halizunguki zinazunguka sayari zingine(kama.ambavyo wewe bado unaamini sababu hutafuti unapenda kulishwa maneno ya upotoshaji) ila Quran imesema jua linazunguka na baada ya sayans kupiga hatua wakagundua jua huchukua siku 26 kumaliza mzunguko wake kuna kitu wanaita black dot kwenye mzunguko wa jua ambayo jua huchukua siku 26 kuifikia ile dot Quran imesema hayo, Quran imezungumzia The big bang kwenye surah ambiya, Quran inazunguzia embriology ambayo hatua za ukuwahi wa binadamu ambazo huwez kuziona kwa macho ya kawaida had microscope ambayo by the time haikuwepo..na ndio maana Allaha kasema mara nyingi hichi ni kitabu kwa watu wenye akili wenye kufikiri...unatakiwa usome sana wengi wenu mnatatizwa na tafsri na mnafata vitabu vya wazungu na wao walivhemka tafsiri au wanapotosha makusud sababu ukiandika kitabu against islam kinapata biashara kubwa sana haswa kwa ulaya na america.!

Allah amezungumza kuchomoza na kuchwea kwa jua ili tuekewa kwasababu ndivyo tynavyozungumza sisi wanadamu ikiwe hata wana sayansi wanatumia neno sun set and sun rise lakin je jua huchomoza?? Jua linaonekana na kupotea kulingana na mzunguko wa dunia.. ALLAH amesema ni yeye ndio analiwezesha hilo mchana ku overlap kiza na kiza ku overlap mchana na akase hii ni kwa watu wenye akili..!

Hich ni kitabu kisicho na shaka ndani na Allah amema "mnasema kitabu hichi kaandika Muhammad basi leten japo mfano wake" pia akajitamba leten japo mfano wa sura moja na kisha akasema leten mfano wa aya kumi na baadae akasema leten mfano wa aya moja...sababu structure ya Quran hajazaliwa mwanadamu wa kuiweka vile ilivyo nikipata muda nitawaletea mada ya muujiza wa Quran kinamba.!
 
Pangoni Hira, Muhammad alikuwa peke yake, unafikiria kutakuwa na shahidi gani tena mkuu? Ukilazimisha sana jambo hilo utaletewa Mijusi,Buibui,kenge na Nge tu.
hahaaa halafu akajiwekea defense mechanism kwamba mtu yeyote atakaye mpinga mtume basi amelaaniwa " means hata ukiona amekwambia uwongo uukubali tu '' Kama huo uwongo wa jua kuzama kwenye matope
 
mate unauwezo mkubwa Sana wakujibu na kujenga hoja aiseee
 
Mpaka sasa watu wanasema mengi sana kuhusu Mungu.

Lakini hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuthibitisha kwa namna isiyojipinga kimantiki kwamba Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
Thibitisha wew kwamba hayupo
 
Hujamalizia....hapo hapo bado pia Mungu ni mwingi wa kusamehe
 
Mkuu umenifanya nikufollow bila kutarajia...you're truly a great thinker...mie napenda kusoma na kufuatilia watu wenye mawazo kama hayo and not otherwise...usiniangushe next tym mkuu...big up sana
 
wewe unaushahidi gani " kuwa muhhamad " hakuwahi kusema uwongo " Kama unahuo ushahidi leta hapa "
 
Hujamalizia....hapo hapo bado pia Mungu ni mwingi wa kusamehe
Contradiction.

Atamsamehe vipi mtu ambaye kamfunga macho na masikio na kamfanya moyo wake uwe mgumu na kakataza watu wasishughulike naye?

Swali langu la msingi hujalijibu.

Kwa nini Mungu wa rehema anawafunga watu mioyo wasimjue badala ya kuwasaidia wamjue?
 
[emoji106] [emoji106]
 
Soma ujihakikishie mwenyewe tujadili hapa.

Ukiniuliza mimi halafu nikakudanganya, kama hujasoma utajuaje?

Au kama nimeelewa vibaya nikakupotosha, utajuaje?

Soma na wewe utoe chako kutokana na ulivyosoma.

Usisubiri kutafuniwa na mtu.
Mimi huwezi kunidanganya kwani siwezi amini bila my own proof. Na wala sihitaji wewe uniambie. Unachotakiwa uwe na proof yako mwenyewe sio ya kuendelea kushikiwa akili na ngozi nyeupe. PROVE BIG BANG THEORY TOFAUTI NA HAPO HUNA TOFAUTI NA WAFUASI WA MUHAMMAD AU YESU
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…