Mukuli Bokera! nikupe kweli hii baada ya miaka.500 Kaja Muhammad ibn abd allah akaanza kusimulia kwamba nimefunuliwa na Mungu kwamba kulikuwa na isa ibn mariam mjukuu wa Imran hawakumsulubu wala kumuua! Unamuelewaje?
Kwani Biblia inasemaje?
Mathayo anatufahamisha katika Injili yake:
"Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia, kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. (Mt. 12:38-40) (Rejea Yona 1:15 –2:1).
Kwa maelezo haya ya Yesu ni kwamba hatakufa kama vile ambavyo Yona hakufa, ila atakaa kaburini siku tatu, mchana na usiku kwa kila siku, na hivyo kusingekuwa na ufufuko. Lakini Mathayo anaeleza katika 27:45 – 28:1-6 kwamba Yesu alikufa, akazikwa kisha akafufuka. Kanisa nalo linafundisha kwamba Yesu alikufa Ijumaa jioni na akafufuka Jumapili alfajiri, yaani kukaa kaburini siku moja na nusu tu.
Bado kuna hitilafu nyingi kuhusu mwisho wa Yesu baada ya kukamatwa.
Kwa mfano, Marko anasema Yesu alisulubiwa saa tatu asubuhi (Mk. 15:25) lakini Yohana anasema alisulubiwa baada ya saa sita mchana (Yn. 19:14).
Luka anapingana anaposema kwamba Yesu alipaa siku ile ile aliyofufuka (Lk. 24:13-51).
Lakini katika kitabu chake cha Matendo ya Mitume akaeleza kuwa alipaa siku ya arobaini baada ya kufufuka (Mdo 1:1-12).
Licha ya hayo, hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kama Waandishi wa Injili nne walikuwa watu wa kutumainiwa na walioongozwa na Mungu. Kwa mfano, Biblia Takatifu, Agano Jipya, UBS 1990, inaeleza katika uk. 13 "utangulizi wa Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo":
Injili ya Mathayo haisemi chochote kuhusu mtungaji wake. Kadiri ya mapokeo ya zamani, Mathayo mtoza ushuru na mmoja wa Mitume kumi na wawili aliandika maneno ya Yesu katika lugha ya Kiaramu. Bahati mbaya mtungaji wa Injili yetu ya sasa aliyeandika katika lugha ya Kigiriki (ambaye habari zake maalum hatuna) aliongozwa na mawaidha ya Mathayo, mfuasi wa Yesu).
Na kuhusu Injili ya Luka tunaelezwa:
Kadiri ya mapokeo ya zamani Injili ya tatu imeandikwa na Luka aliyezaliwa Antokia akawa Daktari. Alikuwa mpagani (au wa asili ya mazingira ya Kigiriki) si Myahudi kama walivyokuwa akina Mathayo, Marko na Yohana (Uk. 84 wa Biblia hiyo hiyo).
Nayo Biblia Takatifu T.M.P. Book Department Tabora, 1967, uk, 911 inaeleza kwamba Marko hakuwa mwanafunzi wa Yesu, na Injili yake ni muhtasari wa mafundisho ya Petro. Na ama Injili ya Yohana inajishuhudia yenyewe kwamba waandishi wake ni wengi na wala hawafahamiki:
Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. (Yn. 21:24).
Na hii ikawa ndio sababu ya wasomi wa juu wa Kikristo kusema kwamba mwandishi wa Injili hii sio Yohana, huenda labda ni wanafunzi wake (Dictionary of the Bible, John Mackenzie; 1981 maelezo kuhusu Injili ya Yohana).
Napenda kukufahamisha kwamba utupe hoja kuthibitisha kwamba itikadi unayoitetea haikujengeka juu ya dhana.
Pia kwa Waislamu kupinga kifo cha Yesu sio kumpinga Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu hajasema mahali popote kwamba Yesu kafa.
Hayo ni madai ya watu wasiofahamika (kwa wanahistoria wa Kikristo na Wakristo wenyewe) pamoja na Wapagani.
Tuzingatie tahadhari aliyoitoa Mwenyezi Mungu katika Qur’an Tukufu:
Basi adhabu kali itawathibitikia wale wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema, "hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu". (Wanasema uwongo huo) ili wachukue thamani ndogo ya kilimwengu. Basi ole wao kwa yale walivyoyaandika kwa mikono yao (wakasingizia kuwa ya Mungu). Na ole wao kwa yale wanayoyachuma. ( Qur’an Tukufu 2:79).