Kiranga
naona hoja hapa ni logical consistency. Je kutokuwepo kwa hiyo consistance kuna fanya kutokuwepo kwa Mungu wa Koran au Biblia? Mimi naamini ktk Mungu wa biblia lakini siamini ktk logical consistency yake hasa nikizingatia kuna vipindi vya uongozi wa Mungu ambavyo sheria na taratibu zinabadilika.
Ukitafuta ushahidi wa ki fact ktk biblia utaukosa ila wa Truth utapata.
Kwa Mungu Truth matters sio FACT
Ukikataa logical consistency, umekataa lolote kuwa na maana yoyote. Umeelewa hili?
Yani, logical consistency ndiyo kitu kinacholeta maana ya kitu chochote chenye maana.
Kwa nini?
Hebu tuseme utupilie embali logical consistency. Uamini Mungu yupo bila logical consistency.
Hili maana yake ni nini?
Maana yake ni kwamba, kuamini kwako Mungu yupo bila logical consistency hakuna maana.
Kwa sababu, ukisema unaamini Mungu yupo, halafu huamini katika logical consistency, ni sawa na umesema kuamini Munguyupo ni sawa na kuamini Mungu hayupo. Kwa sababu, kinachotenmganisha kuaminiMungu yupo na kusema Mungu hayupo ni logical consistency.
Ukisema huamini katika logical consistency, maana yake ni umesema kwamba kuamini kwamba Mungu yupo na Mungu hayupo nisawa. Na ukisema kwamba kuamini Mungu yupo na kuamini Mungu hayupo ni sawa, ukisema unaamini Mungu yupo, ni sawana usema unaamini Mungu hayupo.
Kuamini Mungu yupo, bila kukubali logical consistency, ni kuamini Mungu hayupo.
Ni kuamini Mungu yupo na hayupo kwa wakati mmoja.
Ni kuamini kwamba kusema Mungu yupo au hayupo vyote ni makosa na ukweli upo nje ya vyote viwili hivyo.
Nivurugu zote unazoweza kuzifikiria, kwa tofauti tofauti zake zote kirejareja, na kwa kuunganishwa kwake zote pamoja.
Nakupa mfano wa hesabu, kwa sababu hesabu kwangu huwa zinakata mjadala na zinaonesha mambo kwa uwazizaidi.
Huwezi kusemaunaweza kuvuruga hesabu ndogo tu, kwa mfano uvuruge 1 =1, useme 1=2, halafu ufikiri kwamba vurugu hiiitaishia hapo tu.
Vurugu hii itaharibu number line nzima. Kwa sababu, ukishasema 1=2, hapo ukizidisha kila upande kwa 2 umesema pia kwamba 2=4, lakini, kwa sababu 1=2, na tumeona 2=4, ukiibadilisha hii 2 ya 2=4 ukaifanya iwe 1 (kwa sababu 1=2) utapata 1=4. Ukizidisha pande zote kwa 2 unapata 2 = 8, lakini tukishakubali kwamba 1=2, tunaweza kuiondoa 2 ya 2=8, tukaweka 1 badala ya 2 na kupata 1= 8.
Pretty soon tutajikuta tuna number line ambayo kila namba ni sawasawa na kila namba nyingine na hivyo hiyo number line haina maana.
Wewe unachosema ni kwamba, unaweza kuondoalogical consistency halafu mabo bado yaka make sense. Kwamba unaweza kusema 1=2, halafu hukokwingine kusiathirike na hilo.
Wakati kiukweli nikwamba, ukiondoa logical consistency, umeharibu maana ya maana, ukishakubali 1=2, hujaondoa maana ya 1= 2 tu, umeondoa maana ya namba zote.
Ndiyo maana katika mazungumzo yangu huwa nashikilia sana logical consistency.
Ukiiondoahii, siyo tu huwezi kupata maana, umeondoa hata maana ya maana.